Chadema msisahau: Usipojiandikisha unapoteza haki yako ya kupiga na kupigiwa kura. Msije kulalamika baadae

Kwani kuna uchaguzi au ni uteuzi wa wana ccm kutawala kwa maamuzi ya rais ambaye ndiye mwenyekiti wa ccm? Yaani nipoteze muda wangu kwenda kupiga kura wakati najua kabisa hiyo kura yangu wala haitaangaliwa bali wataamua tu fulani awe kiongozi na anakuwa?
Uchaguzi upo tarehe 24/11/2019........ni uchaguzi wa kikatiba kabisa siyo uteuzi!
 
Ni katika kukumbushana tu.

Nichukue fursa hii kumpongeza mbunge wa Arusha mjini mh Godbless Lema kwa kulielewa hili na kuwaandaa wapiga kura wake.

Maendeleo hayana vyama!
Watu wajiandikishe au wasijiandikishe, hakuna tofauti. Ukampigia mgombea wa CCM au usimpigie, ndiye atakayetangazwa. Hivyo ndivyo alivyowaamrisha wasimamizi wa uchaguzi. Hakuna msimamizi mwenye uthubutu wa kwenda kinyume na aliyemteua na anayedai anawalipa mshahara, japo hela siyo yake.
 
Wati wajiandikishe au wasijiandikishe, hakuna tofauti. Ukampigia mgombea wa CCM au usimpigie, ndiye atakayetangazwa. Hivyo ndivyo alivyowaamrisha wasimamizi wa uchaguzi. Hakuna msimamizi mwenye uthubutu wa kwenda kinyume na aliyemteua na anayedai anawalipa mshahara, japo hela siyo yake.
Kwahiyo 2020 hamtapiga kura?
 
.... kumbe ccm mnajua upinzani nchi hii ni CDM pekee, japo huwa mnajitoa akili, mtapata ushindi wa aibu sana mwaka huu, na mwakani, sijui mtashangiliaje!
 
Unapiga kura anashinda hatangazwi,unapiga kura anashinda anatangazwa baada ya miezi michache anajihuzuru ili kuunga juhudi
 
Wanaogoma kujiandikisha siyo CHADEMA peke yao wapo hata wanaccm wengi tu wanaojitambua ambao wamegoma kujiandikisha kwa kutokuridhishwa na kile wanachofanyiwa watanzania wenzao kwa kisingizio cha kuwadhibiti wapinzani.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom