CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

UPDATE ZA LEO MAHAKAMANI

Jaji: shahidi kiapo chako kinaendelea naamini unakumbuka ulipoishia

Wakili: Baada ya kupata taarifa kwa ma RCO wa mikoa mbalimbali nini kiliendelea

Shahidi: Hatua iliyofuata niliitisha majalada nikiwa na lengo la kusoma na kufahamu ushahidi uliopo ndani ya hayo majalada

Wakili: ni mikoa ipi na ipi?

Shahidi: Mfano mkoa wa kilimanjaro lenye KR/CIB/PE/18/2025 hili lilikuwa jalada la uchunguzi toka Kilimanjaro, Arusha Ars/CIB/PE/40/2025, Mbeya MBE/CID/PE/54/2025 pia kuna jalada lilitoka Ruvuma likiwa na kumbukumbu namba …. ambalo lilikuwa na kosa la kula njama za kuandamana
Pia kulikuwa na jalada toka mkuu wa upelelezi Kinyerezi

Wakili: Baada ya kuitisha haya majalada unakumbuka nini?

Shahidi: Baada ya kuyapokea niliyasoma

Wakili: Baada ya kuyasoma yalikuwa kwenye hatua gani za upelelezi

Shahidi: Baada ya kuyasoma tulibaini wengi waliokuwa kule walikuwa wamehamasika na kauli ya mshitakiwa na tukabaini wengi wao walikuwa wafuasi wa Chadema na wengine wachache wa vyama vingine

Wakili: Baada ya kugundua wengi wao walikua ni wafuasi kilifuata nini?

Shahidi: Nilielekeza majalada yarudi mikoani na nikaelekeza hawa watu watafutwe na waandikwe maelezo kama mashahidi.

Wakili: Waandikwe maelezo kama mashahidi kwenye kesi gani?

Shahidi: Kwenye kesi hii tuliyonayo ya uhaini jambo ambalo liletelekezwa wahusika walipatikana na wakaandikishwa maelezo

Wakili: Baada ya kupata hayo maelezo hasa wewe ulifanya nini?

Shahidi hayo maelezo yaliwekwa kama sehemu ya jalada la ushahidi dhidi ya mtuhumiwa.

Wakili: Unakumbuka nini juu ya tarehe 9/4/2025

Shahidi: Hii ndio tarehe aliyokamatwa mshitakiwa akiwa ziarani mbinga

wakili alafu baada ya kukamatwa

Shahidi: Alisafirishwa siku hiyo hiyo na kuletwa Dar es salaam na alifika kesho yake tarehe 10/04/2025 na kufikishwa kituo cha kati cha polisi alifikishwa na kusomewa tuhuma zake na mtuhumiwa alisema hakua tayari kutoa maelezo pale na alisema atatolea maelezo yake mahakamani.

Wakili: Kisha nini kikaendelea?

Shahidi: Baada ya kupata maelezo yako ofisi ya taifa ya mashtaka ya kanda ya DSM ilipofika majira ya mchana iliandaa mashitaka dhidi ya mshitakiwa na jioni ya hiyohiyo siku alifikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

Wakili: Nini kikafuata?

Shahidi: Nakumbuka baada ya kusomewa mashitaka Jalada la upelelezi lilirejeshwa kwetu kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Wakili: Nini unakumbuka kingine?

Shahidi:Tukiwa tunaendelea na upelelezi tulipokea malalamiko toka kwa baadhi ya mashahidi kuwa kuna matishio kwao iwapo wangetoa ushahidi dhidi ya mshitakiwa.

Wakili: Hao waliokua wanatoa vitisho mlibaini ni nani?

Shahidi: Wengi walikuwa ni wafuasi wa chadema tena wakitumia maneno ya kuwasalimia na kwenda mbali ya kusema waombewe mabaya wapate mikosi na laana.

Wakili: Baada ya kupokea hiyo taarifa mlifanya nayo nini?

Shahidi: Na sisi kwa nafasi zetu tuliingia kwenye mitandao na comments zenyewe zilikuwa na vitisho kwenye mitandao ya facebook, tiktok instagram na x

Wakili: Baada ya kujiridhisha...?

Shahidi: Baada ya kujiridhisha nilifanya mawasiliano na ofisi ya taifa ya mashitaka kueleza juu ya matishio hayo kwa mashahidi ili kuomba wafichwe (ulinzi)

Wakili: Nini kikafuata?

Shahidi: Baada ya hapo nilikwenda kuchukua kiapo maalumu toka ofisi ya taifa ya mashitaka ili mashahidi hao wapatiwe ulinzi

Wakili: Mheshimiwa jaji baada ya kuwauliza wenzangu hakuna swali la nyongeza.
1786387347950.jpg
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda Kuu ya Dodoma, kesho Agosti 12, 2026, inatarajiwa kuanza kusikiliza shauri namba 20581 la mwaka 2026 lililofunguliwa na Barnabas Okola pamoja na wenzake wanne dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kesi hiyo imefunguliwa na raia watano ambao ni Barnabas Okola, Joseph Mwakidasi, Mathias Cosmas, Abubakari Mashambo na Lembruce Mchome, waliotajwa rasmi kama waombaji katika shauri hilo.

Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Gaston Shundo Garubindi, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, amethibitisha kupokea wito huo wa mahakama uliotiwa saini rasmi Agosti 10, 2026.

Katika shauri hilo, wajibu maombi ni Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA (Mjumbe wa Kwanza) na Katibu Mkuu wa CHADEMA (Mjumbe wa Pili), huku Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakijumuishwa kama wajibu maombi wa tatu na wa nne.

Kwa mujibu wa ilani iliyotolewa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, usikilizaji huo utafanyika kwa njia ya mtandao (virtually) kuanzia saa 3:00 asubuhi mbele ya Mheshimiwa Jaji A. Mruma.

#SasaLive #CHADEMA #MahakamaKuu #GastonGarubindi #BarnabasOkola Sheria SiasaZaTanzania
1786445384654.jpg
 
Katibu wa Uenezi wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Felius Festo Kinimi, amesema maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa chama hicho yanaendelea vizuri, huku wanachama na viongozi wa BAVICHA kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiendelea kuwasili jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki maadhimisho hayo.

Kinimi amesema maandalizi yote muhimu yanaendelea kukamilishwa kwa mujibu wa ratiba, na kwamba ushiriki wa vijana kutoka kanda na mikoa mbalimbali unaonyesha mwitikio mkubwa wa wanachama wa BAVICHA.

Kwa mujibu wa Kinimi, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.

Amesema maadhimisho hayo yatafanyika chini ya kaulimbiu “KIJANA NA KATIBA”, ambapo vijana wa CHADEMA wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Katiba Mpya, ushiriki wa vijana katika uongozi, ajira, elimu na maendeleo ya vijana kwa ujumla.

Siku ya Vijana Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Agosti, na BAVICHA imesema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuimarisha ushiriki wa vijana katika mijadala ya kitaifa na mageuzi ya kidemokrasia nchini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom