Mkuu, tatizo si kuwa wewe ni mwana Chadema, Mwana CUF au mwana CCM au wa chama kingine chochote kile. Kiinachotakiwa ni kupingana kwa hoja, na si kutumia matusi na kejeli. Mimi naamini kuwa hakuna chama au serikali isiyopingwa duniani.
Sasa sisi wengine tusiokuwa na vyama, mnatuogopesha na siasa zenu za visasi. Mi natarajia watu washushe nondo za uhakika na waeleze mazuri ya vyama vyao, na ikiwezekana waielekeze serikali nini cha kufanya, pale linapotokea tatizo na si kuleta matusi....! Tanzania ni yetu sote, sasa msituhatarishie amani yetu.
Mtakapoanza kuwatukana kuwa wanachama wa chama fulani i.e CHADEMA/CUF/CCM kuwa ni wajinga au kuwaita wapumbavu, unaye mtukana hapa kama si nduguyo ni nani!?
Mimi binafsi nina ndugu kwenye vyama vyote hivyo, na tunaheshimiana, na wakati mwingine wananishawishi kujiunga na vyama vyao, lakini kwa bahati ghafi mimi si mpenzi wa vyama vyote hivyo, nipo neutral na ninaheshimu mapenzi ya kila mmoja.
Mimi siasa sio zangu ila naingia hapa jukwaa la siasa kuchungulia kwa vile nipende nisipende siasa inaathiri sehemu kubwa ya maisha yangu nikiwa kama raia.Umenena XP,naimiss sana ile JF ya enzi zile kabla ya June 2010.......Natamani Mods wairudishe ile JF ambayo ilifikia kipindi ikaitwa 'The Home of Great Thinkers......
Dah.....................
Mama,Kyoma,Dilunga,Kuhani,YournameisMine,bht,Charity,Game Theory,Icadon,Pundit,Bluray?,Ibrah,Kana Ka Nsungu,Nemesis,Next Level(anategea tegea siku hizi huyu),Sipo,Penny,Mbogela,Baba Mkubwa,Original Pastor,Ladislaus Modest,Asha Abdallah,Mwafrika wa Kike,Mwazange,Hauxtable,Kevo na wakuu wengine kibao ama wamepotea kabisa ama wanaingia JF kwa kusuasua kutokana hali ya hewa kuchafuka mara kwa mara kikubwa kikiwa ni u-CCM na u-CHADEMA....
Nikweli mkuu mi nimesoma mstari mmija tu hoi, inabidi nisome maoni yanasemaje ili nielewe mkuu anamaanisha nini.Well said boss,naamini sio wote wataisoma waimalize hii post
majina na sura za ajabu zilizoko humu zinaonyesha kuwa huu mtandao haupo makini,na most of them ni waoga thats why wanajificha.eg.picha ya hitler inafanya nini hapa?au kwa nini uweke picha ya jini wakati we ni binadamu.kama unaamini unachokisema hupaswi kujificha na unatakiwa uwe tayari kwa lolote litakalokufika.nashauri ufanyike usajili wa information za watu wote wanaotaka kuchangia humu or else discussion zetu zitachakachuliwa kila siku na hatufiki popote!
And viceversa.....wana CCM kwa kweli wanadharauliwa sana humu jamvini,wanaonekana hawana ufahamu wa siasa na hawajui kinachoendelea au ni mafisadi au watoto wa mafisadi,usalama etc..Mkuu XP ulilosema ni point sana tatizo ni moja 2, ckatai kwamba hakuna ucdm na uccm hapa mjamvini ila wengi wanaoipinga au kuikosoa serikali wanaonekana ni wanacdm wala sijui ni kwanini!
ILIFIKIA HATUA NILIKUWA ADDICTED NA JF......! NILIKUWA SIWEZI KOSA...HOJA MOTOMOTO, ZA UNDANI , ZENYE KUIBUA YALIYOJIFICHA KWA MASLAHI YA TAIFA.....!
LO! Baadaye ...mambo yakaanza kwenda mrama.....SIASA ZA CHUKI,UHAFIDHINA,UBAGUZI,KUCHAFUANA,MATUSI NDO IKAWA MAHALI YANAPOPATIKANA NI JF...PICHA ZA KUDHALILISHA, KEJELI ,KUTAMANI KUMWAGA DAMU,MAWAZO YASIYO ENDELEVU NA KILA OVU!
WE HAVE TO TURN BACK WHERE WE WERE
Well said boss,naamini sio wote wataisoma waimalize hii post