Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Bahati mbaya na wewe unasema kwa niaba ya watu wengine ambao unadai wako wengi, umejuaje nafsi za watu wengine.
Maneno mazito haya; sasa tunajua na tumeona tofauti ya watu wanaotaka mabadiliko ya kweli na wanaotaka mabadiliko tu. Wanaotaka mabadiliko tu hawana cha kusimamia isipokuwa kitu kibadilike tu. Hawajali ni mabadiliko gani, ya nini, kwanini na kwa vipi tu. Ni kama watu wanaopigishana stori kijiweni; mtu anaweletea stori za mpirani jinsi magoli yalivyofungwa na watu wanashangilia na kurudia jinsi kona ilivyopigwa n.k kumbe aliyewasimulia alisikia redioni tu. Wanataka tuamini kuwa Lowassa anawakilisha kweli mabadiliko! Hata kusema "CHADEMA" Lowassa maskini wa Mungu anapata tabu, halafu juu yake anatakiwa awakilishe UPAWA vile vile! Ili watu wapewe!
Ndio maana toka mwanzo nilishapuuzia huu UPAWA niliamini wakati ule kuwa ni dubwasha baya zaidi lililovuruga harakati za mabadiliko na litatusumbua baadaye. Lakini sikudhania lingetokea na la Lowassa vile vile. Sasa hivi CCM wala hawana haja ya kupiga kelele tena, wanasubiri vichinjio vyao wafutilie mbali upinzani tarehe 25 liwe onyo na somo kwa wengine!
Umefika golini kabisa na umebaki wewe na kipa mtu anakuonesha kisura halafu unabutua juu; hata wakionesha replay zile unashindwa kuangalia kwani ni aibu.
Mzee, nikisoma maoni ya wengi humu. Ni dalili tosha kuwa hata zile operesheni Sangara na M4C hawakuwa wanaelewa dhima yake hasa.Maneno mazito haya; sasa tunajua na tumeona tofauti ya watu wanaotaka mabadiliko ya kweli na wanaotaka mabadiliko tu...
Baada ya Dr. Slaa kung'atuka siasa za kitapeli za CHADEMA na washirika wake, tumeshuhudia manguli na viwanda vya propaganda wa CHADEMA wakitumia kila mbinu kutuaminisha kuwa kila kitu ni shwari ndani ya Chama hicho na kikundi cha UKAWA. Hoja nyingi zinazokosoa kitendo cha CHADEMA hususani UKAWA kuonyesha taswira ya kununuliwa na mgombea wake wa urais ambaye walipita nchi nzima na kutumia rasilimali nyingi ikiwemo damu na wengine kupata ulemavu kwa kumnadi ni FISADI papa pamoja na wenzake alioambatana nao. Hoja hizi hazijibiwi badala yake viwanda vya propaganda vimekuwa vikifanya CYBER BULLYING kwa yeyote anayehoji ama kukosoa.
Vinara wa uhuni huo wamekuwa wakiongea kwa kusema Dr. Slaa amechelewa na hakuna kinachobadilika na kinachoshangaza zaidi, yule waliyekuwa wanamnadi ni Rais wa mioyo ya Watanzania amepewa majina mapya ya Babu, Mzee, Kizee n.k. Pia wazungumzaji wanaotulazimisha tuwasikilize wao pekee wanajinasibu kuzungumza kwa niaba ya Watanzania wote. Hili ni kosa ambalo si muda mrefu watakuja kujutia na anguko lake si dogo.
Najua, nafahamu, natambua kuwa yeyote asomaye huu uzi anaelewa namaanisha nini lakini kwa kuwa tayari wengi wameshakula kiapo cha giza, wataporomosha matusi, kebehi na kubeza.
CHADEMA mnaodhani mmeshika mpini, tambueni kwamba Dr. Slaa hayupo peke yake. Kuna kundi kubwa la wanamageuzi wa kweli ambao wanamuunga mkono na wanajua cha kufanya ili kuondokana na upuuzi wa viongozi waroho kutaka kutumia njia za mkato kufanikisha malengo yao huku wakisigina misingi iliyofanikisha Chama kukubalika na wengi. Misingi ya kupambana na Ufisadi, ukiukwaji maadili ya uongozi na wizi wa amali za umma.
Dr. Slaa ni kioo, msimamo wake usiyoyumbishwa ni tunu pia ana mapenzi ya dhati kwa Taifa na watu wake.
Babu Slaa yuko na CCM waliomtuma na kumuhonga ,, Slaa amekodishiwa private jet kumpeleka Afrika Kusini akale ela alizohongwa na CCM