CHADEMA tafadhali nawaomba... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA tafadhali nawaomba...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyamgluu, Mar 2, 2011.

 1. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.
   
 2. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mdau-Hebu tuibie sili hata punje tujue pa kanzia. Maana hata Waislam Original(Egypt, Libya.....Etc) wana-protest bad leasdership sasa hawa wa TZ wanayapi.
   
 3. S

  Shauri JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haswaaa!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nyie watu wekeni mambo hadharani...ninini mnachoongelea?
  Kama mnaamua kuposti mtandaoni mnapaswa kuweka hapa hali hiyo mnayoongelea kuwa ni hatari kwa taifa!
   
 5. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  unachosema mkuu ni kweli lakini ungejaribu kuweka wazi tuelewe ni nini huyo Ustaadh alikuwa anasema, nina uhakika kabisa ndugu yangu kuna mengi umeyasikia ambayo ukiyaweka hapa itakuwa ni msaada mkubwa sana wa kuwatoa gizani wenye mawazo na fkra za kama huyo ndugu.
  Note: jumapili moja nilikuwa mitaa fulani hapa stone town (Zanzibar) ambako ni ngome kuu ya CUF walikuwa wanajadili ishu nyingi ikiwemo maandamano ya CHADEMA; walikuwa wanasema CHADEMA wanataka kuleta vita maana tayari kuna majeshi wameshakodi yatakuja kuanzisha vurugu ndio CDM maana wanapita sehemu mbalimbali kuhamasisha vijana ili washirike katika vita na machafuko vile vile hawakusita kuonyesha chuki yao kwa Dr Slaa Mdini, roho mbaya, mbaguzi waliongea mambo mengi s
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  naanza hisi harufu ya damu hapa..........!!
   
 7. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Wadau unajua tatizo la topic kama hii ni watu kuingiza udini na kuanza kupondana na kudharauliana kwenye maswala ya IMANI.
  Ila la ni hivi: mimi nilikaa na huyu ndugu yangu mwenye MBA na anaaminika sana kwenye jumuiya ya waislam hapa nilipo kama msomi. Katika maongezi nikawa naipamba CDM na Slaa akanisikiliza kama 30
  mins hivi. Halafu akaanza kuongea. Si wezi kuyaandika yote kwa ufasaha kwasbabu niko 'via mobile' lakini hata mimi nili pull back na kufikiri labda ni kweli. Waislam wanaanza kukosa nguvu ya kusuport CDM. Ngoja niweke 1 point at a time: Aliniuliza Nyamgluu on a personal level nani aliejilimbikizia mali zaidi kati ya mkapa na kikwete. Kagoda,majumba,mahoteli, mashamba mkapa na mke wake anna wana mabiashara na nyumba hadi nje ya nchi. Kikwete hajajilimbikizia mali kama Mkapa,ila kuna forces zenye nguvu zinazochangia Kikwete kuonekana mbaya. (ngoja niwashe PC kidole gumba kinauma)
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  JK kachochea udini na umekubali.hana hoja ya kuwaambia watu wamsapoti zaidi ya kusema wakristo wanamchukia hivyo waislamu wamsapoti.Tusipotofautisha maslahi ya taifa na dini zetu tumekwisha.
   
 9. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Lakini 4get it tutaingia kwenye udini. Cha muhim ni CDM kuingiza waislam na waonekane. Ikiwezekana hata mnyika,zitto au mbowe a silim nakua muislam.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,968
  Trophy Points: 280
  ..kitakachotuunganisha wa-Tanzania ni UGUMU WA MAISHA chini ya utawala wa CCM.

  ..hivi hukuona kule Egypt jinsi Muslim Brotherhood na Coptic Christians walivyoungana kumuondoa Mubarak??
   
 11. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Jokakuu kuturinganisha waTZ moja kwa moja na Egyptians sio sahihi our situations are very different.
   
 12. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa watu wenye akili kama hizi, Hatutaendelea kama taifa but only kama mafisadi!
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Hizo ni propaganda na mawazo ya kijinga. Haitoshi tu kusema chama fulani wana udini bila kuelezea udini wao ulivyo; na kwa ujinga wetu tunaingia kichwa kichwa kwa maneno ya kutungwa bila kufikiria. Kama udini unapimwa kwa kuangalia dini za viongozi na wanachama au maeneo ambayo chama kina wafuasi na wabunge/wawakilishi wengi basi chama cha kidini hasa ni CUF halafu CCM then vingine vinafuatia. Hilo liko wazi na wala halihitaji mjadala. Huyo Mtatiro (kama si mwislamu) kawekwa pale kama kanyaboya tu.

  Lakini hata hivyo tunajadili na kuchochea udini ambao kimsingi haupo kwa malengo gani na kwa faida ya nani au nini? Hivi viongozi wote kwenye chama wakiwa waisam au wakristo au dini yoyote then? Inakusaidia nini? Tunachohitaji ni uchapakazi wa mtu bila kujali dini yake hata kama wote wangewa wa dini ile.
   
 14. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Gad ONEYA, wakati natafuta leseni ya udereva nchi fulani kuna ushauri unapewa kuwa kuendesha kwa usalama sio tu kuzingatia sheria barabarani lakini kujiepusha na machizi wasiozingatia sheria barabarani. Hivyo pia hatuwezi kusema tu hao wanaofikiri hivyo basi wanasapoti mafisadi, ni busara kuona their point of view na ku formulate jinsi ya kuepuka matatizo hayo,kama kweli wana nia nzuri na nchi. Ignoring the problem wont make it go away,it actually builds the problem.
   
 15. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Kutoa hoja kwa nguvu hakuondoi tatizo. Unasema ni propaganda za kijinga,sawa,ila akili ni kukubali kuwa zipo na kujenga njia za kupambana na hizo propanda za kijinga sio kufoka foka tu kama wewe hapo. NOT EVERYONE SEES THE OBVIOUS KAMA WEWE. Common sense is not common broda!
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Haya mambo ya kuangalia dini ya mtu sipendi kweli. Ila anyway if I may go down to those people's level for a minute hivi Zitto si ni Muislamu? Au kwa sababu hana majina ya Kiislamu?
   
 17. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,063
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka wajaziwe watu wa dini yao ili kuwafurahisha? For sure hata ukifanya hivyo yatazushwa mengine na ndivyo propaganda zilivyo; ukifanya hivi linazushwa lile; ukifanya vile linazushwa lingine endlessly; tena hayo mawazo ya religious balancing ndio unataka kuleta balaa la ajabu - ukijaza Sunni itazuka nchi hii wengi ni Shia; ukiongeza Shia itazuka Kadian tumesahauliwa; ukijaza Katoliki; Lutheran tumesaulika; n.k. n.k. Suala muhimu ni kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoangalia dini, kabila, jinsia, n.k. kwenye masuala ya kitaifa bali uwezo wa mtu.
   
 18. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Mwanafalsafa1 nami udini naona ni jambo low sana. Kwanza kwasbabu haliwezi jadiliwa logically or by proving ni swala la kuamini bila vithibitisho 'halisi'.
  Tatizo kuna wengi wako tayari kuua na kufa kwa ajili ya imani,as ridiculous as that is ni muhim kukubali kua yapo maana ni kweli na kuona ni jinsi gani CDM kinaweza epusha janga hili kwa taifa coz it is our ONLY HOPE!
  Dudu hio elimu tunawepeje wanayohitaji?
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Kwa kiasi kikubwa naweza kuunga mkono hoja ya mtoa mada, kwa nchi kama Tanzania ambapo asilimia kubwa ya Raia wameleweshwa Dini ni busara kwa uongozi wa chama chochote au kiongozi yeyote kuwa makini katika namna ya ku-organize mambo ili kuepusha malalamiko kutoka upande wowote. Kwa kifupi huwa ni ngumu na inakera pale unapojaribu kutetea haki za watu bila kujali itikadi zao za kiimani na kikabila, lakini mwisho wa siku bado ukapata malalamiko kutoka upande mmoja kwamba unapendelea upande mwingine.

  Hivyo ni baadhi ya vizingiti ambavyo chama/kiongozi yeyote atakumbana navyo kwenye kutekeleza majukumu yake. Cha muhimu kufanya ni kutafuta solution ya haraka kabla hii sumu haijaenea zaidi. Wakati mwingine huwa naamini kuwa sisi watanzania tu wavivu wa kufikiri na hatupendi kushughulisha akili zetu kutafakari mambo, kwa mantiki hiyo huwa ni rahisi sana kwa mtu kupotoshwa na mtu yeyote atakayeamua kupotosha pale anapoonekana kuturahisishia mambo, hasa hawa wanaojiita/wanaoitwa viongozi wa dini aidha kwa makusudi (kulinda maslahi) au kwa bahati mbaya (kwa uelewa wao mdogo).

  Tukirejea kwa walengwa, nashauri ninyi wana-CHADEMA mliopo humu ndani, mchukue ushauri wa mtoa mada na mara moja muanze kueneza Propaganda misikitini na kwa waumini wa Uislamu kuwa ukombozi wa Mtanzania hauna uhusiano wowote na CHADEMA kama chama bali unawahusu watanzania wote. CHADEMA wanatekeleza jukumu lao kama sehemu ya watanzania, wengine nao watekeleze kwa upande wao, mradi lengo ni moja, basi tusihitilafiane bali tupeane moyo na ushauri pale mmoja atakapohitaji. Iwepo au isiwepo CHADEMA, ni lazima mtanzania akombolewe kutoka kwenye makucha ya wanyonyaji wachache. Uislamu na Ukiristo ni imani zenu, ziheshimuni, zipo, zilikuwepo, na mtakufa mtaziacha, tuweke imani zetu kando pale tunapodai maisha mazuri, huduma bora za afya, punguzo la bei za sukari, nauli na mchele, kuondoa kero za foleni za magari, kuchelewa kwa mishahara pamoja na kero mbali mbali ambazo zinachangiwa na uongozi wetu kutupuuza waislamu na wakristo na wapagani wa Tanzania. Waambieni kuwa akina mama wajawazito wanaokufa kwa kukosa huduma za afya ni waislam na wakiristo kwa pamoja, vibaka waliopoteza matumaini wanakaba watu wote kwa pamoja, masheikh na wachungaji. Waambieni wakati yote hayo yakitokea Viongozi wao wakuu wa dini wanapewa huduma zote muhimu na Serikali, hawabugudhiwi!!!
   
 20. p

  politiki JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  uwezi kutafuta solution ktk tatizo ambalo haliko mjomba, udini hakuna hizi ni siasa tu waislamu na wakristo wananishi kama ndugu hao wanaoidai kuna udini ni wanasiasa uchwara kama kikwete ambao wanatumia udini kujipatia kura. mashekhe wengi wanaoubiri udini wakati wa uchaguzi ulipwa na wausika kwa ajili ya kufanya kazi hiyo lakini hawawaambiii wanaowaubilia kuwa wamechukua pesa mfano mzuri ni shekhe Halifa wa kariakoo ni maarufu kwa kazi hiyo. ukitaka kujua anachokisema KIKWETE NI PUMBA fikiria kwanini hawachukulii hatua watu anaodai kuwa wanaeneza udini, yeye kama raisi anayo mamlaka makubwa ya kisheria kwanini hawachukulii hatua anakaa pembeni kulalamika kama mwananchi wa kawaida? mdini ni yeye JK akienda kusini anailalamikia CUF kuna udini akienda Kaskazini analalamikia CHADEMA. alipokuwa Lindi aliuliza kwenye mkutano wa hadhara aliwalalamikia CUF kuwa wana mbagua kwani yeye ni john?, hebu fikiria kwahiyo John ndio anastahili kubaghuliwa JK ndiye MDINI MKUBWA na siyo watanzania wengine.
   
Loading...