CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

Hakika hali ni mbaya.......hii ilikuwa jana huko KAHAMA.....watu walikuwa wachache sana!

Slaa+kuagana+na+wananchi.jpg

kujua hi picha niya ukweli angalia mkonon mwa dr pete ya ndoa sote tunajua 2011 alikua bado hajafunga ndoa
 
Shuhudia mwenyewe..........

Slaa+kuhutubia+Kahama+1..jpg

Propaganda za ccm na wapenzi wa usaliti hazitasaidia kudanganya umma wa Tanzania kwa kile chadema inachosimamia.

Nabaki najiuliza, hivi haya magezeti Jamboleo, Majira, Habarileo na Uhuru hakuna sheria za kuyabana kwa kuandika uongo na kudanganya umma?! Kama magezeti yanadanganya na kusema uongo kiasi hicho maana yake ni kwamba magazeti hayo yapo kwa ajili ya kudanganya umma, kama yanadanganya kuhusu ziara ya kiongozi wa chamabcha upinzani kuna uhakika gani kama wanayoandika sio uongo?

Taaluma ya habari imeingiliwa na makanjanja wa Jamboleo, majira, habarileo na kale ka gazeti ka kutegea sumu ya panya UHURU
 
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

Jombaa, achana na propaganda za magazeti magazeti ya CCM, tembelea blog ya MICHUZI leo, uone nyomi iliyojitokeza Kahama......
 
Umefuatilia wapi na sisi tufuatilie tuone

Huna haja ya kufuatilia kokote. Download hii picha kwenye computer yako.
Ukishafanya hivyo, right click kwenye hiyo picha then select properties. Hapo utaona hii picha imepigwa 23.11.2011.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
 

Ushahidi gani zaidi ya yalioyoandikwa magazetini?

Ok.. Tusiamini aliyoandika Makene, bali yaliyoandikwa na magazeti, coz magazeti yanaandikwa na malaika na Makene ni binadamu...
 
Picha hii ni ya mwaka 2011.

Picha hiyo ni ya jana hata nyasi ni maotea ya mvua zilizonyesha wiki iliyopita isitoshe viwanja vya CDT havikuwepo 2011 mwaka huo mkutano ulifanyika Nyihogo community center sasa hapo kwenye picha ni CDT hata ukuta wa CDT garage ya Mchihiyo unaonekana acha uongo ze macopolo gamba mzee wa buku 7.
 
Picha hizi hapa, waweke za kwao basi hizo za kuzomea na mabango. Wakimbie haraka photo shop kufanya hiyo kazi. Wamefanya kwenye stori wanashindwa nini kwenye picha!


 
katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), dk. Willibrod slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.
Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.

Kauli hizo alizitoa jana mjini kahama mkoani shinyanga alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya cdt, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.

Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.

Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.

“watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito,” alisema.

Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa kamati kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa kigoma kaskazini, zitto kabwe.

“mimi nawaambia watulie tu… nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya chadema hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.

“chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na ccm, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.

“wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza,” alisema kiongozi huyo huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi hao.

Dk. Slaa alisema kuwa ccm wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na chadema, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.

safari yapata matatizo

ziara ya dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani kibaha mkoani pwani.

Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.

Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.

Source:tanzania daima alhamisi

sehemu ya umati wa watu uliohudhuria mkutano..........

slaa+kuhutubia+kahama+1..jpg

bora umeweka picha mkuu,, umewakata ngebe
 
Picha hiyo ni ya jana hata nyasi ni maotea ya mvua zilizonyesha wiki iliyopita isitoshe viwanja vya CDT havikuwepo 2011 mwaka huo mkutano ulifanyika Nyihogo community center sasa hapo kwenye picha ni CDT hata ukuta wa CDT garage ya Mchihiyo unaonekana acha uongo ze macopolo gamba mzee wa buku 7.

Wewe ni SIFURI usiyeelewa maana ya photoshop.

Basi amini na zile picha za Lema zilizosambazwa mitandaoni.
 
Mzee wa Moro,

Na wewe umelaghaika? Hujui jinsi ya kutumia yeknolojia kujua picha imepigwa lini?

Umeona kwenye green card wanasema ukitumia picha iliyopigwa zaidi ya miezi 6 unakuwa disqualified, umejiuliza watajuaje picha imepigwa lini?

Una mengi ya kujifunza...

Cc FaizaFoxy

Mbulumundu Leo umeanza shifti mapema namna hii ina maana hujali afya yako kwa kulala usingizi. Heri urudi kwenye kazi uliyosomea ya UNGALIBA huwa kuna mapunziko, hii ya buku Saba hupati hata muda wa kumuhudumia mliberali mwenzio
 
Back
Top Bottom