Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,650
- 6,085
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?
Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?
Kimbunga
Dkt. Slaa alipowasili Kahama majira ya saa 12.15 hivi, kulikuwa na hamasa sana, wengine wanasema mzuka. Alikuwa akisisitiza yeye ni muumini wa sheria kwa sababu siku zote hata mapambano yake dhidi ya vita ya ufisadi yako katika msingi huo. Bila kuwatuliza kwa haraka ili awahutubie ndani ya muda mfupi angelazimika kuwa jukwaani muda mrefu.
Haiwezekani kuwaacha watu waliokusubiri masaa 4, kwa hamu ya kukusikiliza, usitoe hata salaam kwao. Labda kama wapo wanasiasa wa vyama vingine wasiothamini wananchi kiasi hicho lakini si viongozi wa CHADEMA!
Ilikuwa lazima ahutubie kwa sababu watu wamekaa uwanjani tangu saa 8 mchana wakimsubiri yeye. Kuchelewa kwake kulitokana na magari kupata hitilafu iliyotokana na mafuta machafu kama ambavyo tumeshaeleza hapa jana.
Wanaodai kulikuwa na vurugu au mabango au sijui vitu gani, wanastahili kuonewa huruma. Najiuliza binafsi, hivi wananchi wa Kahama waliokuwa pale uwanjani wanawachukuliaje wahariri wa magazeti hayo?
Lakini wasizungumze kwa maneno, hivi kweli kwa uwezo wako wa kufikiri na kujua mambo, kungelikuwa na hali kama hiyo, magazeti hayo yangeandika maneno pekee? Watupatie picha zao! Kama hawana basi hata wafanye doctoring. Kama wameweza kwenye stori, wanasubiri nini kufanya hivyo kwenye picha.
Tunashukuru magazeti kama hayo yataendelea kujifia. Nani anasoma Gazeti la Uhuru? Kama unauliza sheria inayohusu muda wa kuhutubia mikutano, bila shaka anza na Rais Kikwete ambaye aliwahi kuvunja hata sheria ya uchaguzi inayosema specifically mwisho ni saa 12.00.
Kitu cha mwisho kabisa, mnaosema kuna sheria imevunjwa kwa Dkt. Slaa kuhutubia muda huo, mbona mnaweka maneno, wekeni ni sheria gani hiyo.