Dr. Willibrod Slaa
Public Figure
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
MMJ,
Nakushukuru kwa post yako. i) Kuhusu kwenda kwa Wananchi, ni vema mkaelewa kuwa mara tu baada ya uchaguzi kulikuwa na "Katazo la mikutano ya hadhara". Katazo ambalo awali hatukuielewa imetolewa na nani na imetolewa kwa mamlaka gani, kwa kuwa katazo la aina hiyo kimsingi ilihitaji "Hali ya Hatari kutangazwa" na tangazo la namna hiyo lilitakiwa litolewe na Rais, lakini haikuwa imetolewa. Ilichukua muda na ni baada ya kukusanya na kupata nyaraka kutoka kwa ma OCD wa maeneo mbalimbali ya nchi nzima. Asiyefahamu hilo atadhani tulikuwa tumekaa kimya na si kila kitu tunaweza kuliweka hadharani mpaka pale tunapokuwa tumepata ushahidi. Wengi wanajua kuwa tulipopata ushahidi kamili tulipiga kelele kwa Tamko la Press Conference iliyotolewa na Wanasheria wetu Mhe. Tundu Lissu na Mhe.Mabere Marando. Baada ya Tamko hilo hali imeanza kubadilika na mikutano ya Wabunge wetu imeanza kuruhusiwa japo ya kisiasa bado inaendelea kuzuiliwa. Ndiyo maana ninasisitiza kuwa ni muhimu kama Taarifa haitoshi, tukaulizana kuliko kulaumiana bila kujua misingi ya kinachofanyika. Nadhani Chadema tuko very open, nimekuja kwenye Jamvi hili kwa jina langu na mara kwa mara nimekuwa nikifafanua mambo mbalimbali yanayoihusu Chadema bila kusubiri na bila kigugumizi. Ninaahidi kuwa kama kuna jambo linahitaji niingilie kwa nafasi yangu nipo tayari bila kusubiri kujenga "hisia" ambayo inaweza kupotosha jambo jema, na kazi ya kurekebisha mara nyingi ni ngumu zaidi, na wakati unarekebisha "damage"kubwa inakuwa imeisha kufanyika. ii) Kuhusu Msimamo wa " Lawful na Illegitimate" Press Conference niliyofanya jana haikuwa Kauli ya Dr. Slaa, wala ya Mgombea Urais wa Chadema. Ilikuwa kauli ya Kamati Kuu ya Chadema. Sasa kama tunaamini katika misingi ya Demokrasia ya "collective Responsibility" basi kama kuna mtu au kiongozi alikuwa hakubaliani na wazo hilo, ni siwezi akalazimishwa. Lakini katika Demokrasia uamuzi wa wengi ukifanyika, basi ndio uamuzi, na ambao hawakuwa wanapenda uamuzi huo hawana budi kukubali uamuzi huo. Kwa bahati mbaya hii ndio demokrasia na sina namna nyingine ya kuielezea. iii) Kutoka kweda kwa Wananchi nayo ina stategy yake na ni swala linalohitaji "political timming". Nadhani Chadema as party with strategies, inatekeleza mikakati yake ya lini itoke kwa wananchi kwa timming ambayo italeta maximum benefit na kuepuka damage ya aina aina yeyote ile. Mengine siwezi kuyamwaga hadharani, lakini naamini kama kuna nia njema ninachokieleza kinaeleweka. Wananchi wengi wanaotupigia simu binafsi huwa tunawaelimisha na tunakubaliana nao kwa mengi. Nadhani nimeeleweka MMJ na wana Jamvi wenzangu.