CHADEMA mnataka mteremshiwe gunia la chawa?

Baada ya ripoti ya tume ya jaji Manento ambayo ndio tume halali yenye mamlaka ya kisheria yanatakiwa yafanyike maandamano ya yasiyo kuwa na kikomo mkoani Iringa kuhakikisha kuwa Kamanda Kamuhanda,Mwema, chagonja na Nchimbi wanang'oka kwenye nafasi zao. Kuna mambo viongozi wetu wa chama wanatakiwa kuongozwa na busara lakini sio hili ambalo mara baada ya tukio chama kikapakwa matope kupitia vipindi vya kupika kwenye runinga.

1. Dr slaa.
2. Mbowe
3. Lissu
4. Zitto
Popote mlipo, amkeni mhamasishe umma wa wana Iringa ili kumtendea haki marehemu Daudi Mwangosi,ally zona na wengine wengi walio uwawa mikononi mwa Polisi, ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke ndio inatakiwa kutumika hapa kuwaondoa mabaradhuri walio sababisha vifo vya watanzania wenzetu! Chama kitatuangusha kama kitanyamaza baada ya kutolewa ripoti yenye nguvu za kisheria.

Tusisubiri kesho, tuanze sasa maana ukimya wetu ni mauti kwa wengine, 'hakuna kulala mpaka haki ipatikane, na ikipatikana wahusika wawe wameshapoteza nafasi zao'

Kama kweli wewe una uchungu anzisha maandamano yasiyo na kikomo ingia barabarani wewe familia yako makamanda watakufuata anza kesho.
 
Hapo anamtahadharisha tu kwakuwa serikali yenu dhaifu inajua kuonea wananchi wanyonge, hao polisi wakipigiwa simu kwamba majambazi wamevamia sehemu hawfiki hadi wajiridhishe kwamba wameshaondoka.

Chadema si waoga na ndio maana pamoja na vitisho, mateso na mauaji bado tu tunaendelea na movement zetu.

Movement gani wakati mmejificha JF ingieni barabarani kama mnavyopewa ushauri na Mwanakijiji, mnataka nini tena gunia la Chawa.?
 
Sijaona kosa la chadema. Kimya chao kimeleta funzo kubwa kwa jamii

Mkuu!
Ni kweli chadema haijafanya kosa. Na ni kweli ni funzo kwa jamii! Jamii imeshapata mafunzo ya kuzalilishwa ikiwa ni pamoja na raia wasio kuwa na hatia kuuwawa. Mara hii funzo linatakiwa liwapate vibopa wa serikali wanao jiona kuwa wao ni watanzania zaidi ya wengine na hivyo wana mamlaka ya kuamua nani afe na nani aishi.

Huu ndio wakati muafaka wa kukivunja kikombe cha kuwalinda waovu, wawajibike kutokana na makosa yaliyotokea na wafikishwe kwenye vyombo vya haki.

Machozi ya mke wa Daudi Mwangosi na watanzania kwa ujumla hayatakauka! Kamuhanda ang'oke maana mikono yake inavuja damu, hafai kuwepo kwenye nafasi yake, nchimbi nae hafai kuendelea kuwa waziri maana na yeye amekubikwa macho na sanda ya Mwangosi.
 
Hivi kuitisha kikao cha dharura cha kamati kuu au cha Sekretariet ya Chama inachukuwa muda gani? kuna mjumbe ambaye hana simu?

Zitto mbona kwenye mambo kama haya huwa sioni unaibu katibu mkuu wako? hapa ndipo tunapaswa kuona kwa vitendo matakamko na kauli Nzito cha chama na za Viongozi mmoja mmoja. Siasa za kuchekeana Watanzania hatuzihitaji kwa sasa, tunataka misimamo Radical.
 
Kama kweli wewe una uchungu anzisha maandamano yasiyo na kikomo ingia barabarani wewe familia yako makamanda watakufuata anza kesho.

Siwezi kubishana na wewe maana unafikiri kwa kutumia tumbo. Ripoti ya jaji Manento imemvua Nchimbi na kamati yake hadhi ya kuendelea kushikilia nafasi zao, leo tumia akili kidogo kwa kuisoma ile ripoti ya Manento ndio upitie Lumumba kuchukua mkate wako wa wana. Leo nikwa Mwangosi kesho ikitokea kwa nduguyo hata hicho ki-lap top ulicho pewa ili uchangie ***** humu utakivunja na kukirejesha Lumumba.

Think or sink out of Pandora box.
 
Siwezi kubishana na wewe maana unafikiri kwa kutumia tumbo. Ripoti ya jaji Manento imemvua Nchimbi na kamati yake hadhi ya kuendelea kushikilia nafasi zao, leo tumia akili kidogo kwa kuisoma ile ripoti ya Manento ndio upitie Lumumba kuchukua mkate wako wa wana. Leo nikwa Mwangosi kesho ikitokea kwa nduguyo hata hicho ki-lap top ulicho pewa ili uchangie ***** humu utakivunja na kukirejesha Lumumba.

Think or sink out of Pandora box.

Wewe ambaye unafikiri vizuri anzisha maandamano Dr Slaa yeye atakuwa hoteli kapumzika nyie ndio mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana na polisi kuwakomboa watanzania au nyie maandamano yenu mnayafanyia JF.
 
Naona kila mmoja anajitoa anamsukumizia mpira mwenzake kama kweli Chadema mpo na mnakubalika mnataka nini.

ndugu ,ni wewe kweli au kuna mtu anatumia account yako yaani siku hizi ume change au umetoswa kwenye NEC?:biggrin:
 
Kuna watu humu wameshaanza kuwashwa.

Maandamano+Chade.jpg
 
Wewe ambaye unafikiri vizuri anzisha maandamano Dr Slaa yeye atakuwa hoteli kapumzika nyie ndio mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana na polisi kuwakomboa watanzania au nyie maandamano yenu mnayafanyia JF.

Kwa taarifa yako hapa ni daraja tu la kupasha na kupeana taarifa (unajua kuwa hapafai maandamano, acha pumba!) nimekuwa kwenye harakati nyingi za chadema na hata maandamano ya Arusha ambayo polisi waliuwa kama walivyofanya kwa Mwangosi nilikuwepo, sina woga wa kuandamana kwa kile ninacho kiamini kama hili tunalo jadili.
 
  • Thanks
Reactions: ral
Kwa taarifa yako hapa ni daraja tu la kupasha na kupeana taarifa (unajua kuwa hapafai maandamano, acha pumba!) nimekuwa kwenye harakati nyingi za chadema na hata maandamano ya Arusha ambayo polisi waliuwa kama walivyofanya kwa Mwangosi nilikuwepo, sina woga wa kuandamana kwa kile ninacho kiamini kama hili tunalo jadili.
Don't waste you're valuable time kubishana na Anonymous. wewe ni Verified user huna la kuogopa.
 
h.sep7.gif
CHADEMA kujadili ripoti za Mwangosi


na Abdallah Khamis


amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa kinakusudia kufikisha ripoti za kamati mbalimbali zilizochunguza mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha television cha Chanel Ten katika kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa ajili ya hatua zaidi.
Hata hivyo, mbali ya hatua hiyo, chama hicho kimesisitiza kuwa ni wakati muafaka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emanuel Nchimbi, kuachia nafasi au awajibishwe na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutumia fedha za wananchi kwa kamati waliyodai haikuwa na jipya juu ya mauaji ya Mwangosi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri Kivuli wa Wizara hiyo, Vicent Nyerere, alisema wao kama chama wameona watoe tamko la awali wakati wakisubiri majumuisho ya pamoja kwa ajili ya hatua zaidi.
"Serikali toka awali haikuwa na nia ya kuonesha upungufu uliosababisha kifo cha Mwangosi, na kwa kutambua hili Nchimbi aliunda kamati yenye lengo la kuisafisha jeshi la Polisi kwa kutumia kodi zetu,"alisema.
Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Mjini, aliongeza kuwa ni jambo la ajabu kwa mtu kama Nchimbi kukubali kupokea ripoti ya ajabu na yenye kumdhalilisha kisha akasimama hadharani kuitetea.
Alisema ni wakati muafaka kwa Rais Kikwete kumfuta kazi Dk. Nchimbi kwa kuwa ameshindwa kujitathmini kutokana na mauaji yanayotokea sehemu mbalimbali hasa katika matukio ya kisiasa ili liwe fundisho kwa viongozi wengine katika kusimamia majukumu na maslahi ya Taifa.
Nyerere alibainisha kuwa namna kamati ya Dk. Nchimbi ilivyofanya kazi, imeshindwa kuwaelewesha watanzania kiini cha kifo hicho licha ya kutumia kodi zao, hivyo kushauri kuwa inapaswa kuundwa tume ya kimahakama.
Kuhusu maoni ya kamati ya Dk. Nchimbi juu ya shughuli za kisiasa kuishia bungeni baada ya uchaguzi, Nyerere alisema ni jambo la kushangaza kama leo Bunge litakuwa sehemu ya kunadi sera badala ya kuzungumzia matatizo ya wananchi.
"Kama kamati iliyo chini ya Jaji Ihema ndiyo imekuja na mtazamo huu wa kutaka shughuli za kisiasa na mijadala yake ifanyikie bungeni basi ninasisitiza kauli ya Tundu Lissu juu ya kumpinga Jaji huyu mstaafu ni muhimu zaidi,"aliongeza Nyerere.
Alisema ripoti ya kamati ya Nchimbi ingeweza kutoa taarifa zote hadharani bila kuingilia uhuru wa mahakama na kwamba alitaraji kuona ikiwagusa viongozi wa serikali moja kwa moja wanaoingilia shughuli za vyama vya siasa.
Kamati tatu tofauti zimetoa ripoti zake kuhusiana na mauji ya Mwangozi ambapo ile ya Baraza la Habari Tanzania na Jukwaa la Wahariri pamoja na ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, zimeeleza wazi kiini cha mauji hayo na kuwataja waliohusika.
Hata hivyo ripoti ya kamati iliyoundwa na Waziri Nchimbi ililalamikiwa kutokana na kushindwa kuweka taarifa kamili wazi kwa madai kuwa kesi ya mauaji hayo iko mahakamani.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom