ANAANDIKA MH BONIFACE MWABUKUSI RAIS TLS
HII NI HATARI.
Nimepokea taarifa asubuhi hii kwa njia ya Simu kwamba ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia makazi ya muuzaji na msambazaji wa vifaa vya uenezi vya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA) na kwamba baada ya kumkosa mhusika wamemkamata Mke wake na vilevile wamesomba vifaa vya uenezi na kuondoka navyo.
Je hapa Naibu Msajili anasemaje? hii ndiyo siasa safi?
BAK Mwabukusi
Ujumbe huo ni huu hapa?
Muuzaji na Msambazaji (Mzabuni) wa vifaa vya uenezi vya CHADEMA Bw.Mbyela amevamiwa na jeshi la polisi katika makazi yake Mburahati usiku wa kuamkia leo.
Pamoja na jeshi la polisi kumkosa muhusika,wamemkamata mke wa Mbyela na kuondoka na mzigo wote wa vifaa vya uenezi vya CHADEMA.
Polisi wameshuhudiwa na majirani asubuhi hii wakipakia katika lori la polisi vifaa vyote vya uenezi vya CHADEMA vikiwemo bendera zote,Tshirts,kofia,skafu,madera,Kombati,key holders,kanga,viremba,na vikoi vyenye nembo na rangi za CHADEMA.
HUJUMA:
Maana yake jeshi la polisi litakuwa limefanikiwa Kuihujumu CHADEMA hawa wakati huu wa mikutano kwa kuzuia nchi nzima wanachama na viongozi wa CHADEMA wasipate vifaa vya uenezi vya chama chao kwa kushikikia mzigo huo kwa muda usiojilikana.