CHADEMA na ACT-Wazalendo wametuonesha Umuhimu wa ile sheria ya Ushirikiano wa vyama wakati wa Uchaguzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,559
Kwa sasa kuna kutoaminiana kati ya vyama shirika katika uchaguzi mkuu wa 2020 nikimaanisha CHADEMA na ACT-Wazalendo. Kila kimoja kinalaumu kingine kwa maamuzi wanayochukua baada ya kufeli katika uchaguzi mkuu.

Sheria ya ushirikiano wa vyama vya siasa inataka pawepo mkataba wa kisheria unaoonyesha maeneo ya ushirikiano na jinsi mtakavyoshirikiana. Kadhalika mkataba ni lazima uingiwe miezi 3 kabla ya uchaguzi.

CHADEMA na ACT-Wazalendo hawakuzingatia matakwa ya sheria, Tundu Lissu alikurupuka tu akamkana mgombea urais wa Chadema Zanzibar na kumkumbatia maalimu Seif na chama kizima kikafuata mkumbo.

ACT- Wazalendo nao bila hata kujitafakari wakamtosa mgombea urais wao Mh. Membe ili kujipendekeza kwa Lissu.

Kama vyama hivi viwili vingezingatia sheria malumbano yaliyopo leo tusingeyasikia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Umenena Ukweli, ni dhahiri kabsa pande hizi mbili sio rafki tena kama ilivyokuwa hapo awali na hii ni sababu ya kutofuata utaratibu juu ya kile walicho force kuita "muungano".

Matokeo yake saivi kila mmoja anamuona mwenzake mchawi.
 
UPINZANI WA BONGO UMEJAA UNAFIKI TU, KILA MOJA ANAANGALIA MASLAHI KWAKE. Ajabu ni pale wanapotofautiana na kukosoleana hadharani tena kwa viongozi wakubwa kama Zito, Seif na Lisu. Unajiuliza, wameshindwa nini kukaa kikao na kuamua mambo yao kimyakimya, au wanawaona watanzania ni MAZWAZWA kabisa. Inatia aibu kwao.
WAENDELEE KURARUANA HADHARANI ILI WATANZANIA WAWAJUE VIZURI KUWA WAPINZANI NI WACHUMIA TUMBO TU.
 
Umenena Ukweli, ni dhahiri kabsa pande hizi mbili sio rafki tena kama ilivyokuwa hapo awali na hii ni sababu ya kutofuata utaratibu juu ya kile walicho force kuita "muungano".

Matokeo yake saivi kila mmoja anamuona mwenzake mchawi.

Hawakuwa na muungano wowote acheni kupotosha, walikubali kuwaunga mkono baadhi ya wagombea. Hii ni faida kwao na fundisho zuri huko mbeleni. Iwapo wangekubali kushirikiana kisha waanze kuvurugana kwa ajili ya kuwinda mlo pangesumbua.
 
Haiwezekani uipe uhalali sheria kandamizi kwa kuegemea misunderstanding iliyojitokeza kati ya hivyo vyama viwili, think wider.

Kila mwenye akili timamu anajua fika dhumuni la kuanzisha hiyo sheria ni kuvibana vyama vya upinzani visitimize majukumu yao kikamilifu ili CCM ipate nafuu.
 
Tunazungumza Kila Siku
Hakuna Upinzania Tanzania
Upinzani Wa ID fake JF
Upinzani wa Twitter!!
Upinzani wakuropoka hovyo
Upinzani Kila mmoja Mjuaji
upinzani Usio Jua Kipi Ikisimamie!
Unacho Kiomba Leo Ndicho Utakacho kipinga Kesho!
Wapo wapo Tu
 
Yale Yale Ujuaji mwingi kumbe Vilaza Tu
 
Haiwezekani uipe uhalali sheria kandamizi kwa kuegemea misunderstanding iliyojitokeza kati ya hivyo vyama viwili, think wider.

Kila mwenye akili timamu anajua fika dhumuni la kuanzisha hiyo sheria ni kuvibana vyama vya upinzani visitimize majukumu yao kikamilifu ili CCM ipate nafuu.
Sasa mbona Lisu na maalimu Seif hawakutumia hiyo sheria na wamefeli?
 
Tunazungumza Kila Siku
Hakuna Upinzania Tanzania
Upinzani Wa ID fake JF
Upinzani wa Twitter!!
Upinzani wakuropoka hovyo
Upinzani Kila mmoja Mjuaji
upinzani Usio Jua Kipi Ikisimamie!
Unacho Kiomba Leo Ndicho Utakacho kipinga Kesho!
Wapo wapo Tu
Ni kama wale wanyama leo wako Tanzania kesho wako Kenya!
 
Sasa mbona Lisu na maalimu Seif hawakutumia hiyo sheria na wamefeli?
Unashangaa nini watu kutofautiana mitazamo? mbona hata ndani ya vyama wanachama hutofautiana sembuse nje ya vyama vyao?!

Kwani sheria ndio ingefanya watu wasitofautiane mitazamo? amsheni akili zenu.

Thread zako nyingi huwa nyepesi nyepesi sana, mara nyingi hauna logic bwashee, unazunguka zunguka tu kama mtoto, shukuru Mungu huwa tunajitahidi kukujibu hivyo hivyo tu.
 
Hawakuwa na muungano wowote acheni kupotosha, walikubali kuwaunga mkono baadhi ya wagombea. Hii ni faida kwao na fundisho zuri huko mbeleni. Iwapo wangekubali kushirikiana kisha waanze kuvurugana kwa ajili ya kuwinda mlo pangesumbua.
Kwani kuna dhambi gani ukikubali ukweli??
ushauri;kubalini ukweli kuwa mmshindwa,then mjipange kwa awamu ijayo. Simple and clear
 
Kilichotokea kwenye uchaguzi ule hata mtoto mdogo anajua haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Jaji Warioba kavumilia lakini ameona hawezi kukalia kimya uhuni.
 
Sasa mtapinga mpaka lini juu ta uchaguzi wa oct 28 2020??
Jipangeni upya tu.Kama EU wamewaruka,USA wamewaruka,China ndo uaiseme,sasa mtashtaki kwa nani huo upuuzi wenu??
Kwani ukikubali tu,mtapungukiwa nini??
 
CCM wanafanya siasa za hesabu kali sana.
Leo hii A.C.T na Chadema wanapaluwana kwenye mitandao.
Hoja za Lissu na wanachadema zinajibiwa na Maalim na Zito kabwe,CCM wame relax.
 
Sasa mtapinga mpaka lini juu ta uchaguzi wa oct 28 2020??
Jipangeni upya tu.Kama EU wamewaruka,USA wamewaruka,China ndo uaiseme,sasa mtashtaki kwa nani huo upuuzi wenu??
Kwani ukikubali tu,mtapungukiwa nini??

Kwani tunakataa ule uhanithi ili kuwaridhisha hao uliowataja? Na kama ni kuturuka wameturukaje labda? Wamesema uchaguzi ulikuwa wa haki? Tunasema hivi ule haukuwa uchaguzi, bali ukhanithi kama ukhanithi mwingine, hilo haijalishi nchi nyingine wanachukua hatua gani. Na huu ni msimamo wetu usiobadilika fullstop.
 
Mwezi wa pili vikao vya bunge vinaendelea.Mdee na wenzake wote 18 kutoka ufipani ndani ya bunge.Aidan kenan ndani.
Nandipo hapo mtafunga midomo yenu kwa FEDHEHA na aibu iliyo kuu itakuwa juu yenu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom