Chadema ndani ya Bukoba

Mama sisi tunaomba tu AMANI itawale na kusiwe na maneno ya uchochezi na ya kuleta chuki na mifarakano miongoni mwa jamii kiasi cha kuleta vita katika jamii.

CHADEMA KUMBUKENI MDOMO ULIKIPONZA KICHWA

Ufisadi, wizi, uroho na kukosa uzalendo ndio kutasababisha vita katika jamii na sio maneno ya kukemea udhalimu.
 
Hata mimi sielewi these days taarifa za maandamano hazirushwi kwenye tv utaishia kusoma kwenye headlines zinazopita chini habari yenyewe hairushwi,kwa kweli we still have got a long way to go,kama media iko monopolized na gvt hii ni hatari sana> regulatory capture!!!
 
Tunakushukuru Dada yetu Regia Mtema.
Tunakuombea kwa mwenyenzi Mungu awalinde wakati wote wa harakati za kumkomboa mtanzania bila kujali kabila,Dini wala itikadi yake kisiasa
 
Mdogo wangu ndio amewasili kutoka kijijini kwetu kwa ajili ya kumpokea Dr. Slaa na kujiunga kwenye maandamano.

Naomba mlio Bukoba Mjini mtujuze yatakayoendelea....
 
tujuzeni yanayojiri huko kagera (bukoba), mhe. waziri kivuli kazi na ajira
 
lakini mbona hamna anayekanusha ama kukubali kwamba Dr kakamatwa huko kahama, is this tetesi true or not?
 
maandamano yamefikia wap?au jf member kagera hawapo au wamefulia hata vocha wanashindwa kuweka!
 
Ninazo taarifa kuwa yako maandamano yanaendelea kule Bukoba kutokea nje ya mji kwenda mjini Bukoba ya wana chadema. Bado nasubiri updates na picha niwaletee. CCM wanahaha kuona bao walilopigwa haliingii.
Tukutane baadaye.
 
Wakuu.Habari!!!

Yale Maandamano ya CHADEMA katika Kanda ya Ziwa yanatarajiwa kuhitimishwa leo kwa maandamano makubwa na ya aina yake Bukoba Mjini. Maandamano hayo yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.Maandalizi yameshakamilika na msafara wa Vikosi Kazi ndio unajiandaa kutoka Kahama vilipotia nanga kuelekea Bukoba. Kazi kamili itahitimishwa kesho kwa kufanya mikutano ya hadhara kwenye Wilaya za Mkoa wa Kagera. Baada ya hapo Vikosi vitarudi Dar es salam kwa maandalizi ya Kanda nyingine baada ya Bunge la Aprili. Habari ya matukio baadaye kazi ikianza.

Kutoka Kahama
Reagia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.

...thanks mama,,,,,,people's power!!!!!
 
Nimeongea na rafiki yangu toka BKB, amesema ule uwanja wa uhuru umeshajaa wakati maandamano yenyewe hayajaingia uwajani. Ni mlala hoi; hawezi kutuma picha.
 
Ninazo taarifa kuwa yako maandamano yanaendelea kule Bukoba kutokea nje ya mji kwenda mjini Bukoba ya wana chadema. Bado nasubiri updates na picha niwaletee. CCM wanahaha kuona bao walilopigwa haliingii.
Tukutane baadaye.

watahaa sana ...mpira wataukuta nyavuni
 
Nimepita Rwamishenye mida ya saa tano ilikuwa balaaa.

Yaani utadhani wanazindua kampeni za Ubunge Kati ya Rwakatare na Kataraiya. Jana Rwakatare alifanya mahojiano na Redion Vision yahapa Bukoba. Mtaani hii ndo ilikuwa gumzo. Mwamko na ari ya Wananchi iko juu sana.

Kwa hapa, baada ya maandamano na mkutano, CHADEMA inaweza kujikuta imefanikisha mambo mengi sana ikiwemo kuvunjavunja nguvu za ccm. Agenda kuu waliyoiweka mbele (UGUMU WA MAISHA na DOWANS) zimewakamata vilivyo wananchi wa hapa. Hata wiki iliyopita Kagasheki alipofanya Mkutano, wananchi walimweleza bayana msimamo wao juu ya mambo hayo. Kagasheki alikuj ghafla kuwahi KIMBUNGA cha ujio wa Dr. Slaa
 
Msafara ndio uko Rwamishenye Round About kwa sasa.Watu ni wengi,magari na pikipiki za kumwaga.
 
Back
Top Bottom