CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

CHADEMA si Legelege-Dr Slaa

mimi mwenyewe ni mpiga kura wa zzk. . Kusema ukweli dogo watu hawakua na imani naye tena. Hata uchaguzi wa 2010 alipita kwa mbinde
Dogo Zitto amenipunguzia sana kasi ya kupenda siasa na wanasiasa,mm pamoja na UCCM wangu nilikuwa natamani siku awe mwana ccm lakini asiyekuwa mamluki kama alivyo sasa. Namchukulia Zitto kama machagudoa walioko soko la vitunguu Mwanza.
 
Sasa subirini leo Kigoma sukari itakaposhuka

.
Mtakufa kihoro. Labda mna mpango wa kutumia mabomu kama ya kanisani Olisati na mkutanoni chadema Ar? Hata hivyo vita ya wenyewe kwa wenyewe huko Rwanda walio mahakamani kwa zile vurugu ni watu waliofuatiliwa kwenye media na walikuwa wameandika vitisho ama hivi vya kwako. Jaribu kuchunga kauli zako.
.
 
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

Mwanzoni nilidhani na wewe ni kamanda wa ukweli. Kumbe ndo walewale!!!.
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.
Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.

Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.

Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.

Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.

“Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito,” alisema.

Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

“Mimi nawaambia watulie tu… Nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya CHADEMA hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.

“Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na CCM, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.

“Wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia Watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya Watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza,” alisema kiongozi huyo huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi hao.

Dk. Slaa alisema kuwa CCM wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na CHADEMA, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.

Safari yapata matatizo

Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha Dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.

Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.

Source:Tanzania Daima Alhamisi

Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria mkutano..........

Slaa+kuhutubia+Kahama+1..jpg


Dr Slaa akiaga umati huo huku wananchi wakiwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza..........
Slaa+kuagana+na+wananchi.jpg

Pamoja sana Dr Slaa. Chanja mbuga baba.
 
Poleni sana ule umati wa wanakahama ni pigo takatifu kwenu masalia na vimelea vyake vyote

Kama wewe ndy mkweli weka picha za mabago. halaf utupe na ukweli mkutano wa ccm mbeye ilikuwaje?
 
Ile picha watu werevu waliishtukia kwa sababu Dr. Slaa kafika uwanjani saa 12 na robo lakini kwenye ile picha jua kali linawaka. Kahama saa 12 na robo hakuna jua kali!

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...

CCM si chama laghai miaka 50 stil shule hazina dawati barabara hazipiti na kodi nalipa, tembo wanateketea viongozi wanachekeana. hongelen ccm matatizo tuliyonayo kwa sasa ni zzk na cdm.
 
“Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi" - Slaa

Jamani hayo ni maneno ya Slaa, anamaanisha nini?
 
Kuna picha za Nov 2011 ziliwekwa kwenye thread na Kurugenzi ya Habari CHADEMA zikidai ni mkutano ulifanyika Wilayani Kahama jana wakati ni ulaghai wa kiwango cha juu kabisa.

Imebidi MOD's waifunge hiyo thread.

Wananchi wameisha anza kuuelewa ulaghai wa CHADEMA na kwa sasa CHADEMA wako desparate mpaka wanachakachua picha.

Ukweli utaendelea kujipambanua kila siku

Lete picha yako ya jana basi, kinyume chake piga kimya
 
Mapambano yanaendelea....


“Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi,"- Slaa

Sisi tnaelewa mkisema mapambano mnamaanisha nini, si mnataka "kufika nchi ya ahadi"? - Halima Mdee - Bungeni
 
Tatizo watu mnaanza kutukanana jamani why?

Naomba huyu anaejiita molemo atutajie kituo cha mafuta kilichowekwa mafuta machafu...maana ni kosa kabisa kisheria, sasa ataje hicho kituo sasa ili watu waamini kuwa mzee slaa alichelewa kufika kahama...nachojua slaa alifika kahama saa 9 alasiri lakini alishindwa kwenda uwanjani kwa idadi ndogo ya watu na aliambiwa kuna abango yamebebwa na ataweza kuzomewa lakini aliamua kukaa mpaka saa 11;30 aliponda uwanjani kusalimia tu wala hakuhutubia

Mnashindwa kunishawishi hakuna hata picha inayoonyesha hayo mabango, nitaaminije?
 
Mapambano yapi? Kati ya nani na nani?

Kati ya Mafisadi na wapigania haki za raia
Kati ya wala Rushwa na Wakemea Rushwa
Kati ya CCM na CDM
Kati ya Waua Tembo na Walinda tembo
Kati ya Wewe na mimi
 
Je Havikuwepo vyombo vya habari TV ili watuoneshe live kwenye taarifa zao za habari. Penye ukweli uongo ujitenga
 
Pamoja na udaku wake ni moja ya gazeti linalopendwa hapa nchini na mauzo yake ni ya juu sana ukilinganisha na uhuru, habari leo, etc

Magazine ya UDAKU huitwa magazeti pendwa kwa sababu watu wengi hupendelea kusoma UDAKU.
 
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?

Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?

Kimbunga akili yako ina kimbunga kama jina lako ? Vurugu ndiyo hizo ?
 
Back
Top Bottom