Bayana hana mada yenye mashiko. Ni wale wale wanaotumwa kukatisha watu tamaa ya abadiliko baada ya kuona Chadema wanachanja mbunga. Hana kitu cha kuwaeleza wa tz. Ukabila na ukanda uko wapi? Huko tumeshatoka tunasonga mbele haturudi nyuma kwa sababu za kizee. Kiwewe cha nini? Kama ni yeye na wajomba zake wakae chonjo kujibu mashtaka ya wizi na matumizi mabaya ya raslimali za taifa. Hakuna pa kujificha, hatuna haja ya chama mnachotaka nyie. Jibuni hoja na mkae mkao wa kushughulikiwa kila mtu kufuatana na makosa yake kwa jamii. hatudanganyiki sisi. pole sana kwa yanayowafika sasa hadi mnapanda majukwaani kulalamika badala ya kutatua kero