Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 18,173
- 27,223
Habari wana JF,
Poleni kwa wote ambao matokeo yamewaumiza.
Ipo hivi, kwenye mambo kama haya kuna kushinda na kushindwa hivyo ni vyema tukapunguza hasira na kuangalia tunafanyaje kwenye chaguzi zijazo.
Ila natoa rai kwa wana Chadema wenzangu, tupunguze ujuaji, matusi, kebehi na dhihaka za kila namna.
Kabla ya matokeo wengi tuliona humu jinsi maneno yetu yalivyo makali, tujirekebishe hapo.
Ninatoa rai kwa chama kujipanga kwa ajili ya 2025, kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi.
Mipango isukwe vizuri na pia kweli tuwe na nia ya kushika dola. Mara kadhaa humu nilikuwa nikishangaa tunawezaje kushinda uchaguzi kama huu ikiwa ni kama tumekurupushwa tu? Nikaishia kutukanwa kila aina ya tusi. Yote kwa yote tujipange, kwenye kushika dola hakuna shortcut.
Mwisho, ninamuomba Mh. Rais Magufuli akiona inafaa ampe ubunge wa viti maalum(vile 10) Mh Mbowe. Mbowe anaweza kuchaguliwa hata kama yupo Chadema, ishawahi kutokea kwa Mbatia.
Hivyo kwa unyengekevu ninamuomba Mh. Rais amteue Mbowe kuwa mbunge wa viti maalum.
Nawasilisha