Kama kuna jambo ambalo ni dhahiri kwa sasa kwa Tanzania, ni hamu ya watanzania kupata mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi. Lakini pengo kubwa linaloonekana ni kukosekana kwa nguvu na sauti moja ambayo itaungwa mkono na watanzania kutoka makundi yote ya kijamii bila kujali makabila yao, dini zao, rangi zao, jinsia n.k.
Wakati ikionekana ni wazi kuwa CCM ni chama ambacho watanzania wangependa kikae chonjo ili kupisha mabadiliko na kujikarabati upya, hakuna chama cha upinzani ambacho kinawaunganisha watanzania kufikia malengo hayo kwa mujibu wa tofauti zao. Hii ni kutokana na kasoro mbali mbali zikiwemo za kuzuwa na nyingine ni za kweli ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kuaminiwa na baadhi ya wananchi walio wengi.
Vyama vingi viliibuka na kufifia mfano TLP na NCCR kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubinafsi wa viongozi waliovianzisha, migogoro ya kimaslahi na mapandikizi kutoka chama tawala. Mfano wa udhaifu katika vyama vya upinzania hapa Tanzania ni kama ifuatavyo:
1) CHADEMA
Kwa sasa ndicho chama ambacho kinaonekana kuwa na nguvu kubwa kama chama kikuu cha upinzani.
Hata hivyo kinakabiliwa na shutuma zifuatazo:
i)Ukabila na ukanda
ii)Ukosefu wa maadili kwa watendaji wake wakuu
iii)Kutokuaminiana kati ya viongozi wake wakuu ikidhaniwa kwamba baadhi ni mapandikizi kutoka chama tawala.
iv)Dhana ya CHADEMA kwamba vyama vyote vya upinzani ni mapandikizi ya CCM, hivyo kukataa ushirikiano na vyama vingine.
v)Udini
2)CUF
Ni chama ambacho ni cha pili cha upinzani baada ya CHADEMA. Hata hivyo kinashutumiwa kwa mambo yafuatayo:
i) Udini
ii) Usultani wa viongozi wakuu kuhodhi madaraka na kutokuwapisha wengine kukamata nafasi kubwa za uongozi
iii) Kuwa na nguvu upande mmoja wa muungano
3) NCCR: Huko mwanzo kilishawahi kuhusishwa na ukanda na ukabila. Hata hivyo kwa sasa madai haya hayasikiki kwa vile nguvu zake zimepungua kama ilivyo TLP.
4) Vyama vingine vilivyobaki vinachukuliwa kama NGOs za kujipatia mapato kwa waliovianzisha.
Hizi shutma iwe zina uhakika au ni za kukisia, tukubali kuwa ni pengo kwa ukombozi wa kweli wa Tanzania na ni ngumu kuziondoa kwa sasa kwa vile jamii imeshagawanywa kwa misingi hiyo.
HITIMISHO:
Ili kukata kiu ya mabadiliko ya watanzania, ni vyema wasomi mbalimbali maarufu wanaokubalika wasiohusika na kashfa hizo hapo juu kuungana na kuanzisha chama ambacho kitakubalika na watanzania walio wengi. Vugu vugu hili la mabadiliko ya kweli litafaa zaidi kama litaanzia kwenye taasisi za elimu ya juu.
Tukifika hapo TZ in 2015 ni vifijo na nderemo! Kinyume chake, tusahau kuingóa CCM madarakani kutokana na advantage ya mgawanyiko kutokana na tofauti tajwa hapo juu. Weka ushabiki wa chama pembeni unapochangia hii thread! Mihemko ikikuzidi, fanya kama vile hujaiona hii thread!