CHADEMA tujipange kwa ajili ya 2025, hatujachelewa

CHADEMA tujipange kwa ajili ya 2025, hatujachelewa

Kamanda lissu kasema tuandamane, vipi mbona hamtokei?
nalishangaa hili gasho msosi wa polepole linajifungamanisha na chadema badala ya kupepea mmewe kitambi kwa mafanikio waliyopata!
 
Kajazaneni bungeni mlete maendeleo. Imeisha iyoo
 
Hivi ili tume iwe huru Nani anatakiwa kuiunda au inakuaje
 
Pole sana, sina mihemko kama weee. Huonj hapo ulipo unavyougulia maumivu kwa kusubiria visivyowezekana?
Pole, najitolea kukununulia pain killer
nalishangaa hili gasho msosi wa polepole linajifungamanisha na chadema badala ya kupepea mmewe kitambi kwa mafanikio waliyopata!
 
Sio tujipange :tunataka mpaka hiyo 2025 kwa kua mmeshinda nchi nzima Tanzania iwe Kama Dubai msije na visingizio tena kua upinzani ndio wanasababisha msilete maendeleo panya nyie ccm.
 
Huu ni uchaguzi wa mwisho wananchi kupoteza muda wao kwenda kujiandikisha na kupiga kura.
 
Mbowe apewe viti maalum vya msaada kwa shida gani aliyonayo?!

Unataka wapate sababu ya ku justify wizi wa kura walioufanya?

Never.
 
Kamanda saa ngapi tunaingia barabarani? Lissu kishatoa tamko
Mbowe apewe viti maalum vya msaada kwa shida gani aliyonayo?!

Unataka wapate sababu ya ku justify wizi wa kura walioufanya?
 
Habari wana JF,

Poleni kwa wote ambao matokeo yamewaumiza.

Ipo hivi, kwenye mambo kama haya kuna kushinda na kushindwa hivyo ni vyema tukapunguza hasira na kuangalia tunafanyaje kwenye chaguzi zijazo.

Ila natoa rai kwa wana Chadema wenzangu, tupunguze ujuaji, matusi, kebehi na dhihaka za kila namna.

Kabla ya matokeo wengi tuliona humu jinsi maneno yetu yalivyo makali, tujirekebishe hapo.

Ninatoa rai kwa chama kujipanga kwa ajili ya 2025, kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi.

Mipango isukwe vizuri na pia kweli tuwe na nia ya kushika dola. Mara kadhaa humu nilikuwa nikishangaa tunawezaje kushinda uchaguzi kama huu ikiwa ni kama tumekurupushwa tu? Nikaishia kutukanwa kila aina ya tusi. Yote kwa yote tujipange, kwenye kushika dola hakuna shortcut.

Mwisho, ninamuomba Mh. Rais Magufuli akiona inafaa ampe ubunge wa viti maalum(vile 10) Mh Mbowe. Mbowe anaweza kuchaguliwa hata kama yupo Chadema, ishawahi kutokea kwa Mbatia.

Hivyo kwa unyengekevu ninamuomba Mh. Rais amteue Mbowe kuwa mbunge wa viti maalum.

Nawasilisha
Mbowe asipewe ubunge hata kidogo akipewa ubunge atasahau kazi ya kujenga chama
 
Mimi sijaona mwananchi hata mmoja aliyetii agizo la kubaki na kulinda kura.
 
Back
Top Bottom