johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,147
Kwa sasa kuna kutoaminiana kati ya vyama shirika katika uchaguzi mkuu wa 2020 nikimaanisha CHADEMA na ACT-Wazalendo. Kila kimoja kinalaumu kingine kwa maamuzi wanayochukua baada ya kufeli katika uchaguzi mkuu.
Sheria ya ushirikiano wa vyama vya siasa inataka pawepo mkataba wa kisheria unaoonyesha maeneo ya ushirikiano na jinsi mtakavyoshirikiana. Kadhalika mkataba ni lazima uingiwe miezi 3 kabla ya uchaguzi.
CHADEMA na ACT-Wazalendo hawakuzingatia matakwa ya sheria, Tundu Lissu alikurupuka tu akamkana mgombea urais wa Chadema Zanzibar na kumkumbatia maalimu Seif na chama kizima kikafuata mkumbo.
ACT- Wazalendo nao bila hata kujitafakari wakamtosa mgombea urais wao Mh. Membe ili kujipendekeza kwa Lissu.
Kama vyama hivi viwili vingezingatia sheria malumbano yaliyopo leo tusingeyasikia.
Maendeleo hayana vyama!