CHADEMA ni wachawi wa upinzani - Mtatiro

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV
 
Hana jipya huyo, kwa hiyo kupewa hela na SABODO ni kuungana na CCM? Huyu bwana mdogo akubali tu kwamba alishaingia choo cha kike, wenzake wanajadiliana maswala ya CUF mskitini ambapo yeye hawezi kufika, halafu anakuja kukurupuka na kuongea upuuzi tu.

CUF wameungana na CCM Zanzibar kuunda what is called serikali ya kitaifa, je wana-qualify vipi kuwa wapinzani? Dogo akiweza hata achomoke tu na aende CHADEMA anaweza pokelewa tu, muulize alijaribu ubunge Ubungo alipata kura ngapi??
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV

Mtatiro naona una matatizo makubwa. Kama CUF hamjaungana na CCM tuambie katibu mkuu wa Chama chako yuko wapi sasa hivi? Katibu Mkuu wa CUF ni makamu wa rais wa Zanzibar na kwa namna yoyote ile hawezi kuipinga serikali anayoiongoza. CUF na CCM wanaongoza serikali ya Zanzibar kwa pamoja bila ubishi wowote, unataka kusema huo sio ushirikiano? mwenye propaganda kati wewe na Chadema ni nani?

Labda Mtatiro huifahamu CUF ila upo upo tu? Katazame vizuri kwenye kamusi nini maana ya kushirikiana halafu tuambie kama kitendo cha chama cha CUF kushirikishwa katika uundaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa Oktoba 2010 siyo ushirikiano.
 
Mtatiro amechemka vibaya sana

Jamani kama anaingia humu, mwambieni he has gone too low for a young and intelligent guy kama yeye
 
Kupokea msaada (tena kwa uwazi) huwezi kulinganisha na kuwa ndani ya serikali wakati huohuo unakuwa mpinzani..!
Mtatiro, Bosi wako akiwa ZnZ ni makamu wa Kwanza wa Rais katika serikali ya pamoja na ccm,kilometa kadhaa bara ni katibu mkuu wa chama cha upinzani kikiipinga serikali ileile inayoongozwa na ccm..,hamueleweki ni vuguvugu au moto...
 
mtatiro rafiki yangu nilikuambia chama makini Tanzania ni kipi lakini ulinipuuza sasa unapoenda ni kujishusha kisiasa,si umeona prof safari ashatoka huko sasa yuko kwenye michakato mingine! karibu chamani kwetu tujenge nchi yetu
 
Mtatiro naona una matatizo makubwa. Kama CUF hamjaungana na CCM tuambie katibu mkuu wa Chama chako yuko wapi sasa hivi? Katibu Mkuu wa CUF ni makamu wa rais wa Zanzibar na kwa namna yoyote ile hawezi kuipinga serikali anayoiongoza. CUF na CCM wanaongoza serikali ya Zanzibar kwa pamoja bila ubishi wowote, unataka kusema huo sio ushirikiano? mwenye propaganda kati wewe na Chadema ni nani?

Labda Mtatiro huifahamu CUF ila upo upo tu? Katazame vizuri kwenye kamusi nini maana ya kushirikiana halafu tuambie kama kitendo cha chama cha CUF kushirikishwa katika uundaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa Oktoba 2010 siyo ushirikiano.
Penye rangi nyekundu. Mtatiro haifahamu CUF, AWAULIZE JAMES MAPALALA NA WILIAN LWAKATARE. Namtabiria Bw. Mtatiro siku ya kutoka CUF atatokea mlango wa nyuma
 
Hivi hawana mambo ya kuongea na kufanya hadi wapambane na chadema? Wehu kweli hawa!
 
waache waamini wanavyoamini? na kama kipofu nimbishi bas mwache ajiongoze aingie shimoni kwa mwerevu atampuuza tu huyu zumbukuku
 
Wamepewa kazi na ccm kupambana na chadema,lakini wanadhani watanzania wa leo ndio walewale wa miaka ya nyuma
 
Nadhani tuna haja ya kuamini kuwa Chadema ndiyo chama Tawala kwa sababu ndiyo chama ambacho kinapingwa. Wapinzani wa Chadema ni CCM, CUF, NCCR - Mageuzi, TLP, UPD... Mti wenye matunda ndio unaorushiwa mawe.

Kama Chadema siyo chama Tawala iweje CCM waungane na vyama vingine kukipinga? Mara nyingi tumeona vyama vingine vinavyodhaniwa kuwa vya upinzani vikikashifu Chadema badala ya chama kilichopo madarakani. Kwa hili tukubaliane tu kwamba CCM na vyama hivyo vingine vitangaze kuwa Chadema ni chama Tawala ili yaishe.
 
Mimi naona kabla hajaharibu zaidi angerudi kundini, kwasababu neno "ningejua" huja mwisho wa safari.......Akamuulize profesa SAFARI na ajifunze kuwa CUF huku Tanganyika sio chama bali ni mfano wa chama cha upinzani lakini wenye lengo la kuua upinzani.
 
Kupokea msaada (tena kwa uwazi) huwezi kulinganisha na kuwa ndani ya serikali wakati huohuo unakuwa mpinzani..!
Mtatiro, Bosi wako akiwa ZnZ ni makamu wa Kwanza wa Rais katika serikali ya pamoja na ccm,kilometa kadhaa bara ni katibu mkuu wa chama cha upinzani kikiipinga serikali ileile inayoongozwa na ccm..,hamueleweki ni vuguvugu au moto...
Mtatiro atafundishwa polepole ataelewa tu!!!!!! Nikijana hodari wa kisiasa, mwenye hoja malidhawa, lakini yuko ndipo siyo. Mwambie achomokee CDM hapo atakuwa mpinzani wa ukweli sio umang'amung'amu!!!!!!
 
Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Jurius Mtatiro amesema Chadema ni wachawi wa upinzani Tanzania, tena ni vigeugeu wakubwa watu wa propoganda kila siku wanaumiza vichwa vyao jinsi gani watawauwa CUF; wanaeneza propoganda CUF wamaeungana na CCM hawawezi kushirikiana nao wakati huo huo Chadema wanachukuwa pesa kutoka kwa kada wa CCM SABODO, ni sawa sawa kusema utaki kula nyama ya nguruwe lakini supu yake unakunywa.

MLIMANI TV
Mtatiro ni mtu mwenye maneno mengi tena yasiyojenga zaidi sana ni kujihami na kujaribu kuharibu hali ya hewa ndani ya CDM na wananchi dhidi ya CDM, binafsi huyu jamaa ni kati ya watu ambao nimewapuuza muda mrefu, mtatiro anafaa sana kwa maneno yake mengi ya hovyo hovyo kuwa MC kwenye kicheni parties/unyagoni.
 
Back
Top Bottom