Chadema msisahau: Usipojiandikisha unapoteza haki yako ya kupiga na kupigiwa kura. Msije kulalamika baadae

Ni katika kukumbushana tu.

Nichukue fursa hii kumpongeza mbunge wa Arusha mjini mh Godbless Lema kwa kulielewa hili na kuwaandaa wapiga kura wake.

Maendeleo hayana vyama!


!
!
Kutokujiandikisha Na Kutokupiga Kura Vyote Nii Haki Yangu. Msituchoshe. Chaguaneni Tu Muendee Na Mishe Zenu
 
huu uchaguzi WA kulazimishana.
Unaonyesha ni jinsi Gani ccm na mwenyekiti wao wamewavunja moyo wa kupiga kura wananchi.
Maneno Kama."CCM ITATAWALA MILELE"
ndo chanzo cha kuwavunja moyo wananchi.
leo hii mnataka watu wajiandikishe.
Ila WASHINDI WENU MMESHAWAPANGA.
bado kutangazwa tu.
KUNA HAJA GANI YA KUPOTEZA MUDA KUPIGA KURA?.
kila anayepanda uvuna alichopanda
 
Mkuu CCM inawanachama 15milioni na wale oyaoya wasio wanachama wanaweza kuwa kama 10mil jumla 25milioni wanatosha kabisa mkuu
 
Ni katika kukumbushana tu.

Nichukue fursa hii kumpongeza mbunge wa Arusha mjini mh Godbless Lema kwa kulielewa hili na kuwaandaa wapiga kura wake.

Maendeleo hayana vyama!
hata wakipigiwa kura hawatatangazwa mpaka DED aoate maelekezo.haina haja wapite tu wenyewe
 
Ni katika kukumbushana tu.

Nichukue fursa hii kumpongeza mbunge wa Arusha mjini mh Godbless Lema kwa kulielewa hili na kuwaandaa wapiga kura wake.

Maendeleo hayana vyama!
Ajabu wanapigia debe watu wasijiandikishe ! Hawajiulizi hao wachache waliojiandikisha ni wa cjama gani ? Je, kuna maeneo upinzani una mpaka Halmashauri unaziongoza. Hivi wakishindwa kwa kishindo watadai ni 'bao la mkono !?'
 
Tumeshajiandaa kisaikolojia kuwa nchi inarudishwa kwenye enzi za ujima wa mfumo wa chama kimoja Kwa mabavu.
 
Kwani kuna uchaguzi au ni uteuzi wa wana ccm kutawala kwa maamuzi ya rais ambaye ndiye mwenyekiti wa ccm? Yaani nipoteze muda wangu kwenda kupiga kura wakati najua kabisa hiyo kura yangu wala haitaangaliwa bali wataamua tu fulani awe kiongozi na anakuwa?
Hao wabunge, madiwani na halmashauri zinazoongozwa na upinzani zilipatikana vipi !? Hakukosea aliyewaita 'malofa'
 
Watu wajiandikishe au wasijiandikishe, hakuna tofauti. Ukampigia mgombea wa CCM au usimpigie, ndiye atakayetangazwa. Hivyo ndivyo alivyowaamrisha wasimamizi wa uchaguzi. Hakuna msimamizi mwenye uthubutu wa kwenda kinyume na aliyemteua na anayedai anawalipa mshahara, japo hela siyo yake.
Hao akina Mdee, Mnyika, na Kubenea walipataje ubunge !? Hapa mtaani kwangu Diwani ni chadema na mwenyekiti ni chadema. Walipataje hawa ? Ulofa mbaya sana !
 
Upinzani komaeni. Tujiandikishe na tupige kura nadhani itatupa sauti na dunia itasikia. Wale wanaoiona tanzania ni mali yao wataishia kama Ghadaffi. Naunga mkoni tujiandikishe ili tutetee kura zetu kwa sauti.

Tukijificha tutaongozwa kama maiti tutoke tupaaze sauti kwa kura. Ila ipo siku wataona aiibu.
 
Back
Top Bottom