CHADEMA tafadhali nawaomba...

CHADEMA tafadhali nawaomba...

Sasa mkuu si ungetuambia hayo uliyoyasikia, kwa sababu hiyo taarifa hata haitusaidii hapa big thinkers forum.
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.

Nyamgluu sijakuelewa unataka nini hasa kwenye hii thread yako.
CDM watafute MUISLAMU VOCAL hata wa KUNUNUA...!!???Huyu MUISLAM ni wa nini na kwa ajili gani???
Ninachoelewa mimi mpaka sasa kuna WAISLAMU ndani ya CDM tena wengi tu na wanakipenda chama. Kwa mfano wazi na rahisi kuonekana ni ZITTO ZUBERI KABWE(Muislamu halisi). Sasa unaposema CDM watafute waislamu wa kununua yaani SIKUELEWI ndugu yangu.

Wewe unaonekana una ajenda yako ya SIRI yak kuataka kuonyesha kuwa CDM ni chama cha WAKRISTO watupu kitu ambacho ni UONGO WA MCHANA KWEUPE.

CHADEMA kwa sasa ni CHAMA CHENYE NGUVU,MVUTO NA USHAWISHI MKUBWA SANA KWA WATANZANIA.
CHADEMA ni CHAMA CHA WATU WOTE yaani rangi zote,kabila zote na dini zote(Wakaristo,Waislamu na Wapagani.
 
unachosema mkuu ni kweli lakini ungejaribu kuweka wazi tuelewe ni nini huyo Ustaadh alikuwa anasema, nina uhakika kabisa ndugu yangu kuna mengi umeyasikia ambayo ukiyaweka hapa itakuwa ni msaada mkubwa sana wa kuwatoa gizani wenye mawazo na fkra za kama huyo ndugu.
Note: jumapili moja nilikuwa mitaa fulani hapa stone town (Zanzibar) ambako ni ngome kuu ya CUF walikuwa wanajadili ishu nyingi ikiwemo maandamano ya CHADEMA; walikuwa wanasema CHADEMA wanataka kuleta vita maana tayari kuna majeshi wameshakodi yatakuja kuanzisha vurugu ndio CDM maana wanapita sehemu mbalimbali kuhamasisha vijana ili washirike katika vita na machafuko vile vile hawakusita kuonyesha chuki yao kwa Dr Slaa Mdini, roho mbaya, mbaguzi waliongea mambo mengi s

crap !
 
Jamani mi naogopa, vita iskie kwa nchi jirani ndugu zangu, i wish mgekuwepo kwenye vita au mauaji ya kimba' au burundi na kongo enzi za wanyamurenge guyz si kitu cha kuomba, inatisha acheni tu.

Kama unaogopa hama ndugu yangu, utakuja tukishawatoa hawa nchini
 
Kimsingi hizo propaganda zipo lakini suluhisho haliwezi kuwa hilo la kumtafuta muislam.
Mbona zitto ni muislam,,,,,,,halafu hapa mbona wote ni great thinkers na tunaelewa kuwa hizi ni propaganda, tatizo ni namna ya kuziondoa miongoni mwa hao wenzetu wengine.
Au mmeshasahau ile slogan ya" divide and rule?"
 
Wadau unajua tatizo la topic kama hii ni watu kuingiza udini na kuanza kupondana na kudharauliana kwenye maswala ya IMANI.
Ila la ni hivi: mimi nilikaa na huyu ndugu yangu mwenye MBA na anaaminika sana kwenye jumuiya ya waislam hapa nilipo kama msomi. Katika maongezi nikawa naipamba CDM na Slaa akanisikiliza kama 30
mins hivi. Halafu akaanza kuongea. Si wezi kuyaandika yote kwa ufasaha kwasbabu niko 'via mobile' lakini hata mimi nili pull back na kufikiri labda ni kweli. Waislam wanaanza kukosa nguvu ya kusuport CDM. Ngoja niweke 1 point at a time: Aliniuliza Nyamgluu on a personal level nani aliejilimbikizia mali zaidi kati ya mkapa na kikwete. Kagoda,majumba,mahoteli, mashamba mkapa na mke wake anna wana mabiashara na nyumba hadi nje ya nchi. Kikwete hajajilimbikizia mali kama Mkapa,ila kuna forces zenye nguvu zinazochangia Kikwete kuonekana mbaya. (ngoja niwashe PC kidole gumba kinauma)
Katika kashfa ya Kiwira BankM, EPA nk. Dr Slaa (Mkatoliki) alimshikia sana bango Mkapa (Mkatoliki) ili avuliwe hiyo kinga na ashtakiwe, lakini ni JK aliyeshindwa kuchukua hatua stahili. Sasa alaumiwe nani? Slaa au JK.
Hapa si swala la udini, ni sula la JK kutochukua hatua; na si katika hili tu! WaTZ - amka!
Unajua shida ni waislamu kufikiria kuwa kikwete ni mtawala wa kiislamu; siyo, hii ni secular state rais hatawali kwa dini yake
 
My fellow Tanzanians; CCM have succeeded to Devide us! Sipendi kweli kujadili udini maana mimi ni mkristo
lakini 80% of my friends are not christians, this is the life I am used to! Kujadili udini kwenye hii nchi hakutaondoa ugumu wa maisha yetu kama watanzania, na hizi ni dalili za kufilisika kimawazo na kifikra. Jamani watanzania nataka mtambue kuwa kwenye siasa hatutafuti kiongozi wa kutuongoza kwenda peponi, hao tunao kwenye misikiti yetu na makanisani; tunatafuta mtu mwenye uwezo wa kuongoza nchi hata kama hana dini! kujadili dini za viongozi wetu hakuleti tija yoyote wala hakuta punguza makali ya maisha yetu; ila kujadili udini wetu kuna maslahi makubwa sana kwa wale wanaotaka madaraka, maana wanaotaka madaraka hawajali namna gani yamepatika hata kama kwa kutumia dini, si kitu ilimradi kaweka kibindoni madara! Ni hatari kwasisi raia wa kawaida kujadili udini. Ni mauti yetu kujadili udini wetu! Napenda kusema kwamba hii ni mara yangu ya mwisho kujadili hoja kama hii kwenye jamii forum. Ila nitakemea kila mtu atayejadili hoja hii popote!
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.

tuweke bayana hili tuelewe!!!!
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.
Please yaweke hadharani, unaogopa nini? Ni kweli lakin tunahitaji uthbitisho!, emu ongea yote uloambiwa then tuangalie how to tackle the situation. But angalizo ni kwamba ata wafanyeje hawatofanikiwa kwani tunaye BWANA asiyeshindwa, wasjaribu kupingana na uwezo wa JEHOVAH!
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.
Please yaweke hadharani, unaogopa nini? Ni kweli lakin tunahitaji uthbitisho!, emu ongea yote uloambiwa then tuangalie how to tackle the situation. But angalizo ni kwamba ata wafanyeje hawatofanikiwa kwani tunaye BWANA asiyeshindwa, wasjaribu kupingana na uwezo wa JEHOVAH!
 
Wananpu nilwahi kuuliza humu jamvini, jee wanaoandamana ni wakristo tu?
Nashukuru kusema umati wote ule umeungana bila kujali dini wala kabila ili kupambana na dhulma wanayo fanyiwa.
Na wanaofanya dhulma hiyo ni Waislamu,Wakristo na wasio Wa dini hizo!
Wanaokuza mambo ya dini ukichunguza utaona ni vipaza sauti tu vya mafisadi ili waibemende nchi kwa raha zao.
HATUDANGANYIKI.
 
Hivi huko CDM "unaingizwa" au "unaingia" mwenyewe!!?
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.
Ndugu zangu tuache unafiki, tuache magungu, tutafute maendeleo. Chadema ni chama ambacho kipo wazi hakija wahi kutamka kitu chochote cha udini au kuweka sheria kwa ajili ya kutetea watu fulani au dini fulani. Mh ZITTO na wenzio amkeni kuwaelimisha umma kwa pamoja mfanye kazi bila kupendelea upande wowote tumechoshwa na haya maisha ya kupigika kila siku. Maendeleo ya Tanzania hayataletwa kwa ajili ya dini fulani ila ni utendaji wa watu wenyewe bila kuangali dini, kabila kanda nk.

Zanzibar wameshaanza kupambana kuendeleza uchumi wao japokuwa serikali yetu ya jamhuri ya Tanzania haijawa wazi kwa hilo. Ina maana sisi watanganyika tumelaaniwa kuwa na majungu tuuuuuu! Jamani tuache hizi fikra za uenda wazimu za udini. CHADEMA tunashukuru kimekuwa na nguvu tukisapoti nacho kijaribu kama nacho hakita leta maendeleo sisi wananchi, umma tunakitoa kinachukua kingine. Hakuna mtanzania aliezaliwa na chama ila unapenda kitu kutokana na mafanikio yake. Mtakuja kushtukia Zanzibar wameshapanda chati sisi tunapigana na maneno na siasa za kuogopana. Kama mtakubaliana na mimi kipindi cha Mkapa alikumbana na makashikashi mengi sana katika uongozi wake na hawahawa akina MBATIA ndio waliosaliti upinzani wa mkapa kwa sababu tulikuwa hatujapata wapinzani wa kweli. Sasa tumesha pata upinzani wa kweli ambao unaweza kuikosoa serikali yetu tuwaunge mkono basi. CUF ya bara msipate shida kuunga mkono CHADEMA KUELIMISHA UMMA sio waislamu tu hata wakristo.

Tunataka Tanzania yetu nayo iingie kwenye ramani ya dunia tuachane na mambo ya kutegemea misaada kutoka kwa watu wengine. Hizo ndoto tunatakiwa tuaanze kizifuta akilini mwetu na kupambana kuutokomeza huu umaskini. Tusikubali kurudi nyuma ndugu zanguni kwa ajili ya udini fulani. Yaani tunaacha kusifika kwenye mambo ya ujuzi, uchunguzi, uvumbuzi nk tunasifika kwenye mambo ya ushirikina duniani tuone aibu.
 
Tafuteni muislam vocal hata wakununua. I smell trouble. Nina ndugu yangu ustaadh ni mstaarab na mpole sana ila mambo aliyoniambia yaliyoko kichwani kwa waislam wengi ni hatari kwa taifa. Uongozi wa CDM tumieni inteligensia yenu tafadhali kwenye hili.
Inteligensia ya Chadema ni kali sana kwani ipo chini ya Dr Padri muasi aliyevaa ngozi ya kondoo.
 
Nimekubali hili TZ hakuna udini hi ni propaganda ya CCM wakamatwe basi hao wadini watu tumezaliwa mama muislam baba mkristo na hawabaguani udini uko wapi huko ni kuomba huruma wakati wewe ndo mtesaji ukombozi daima TUSIKUBALI KUGAWANYWA aluta continuaaaa!

Ndugu yangu lisemwalo lipo na kama halipo basi lipo mlangoni linakuja.

Uwe muwazi hukuona harufu ya udini wkati wa uchaguzi mkuu?
 
Msanii wetu JK anataka kuwafanya waislam kama wahutu wa Rwanda. Habyremana alipoona kuwa nchi inamshinda aliamua kuwagawia wahutu mapanga na kuwaelekeza kuwa atakapouwawa waanze kuwaua watusi. Naye Msanii wetu kaona hawezi tena kuongoza nchi na sasa anataka kutuchonganisha pasipo sababu ili tuuane wenyewe kwa wenyewe. Hivi ni familia gani au ukoo gani ambao haujachanganya dini hizi mbili, Mungu pishilia mbali. Kwani hali ya maisha ilivyo ngumu ipo kwa wakristo peke yao? Mgao wa umeme, kufeli kwa Form 4 kwa asilimia 88, kufariki kwa wajawazito, huduma mbaya hospitali, ufisadi wa kutisha na madhira mengine yanawapata wakristo peke yao. Ushabiki wa kuwa huyu ni mwislam mwenzangu hautatupeleka popote, tujiunge wote kuikomboa nchi yetu,
 
CDM is for CHURCH as CHURCH is for CDM!

Hatuwahitaji hao, tutashinda tuu!

Long Live Christian Democratic Movement (CDM)!
 
Hilli swala linaonesha ni jinsi gani wanasiasa wetu jinsi wanavyokosa kujiamini,this is NON SENSE kusema kuwa CDM kina mlengo wa kidini,mara ya kwanza kama tunakumbuka CUF kipindi ilipokuwa mwiba mkali kwa CCM walikuja na mbinu hiyo hiyo ya kusema CUF ni chama cha udini na wakadiriki hata kusema kuwa tukiwaacha waongoze serikali basi nchi itauzwa kwa mataifa ya waarabu,sasa leo CDM nae amekuwa mwiba kwa CCM tayari mmeashaanza kuzungumzia kuwa ni cha kidini,huo sio ukamavu wa kisiasa,tusizungumze kitu ambacho hakipo ndugu zangu.......kama kina udini njooni na ushahidi kamili hapa tuweze jua kuwa kweli ni cha udini lakini tu blaa blaa,ACHENI HIZO
 
Back
Top Bottom