Je inawezekana kumtoa mtu aliyewekwa madarakani kwa wingi wa kura za wananchi na kuapishwa kisheria. Chadema lazima mtumie japo akili kidogo kujua kuwa hamtaweza kumng'oa JK mpaka miaka mitano yake imalizike. sasa msituletee balaa kwa maneno yenu ya uchochezi na kufarakanisha watu ili damu imwagike.
Sisi tunazidi kuomba amani itawale na wenye nia tofauti na hiyo Mola awaadhibu sana.
Wale wote wanaojidanganya kuwa Tanzania ni nchi ya amani poleni sana.
Angalia jinsi nyumba zinavyojengwa na kuta na mageti kama jela, pamoja na joto lote hili watu hawathubutu kuacha hata mageti wazi ili wapate upepo mzuri unaotoka nje.
Kupokea simu sehemu zingine ni balaa, kuna watu hata vibrations wanaziondoa maana vibaka wanazistukia mpaka vibrations.
Kina mama kunyang'anywa mikoba yao na hata kina baba ukiweka pesa kwenye pochi kaa chonjo.
Usiku unalala huku sikio liko nje, kusikikilia kelele za mwizi.
Gari ukiliegesha usishangae kurudi hakuna side mirrors, alama za gari kama TOYOTA, MITSUBISHI n.k. Hata gari lenyewe ukizubaa linaenda. Magari mengi yamewekewa alarm ukipita karibu tu unasikia king'ora.
Na wale majambazi waliouawa jana Morogoro wakiiba duka la sonara, kweli inaashiria amani.
Orodha ni ndefu sana wengine wanaweza kuongeza.
Naomba ninukuu usemi kwa lugha ya kiingereza,
Peace does not mean the absence of war!
Amani ni kuwa na utulivu mpaka wa kisaikolojia, kuwa na uhuru wa kutembea, kulala bila hofu, kuwaacha watoto wako waende matembezini ama ufukweni kuogelea wewe mwenyewe ukiwa umepumzika nyumbani kwako bila hofu yoyote. Kuwa na uhuru wa kuacha mlango wazi wakati wa joto na kuanika nguo zako kwenye kamba nje mwenyewe ukaingia ndani. Amani ikuwezeshe kuacha gari lako mahali ukaenda kwenye shughuli zingine ukarudi baada ya masaa matatu ukalikuta liko salama. Amani ni kumpa mtoto wako simu ya Nokia akienda shule ukamwambia ukiona nimechelewa kuja kukufuata, mpigie simu mama yako mdogo halafu umsubiri kituoni aje kukuchukua. Nawe uwe na amani kabisa kuwa itakuwa hivyo. Kama hayo hayawezekani, basi Tanzania hakuna amani. Huhitaji Chadema kuvunja amani maana haipo.