CHADEMA na CCM Mnaiharibu JamiiForums | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na CCM Mnaiharibu JamiiForums

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jun 5, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nachukua nafasi hii nami nitoe yangu machache, kati ya mambo kadhaa yanayo kera ndani ya Jamiiforums. Siku za hivi karibuni limekuwa ni jambo la kawaida sana kukuta washabiki wa hivi vyama viwili wakirushiana vijembe na wakati mwingine hata kutukanana na kuitana majina yasio pendeza.

  Hivi vyama viwili, kwa uoni wangu, vina wanachama wa aina mbali mbali, na haswa dini hizi mbili, Uislam na Ukikristo na pia wasio na imani za hizi dini mbili, vile vile wana wanachama wa kutoka makabila mbali mbali ya Tanzania.

  Dini na Siasa ni sehemu ya maisha, mang'amuzi na maendeleo endelevu ya mwanadamu sanjari na haki zake zote msingi. Kashfa za kisiasa na kidini ni uvunjifu wa haki msingi za binadamu zinazohatarisha pia mafao ya wengi ndani ya jamii. JF tunao wajibu wa kulinda na kudumisha haki msingi za Kisiasa na Kidini, kwani hizi pia ni sehemu ya haki za kila mmoja wetu.

  Mimi ambaye ni Muislam, na si mfuasi wa chama chochote kile cha kisiasa, nikisoma bandiko la mfuasi wa Chadema au CCM, na katika hoja zake akausema vibaya Uislam kwa ubaya bila ya ushahidi, kwa kuwa tu muhusika ni Muislam, atakuwa ajanitendea haki mimi ambaye ni mfuasi wa imani hiyo ya Kiislam. Alikadharika pia kwa wale wanao amini Ukristo. Inanishangaza sana watu wanaposhindwa kumjadili mtu kama yeye bila ya kumuhusisha na imani yake. Hii yote ni kutokana na kutojua misingi ya majadiriano, na kukimbilia kujibu hoja hata pale unapokuwa huna la maana katika kuchangia hizo hoja.

  Watanzania tuliipokea Demokrasia ya vyama vingi kwa moyo mkunjufu miaka mingi iliyopita, baada ya kuamua kuachana na ukiritimba wa chama kimoja tukilenga kupata fursa zaidi ya kuchagua viongozi tunaowataka. Hiyo ilikuwa hatua muhimu katika kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kikamilifu kutoa ridhaa juu ya nani anaefaa kuongoza nchi.

  Demokrasia ni neno pana sana, linaweza kutafsiriwa kwenye kanuni ya wengi wape au ikimaanisha kuwa watu wawe huru kujieleza au kuelezea hisia zao lakini kwa kutumia maneno yalio na adabu na nidhamu, bila ya kuvuka mipaka ya kisheria.

  JF ni mkusanyiko wa watu wa aina mbalimbali, wanasiasa, na wasio wanasiasa, wenye imani za dini na wasio na imani za dini. Mkusanyiko huu, unahashiria kuwa JF ni tovuti baraza linalo kusanya watu wa aina mbali mbali na wenye mitazamo tofauti tofauti.

  Kipindi JF ilipokuwa inaitwa jamboforums, tulishuhudia wanachama wake wakitoa na wakishindana kwa kuchangia hoja zenye nguvu. Hoja ambazo zilweza kuamsha hari ya msomaji kuchangamsha akili yake na kufanya utafiti kabla ya kuja kujibu hoja husika. Na hii ndio ikapelekea kuwa na kauri mbiu ya Where we dare To Talk Openly. Kauli hii haimaanishi kuwa watu waseme tu kila kitu kinachopita kwenye akili zao, bila ya kuchunywa kwanza. Lakini hivi sasa tunashuhudia kila aina ya matusi na maneno yasio na maana kiasi ya kutia shaka akili ya wachangiaji wengi.

  Ndani ya JF, kuna viongozi wa vyama hivyo viwili, nikimaanisha CHADEMA Na CCM, kama hakuna viongozi wa hivyo vyama basi kuna makada wake, ambao wanajulikana kwa majina yao, lakini cha ajabu sijawasikia wakikemea huu upuuzi unao endelea kila kukicha. Kwangu mimi inanipelekea kuamini kuwa wanayapenda haya yanayo endelea humu, kwa sababu ndio sera za vyama vyao. Na kama wanayakubali haya yaendelee humu ndani ya JF, yatashindikana vipi yasitokee huko nje kwenye utendaji!?

  Tusifikie mahala ikaonekana kuwa JF inapendelea matakwa ya watu au kikundi fulani cha watu. Na hii ni hatari sana kwani itasababisha chuki kati ya wanaJF, wakati sote tu Watanzania na tunaitakia amani na utulivu nchi yetu. Mimi nilitegemea wenye kutete vyama vyao, wangekuwa wanatetea kwa kutumia sera za vyama vyao na si kwa kutumia matusi.

  Teteeni sera zenu na kisha iachwe ridhaa ya wasomaji. Vitisho, ubabe, kashfa, matusi, upendeleo na kuitana majina yasio pendeza vitavuruga amani ndani ya JF...!

  Najuwa kuwa kuna watu wanajiona wao wana haki ya kutukana, kukashifu na hata kuwaita wengine majina yasio pendeza, hii yote ni kuishiwa kwa hoja za msingi na kutokuwa na uvumilivu. Kwani kuna ulazima gani kama umeishiwa hoja, utukane ili uonekane kuwa umeshinda? Tuache huu ubalakala wa kujitia kujua sana.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Maxence Melo ameshaanza kazi ya kuwapa ban...we wala usiwe na hofu,Blessing,Omr na Technology tayari washalimwa ban...na list inaendelea wiki nzima hii tangu Kamanda Mbowe akamatwe na humu ndani kuna shikashika aka ban...hadi kieleweke!!
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well said boss,naamini sio wote wataisoma waimalize hii post
   
 4. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena,
  Uongozi wa JF usipokuwa makini...mtandao wetu huu utapotea kwa kushitakiwa ya kwamba hautumiki kwa maslahi ya taifa bali ni chanzo na sehemu ya kulumbana kwa wakereketwa wa vyama vya siasa, the gov't may ban JF kwa maslahi ya umma (if any).
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I suggest more bans na more warnings,topic za kuchefua zifutwe,na wanao toa watu kwenye mada waonywe pia
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  CRAAAAAAAAAAAAAAAA.................... Hapana, sijaweka P mwisho :)

  Umenena Mkuu na huo ndiyo ukweli. Mijadala sasa imekosa maana kwani kila kikiandikwa, watu wanajadiliana kishabiki badala ya points. Mtu anapindisha mistari ili muradi ushindi uwe wake na akishindwa kabisa anamalizia kwa maneno ya dharau/matusi kwa wapinzani wake.

  Kibaya zaidi ni kuwa wapenzi wote wawili wanakuwa wanafahamu kabisa kuwa WANADANGANYA na hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo wenyewe wanaanza kuamini uongo wao huo...... Kasheshe kweli kweli.

  Jitu jana linakuja na kusema "Mbowe kauawa...." Hili kama ninaweza, ninalirushia VIRUS na kuharibu Computer yake.
   
 8. T

  T.K JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa mods na wao wamezidi kucheka na nanyi, wapo watu humu wanapost upupu kila bandiko, wako wengine kila likiandikwa jina anarefeer kwny udini na ukabila, lkn cha ajabu wanaachiwa wanazidi kupeta tu
   
 9. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,070
  Likes Received: 7,548
  Trophy Points: 280
  Sawa sawa kabisa
   
 10. Yousuph .M.

  Yousuph .M. Senior Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very true indeed,
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Umenena XP,naimiss sana ile JF ya enzi zile kabla ya June 2010.......Natamani Mods wairudishe ile JF ambayo ilifikia kipindi ikaitwa 'The Home of Great Thinkers......

  Dah.....................

  Mama,Kyoma,Dilunga,Kuhani,YournameisMine,bht,Charity,Game Theory,Icadon,Pundit,Bluray?,Ibrah,Kana Ka Nsungu,Nemesis,Next Level(anategea tegea siku hizi huyu),Sipo,Penny,Mbogela,Baba Mkubwa,Original Pastor,Ladislaus Modest,Asha Abdallah,Mwafrika wa Kike,Mwazange,Hauxtable,Kevo na wakuu wengine kibao ama wamepotea kabisa ama wanaingia JF kwa kusuasua kutokana hali ya hewa kuchafuka mara kwa mara kikubwa kikiwa ni u-CCM na u-CHADEMA....
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Umenena mkuu wangu
   
 13. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo ndiyo maneno.Watu hawana hoja kazi kupiga majungu mambo ya msingi yanaachwa.Umbea wa kutokua na hoja.Asiye na hoja ban impitie ili Jf ibaki kuwa a home of GREAT THINKERS iendelee kuelimisha watu na siyo kuchonganisha watu.
   
 14. notmar

  notmar Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  majina na sura za ajabu zilizoko humu zinaonyesha kuwa huu mtandao haupo makini,na most of them ni waoga thats why wanajificha.eg.picha ya hitler inafanya nini hapa?au kwa nini uweke picha ya jini wakati we ni binadamu.kama unaamini unachokisema hupaswi kujificha na unatakiwa uwe tayari kwa lolote litakalokufika.nashauri ufanyike usajili wa information za watu wote wanaotaka kuchangia humu or else discussion zetu zitachakachuliwa kila siku na hatufiki popote!
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Bila kuwasahau Mtaalam,Kilbark,Capitol Hill,Mbalamwezi,Morani75,Mchongoma,Mtanzania,Mzalendohalisi,Maane,MegaPyne,Uwiano Maalum,Mwalimu Zawadi,YE,Calnde,Mchaga,Shemzigwa na wengine kibao.............Inasikitisha sana aisee....

  Siku hizi hata mathread matamu kama hili hapa chini hayatokei:

  https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/20835-walinzi-wa-viongozi-mataifa-mbalimbali-reconstructed-2.html
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ILIFIKIA HATUA NILIKUWA ADDICTED NA JF......! NILIKUWA SIWEZI KOSA...HOJA MOTOMOTO, ZA UNDANI , ZENYE KUIBUA YALIYOJIFICHA KWA MASLAHI YA TAIFA.....!
  LO! Baadaye ...mambo yakaanza kwenda mrama.....SIASA ZA CHUKI,UHAFIDHINA,UBAGUZI,KUCHAFUANA,MATUSI NDO IKAWA MAHALI YANAPOPATIKANA NI JF...PICHA ZA KUDHALILISHA, KEJELI ,KUTAMANI KUMWAGA DAMU,MAWAZO YASIYO ENDELEVU NA KILA OVU!
  WE HAVE TO TURN BACK WHERE WE WERE
   
 17. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mkuu XP ulilosema ni point sana tatizo ni moja 2, ckatai kwamba hakuna ucdm na uccm hapa mjamvini ila wengi wanaoipinga au kuikosoa serikali wanaonekana ni wanacdm wala sijui ni kwanini!
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu, tatizo si kuwa wewe ni mwana Chadema, Mwana CUF au mwana CCM au wa chama kingine chochote kile. Kiinachotakiwa ni kupingana kwa hoja, na si kutumia matusi na kejeli. Mimi naamini kuwa hakuna chama au serikali isiyopingwa duniani.

  Sasa sisi wengine tusiokuwa na vyama, mnatuogopesha na siasa zenu za visasi. Mi natarajia watu washushe nondo za uhakika na waeleze mazuri ya vyama vyao, na ikiwezekana waielekeze serikali nini cha kufanya, pale linapotokea tatizo na si kuleta matusi....! Tanzania ni yetu sote, sasa msituhatarishie amani yetu.

  Mtakapoanza kuwatukana kuwa wanachama wa chama fulani i.e CHADEMA/CUF/CCM kuwa ni wajinga au kuwaita wapumbavu, unaye mtukana hapa kama si nduguyo ni nani!?

  Mimi binafsi nina ndugu kwenye vyama vyote hivyo, na tunaheshimiana, na wakati mwingine wananishawishi kujiunga na vyama vyao, lakini kwa bahati ghafi mimi si mpenzi wa vyama vyote hivyo, nipo neutral na ninaheshimu mapenzi ya kila mmoja.
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  cjui kama una adhi ya kusema ivi wakati wewe na wengine ndo mnaongoza kwa kejeli na matusi ktk mijadala ya maana. Nadhani ni muhimu Mods wawape onyo kali sana.
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,889
  Trophy Points: 280
  Tears!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...