Chadema ndani ya Bukoba


PJ rafiki yangu, I see your point but if hilo ndilo lengo la Chadema basi tutafute option nyingine. Tupo katika hali ambayo hatukusudii kujenga umaarufu wa Chadema kuelekea 2015 bali tumechoka, tunataka nguvu ya umma kuiondoa serikali madarakani. Box la kura halitaweza kuleta Uchaguzi wa haki tz.

Tunaweza kuwatetea Chadema kwa sababu tunawapenda mno hivyo tunawaonea huruma na hatujisikii raha wakikosolewa.

Tunaweza kuridhika na Chadema kufanikisha maandamano makubwa na mabango yenye ujumbe mkali. Ni kwa sababu tu tuko fascinated na Chadema na siyo kwa sababu hayo maandamano yametatua matatizo yanayotuzidi kila uchao.

Kwa hiyo maandamano ya Chadema yanageuka moja ya burudani kwa wananchi, which is not bad, but is that all?
 
Hizi habari kama vile sizielewi au sijazitegemea...!?
Inamaana hamtafika Arusha mpaka baada ya bunge la April???????
Crashwise , Arusha kuna taarifa za kiingtelijensia, bado hazijaisha hata siku ya kesi hivi karibuni tulisikia mabomu, huyo RPC Arusha nadhani anajisikia vibaya anapoona wenzake hawatumii nguvu.
 
Hongereni viana na wananchi wa Bukoba kwa kazi mlioifanya kuwapokea hao wageni fanyeni hivyo hata kwenye mikutano kesho mpewe elimu ya uraia.
 

Hujanielewa mkuu, siyo kila post ni ushabiki. Mimi sina chama lakini nina imani na Chadema kwa sasa. Ni jukumu langu kuwaeleza fikra zangu hata kama wengi mtazichukia

kwa hiyo, kwa mantiki yako, Chadema wakitumia vibaya rasilimali zetu tusiwaulize kwa sababu ccm wanatumia nyingi zaidi vibaya?
 
Hawawezi kufanya hivyo maana walijaribu ziara za aina hii kuelezea wananchi mafanikio ya serikali wakaishia kuzomewa
 
Tunashukuru tume enjoy sana . peeeeeeplessss powerrrrrrrrrrrr
 

AMEN KIWI !!
:amen::wave:
 
na Sitta Tuma na Janet Josiah, Bukoba



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuitikisa nchi kwa maandamano na mikutano yake ya hadhara kuzidi kuungwa mkono na umati mkubwa wa watu katika kila mkoa kinakopita.
Baada ya kuiteka mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga, jana chama hicho kiliuteka kwa kishindo mji mzima wa Bukoba kwa mapokezi, maandamano na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wingi wa watu ambao kwa mujibu wa wenyeji wa hapa, haujapata kutokea huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Willbrod Slaa, akitoa tamko la msisitizo akisema “moto wa maandamano ya kudai mabadiliko sasa hautakoma, utaendelea nchi nzima.”
Dk. Slaa aliwataka wakazi wa mji huo kumbana waziri mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kashfa mbalimbali za ufisadi na uzembe zinazoikabili serikali yake. Pinda anatarajiwa kuanza ziara yake mjini hapa leo.
Alisema CHADEMA itaendelea kufanya siasa kwa kuwafuata wananchi walipo na haitabakia kutegemea Bunge kama anavyotaka rais Kikwete wafanye kwani tayari chombo hicho cha wananchi kanuni zake zimechakachuliwa ili kudhibiti wabunge wa chama hicho.
Awali maelfu kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walitanda na kufunga barabara na mitaa ya mji huo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana walipoanza maandamano makubwa ya kuelekea viwanja vya mashujaa mjini hapa kulikofanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Maandamano hayo yalifanyika katika staili ya makundi huku kila kundi likichomoza katika mitaa tofauti na lingine na kujaza watu katika uwanja huo.
Baadhi ya waandamanaji hao walionekana wakiwa na mabango mbalimbali yaliyosheheni ujumbe wa kuilaani na kuipinga vikali serikali ya rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati mji wa Bukoba ukiwa ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa sana na janga la ugonjwa wa Ukimwi nchini, wananchi hao walionyeshwa kukerwa kwao na serikali ya CCM na katika moja ya mabango yao walisema hivi: “Keri ya ukimwi kuliko CCM”.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alipokewa kwa nyimbo zilizokuwa zikimtaja kuwa yeye ndiye rais halali wa nchi hii.
“Rais, rais, rais, rais….”, ulisikika umati wa watu ukiimba katika maandamano hayo.
Dk.Slaa aliingia kwa kishindo Bukoba baada ya kuachiwa huru na polisi mjini Kahama walikokuwa wanamshikilia akidaiwa kuwa alifanya mkutano bila kupata kibali wilayani Maswa.
Akizungumzia kukamatwa kwake katika mkutano huo wa hadhara jana, Dk. Slaa alisema “walionikamata walitumwa wanikamate kwa sababu Kikwete ananiogopa, lakini sasa hawatuwezi, CHADEMA haikamatiki”
Kabla ya tukio la kukamatwa kwa Dk Slaa juzi usiku askari polisi waliizingira hoteli ya Panich aliyokuwa amefikia kiongozi huyo.
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi Mnadhimu huyo wa polisi alimhoji Dk Slaa: kwanini jana usiku ulikataa kuja polisi kama ulivyotakiwa? Dk Slaa alijibu “Nilihofia usalama wangu kwa sababu watu waionifuata hotelini sikuwatambua kwa sababu walikuwa wamevaa nguo za kiraia”.
Mnadhimu Kamugisha alimuuliza tena kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani kwamba kwanini juzi alifanya mkutano Imalampaka bila kibali cha polisi? Dk Slaa alijibu, “nadhani mnafahamu kwamba chadema tunafanya maandamano na mikutano mikubwa ya hadhara na kila eneo tunalokwenda majimboni kuna ratiba, halafu ninyi mnauliza mambo kama haya hapa lakini juzi kiongozi wetu alipigwa jiwe na polisi hamjawakamata wahusika”
Mbali na Dk Slaa kukamatwa na kuhojiwa na polisi wa wilaya hiyo ya Kahama kwa zaidi ya saa 1:30 wabunge wengine wawili wa CHADEMA, Chiku Abwao na Rachel Mashishanga pia walishikiliwa kwa mahojiano na jeshi hilo. Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani (RPC) alipoulizwa sababu za jeshi lake kumkamata Dk Slaa wilayani Kahama badala ya kumkamatia wilayani Maswa alikofanyia mkutano huo, alisema waliogopa kumtia nguvuni wilayani Maswa kwa kuhofia uvunjifu wa amani.
Kafulila aifagilia CHADEMA

MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) amemshangaa Rais Jakaya Kikwete kuogopa kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuzungumza na wananchi.
Licha ya kumshangaa rais Kikwete kwa hofu aliyonayo amekipongeza CHADEMA na kusema chama chake kinajipanga kwenda kwa wananchi kwa kuwa ni utekelezaji wa kazi za siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya NCCR-Mageuzi Dar es Salaam jana, Kafulila aliyewahi kuwa kada wa CHADEMA, alisema hofu ya kupinduliwa aliyonayo rais inatokana na watawala kushindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wananchi wengi kukata tamaa.
Mbunge huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba licha ya kutofautiana kwenye baadhi ya mambo na chama alichokuwepo mwanzo alisema kazi nzuri inayofanywa na CHADEMA mikoani inastahili kuigwa na vyama vingine.
Alisema sababu ya kutoweka kwa hali ya amani nchini sio wanasiasa bali ni watawala kushindwa kutimiza wajibu wao hivyo ni rahisi kwa waliokata tamaa kufanya lolote watakaloona inafaa. “Rais Kiwkete ni rais wetu namheshimu lakini katika hili natofautiana nae…CHADEMA wapo mikoani wanazungumza na wananchi, hiyo ni kazi ya chama chochote cha siasa binafsi nawapongeza, mimi na chama changu tunawaunga mkono. Wapo sahihi kabisa. “…Hata sisi tutakwenda kwa wananchi tutafanya mikutano, unajua kuvunjika kwa amani ni matokeo ya watawala kushindwa kutimiza wajibu wao sasa wananchi wanakata tamaa wanaamua kufanya yao,” alisema Kafulila.
 
Thanks

Mnyika kaongea vizuri hope wananchi wafunguka macho
 
wape wape wale CCM B wayaone haya kwamba mapambano ni mstari wa mbele siku zote..
 
kutumia rasimila, then angalia kuna impact gani?
is it positive or negative?
CDM wanatumia maandamano kutoa elimu ya uraia..so kaa fikiria, Je elimu ya uraia ina positive au negative impact.
then utapata jibu kama wanatumia hela vibaya, au wanamwaga unga baharini kama unavyofikiria wewe. na akili yako inavyokutumua.
Jua kwamba, elimu ni ghari (education is expensive), huwezi kuitoa bila kutumia hela.
ila ni bora kutumia hela kutoa elimu ya uraia na wananchi wakazijua haki zao. kuliko chama chako wanavyochoma mabilion ya hela kwa ufisadi,
 



Kiwi, nobody could have said it better!!!!!! I salute you! Nimeyaandika haya maneno yaliyo bold kwenye note book yangu na ninayakariri kwenye ubongo wangu. Asante:first:
 
Sidhani kama hujui faida ya maandamano au hujui maana ya kujenga umaarufu kwenye siasa kama hujui basi siasa zinakupitia kushoto. If people are tired join and help them if you can't join let them fight alone.
 
More pics from Bukoba.
 

Attachments

  • IMGP0603.jpg
    26.7 KB · Views: 358
  • IMGP0606.jpg
    33.7 KB · Views: 356
  • DSCF0337.jpg
    40.7 KB · Views: 356
  • IMGP0604.jpg
    27 KB · Views: 357
  • IMGP0607.jpg
    28.2 KB · Views: 372
  • IMGP0636.jpg
    23.5 KB · Views: 366
  • IMGP0616.jpg
    37.8 KB · Views: 362
  • IMGP0719.jpg
    46.5 KB · Views: 367
  • IMGP0651.jpg
    29.6 KB · Views: 375
  • IMGP0712.jpg
    39.9 KB · Views: 373
  • IMGP0608.jpg
    35.3 KB · Views: 372
  • IMGP0631.jpg
    24.7 KB · Views: 363
  • IMGP0713.jpg
    40.7 KB · Views: 368
  • IMGP0657.jpg
    32.1 KB · Views: 389
  • IMGP0633.jpg
    28.8 KB · Views: 361
  • IMGP0710.jpg
    46.3 KB · Views: 370
  • IMGP0626.jpg
    34.1 KB · Views: 257
  • IMGP0654.jpg
    32.7 KB · Views: 532
  • IMGP0721.jpg
    41.8 KB · Views: 400
  • IMGP0611.jpg
    24.3 KB · Views: 482
  • IMGP0714.jpg
    45.3 KB · Views: 364
  • IMGP0634.jpg
    24.2 KB · Views: 357
  • IMGP0709.jpg
    40.7 KB · Views: 157
  • IMGP0691.jpg
    38.4 KB · Views: 358
  • IMGP0615.jpg
    30.6 KB · Views: 357
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…