CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

Status
Not open for further replies.
HAMMY-D, msalimie sana RAMA (Ighondu).......mwambie wachina now wameleta plaizi zina Bluetooth, zinatoa watu meno bila kuwateka...zipo kariakoo!
 
Mkuu, ukiona mtu mzima anatoa chozi hadharani ujue kuna jambo, ni kheli CDM warudishe moyo wao nyuma na wamfikilie kijana Ludo.
Watarudishaje moyo nyuma wakati unakaa kifuani upande wa kushoto..
 
Nimeyasoma maelezo yako mkuu na kwa namna unavyomuelewa ni kuwa ana uhusiano wa karibu na Chadema...

Sasa swali jingine, "Je hizi tuhuma zinazomkabili na kupelekewa kushikiliwa na Vyombo husika zina uhusiano gani na Chadema?"

Pia swali la pili ni hilo alilouliza Matola hapo juu...

"Na unaweza kutueleza yeye na Maggid Mjengwa wana uhusiano gani au alikuwa anafanya nini na Maggid?"

Ok, Ludo kipindi yuko UDSM-DUCE alikuwa ni miongoni mwa vijana wana harakati wa kukijenga CDM, hasa kupitia jumuiya ya CHASO ambayo Mwampamba ni mwasisi wake.

Kijana huyu alivyo maliza masomo yake akaacha vyote, na kwenda kukitumikia CDM makao makuu, hii sacrifice sio ndogo mkuu.

Pale makao makuu, alikuwa chini ya uangalizi wa Lwakatare katika majukumu yake, pia alikuwa mtu wa muhimu sana kwa Dr Slaa hasa katika masuala ya intelligence.

Mkuu, hapa bado ujaona nafasi ya huyu kijana ilivyo nyeti na muhimu kwa chama?
 
Last edited by a moderator:
Sasa mkuu utafananisha shughuli za blog na chama?

You can't be serious!
Am serious, huyu anapata hukumu yake hapa hapa Duniani, kwanza ashukuru hata hiyo dhamana kuwa wazi ni kazi ya timu ya Mawakili wa Chadema.

Swala la mtu kuwekewa dhamana ni la kifamilia zaidi na kirafiki, ndio maana nimekuuliza swali rahisi sana j kina Maggid Mjengwa wako wapi?

Tuasume kwamba Chadema imetelekeza what is plan B kwake? mtu mwenye Connection na watu wakubwa na wazito kama Mwigulu ni kwa nini akae jela wakati dhamana iko wazi? shirikisha ubongo wako kuna kitu marafiki zake wanakijuwa na Maggid Mjengwa atakuwa anajuwa zaidi.

Usilete siasa uchwara kwenye fact kama hizi, changudoa tu Lulu baada ya kukubaliwa dhamana amedhaminiwa mara moja why not Ludovic?
 
Kwani Mwigulu bado hajamwekea dhamana? Mshahara wa dhambi ni mauti. Na hili linatakiwa liwefunzo kwa vijana mnaokubali kununuliwa na kutumiwa katika uovu kuachana na tabia hii ovu. fanyeni kazi halali mpate utajiri wa halali na si kutamani kutajirika kwenye uovu.
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezaura ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna yake, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.
 
Ok, Ludo kipindi yuko UDSM-DUCE alikuwa ni miongoni mwa vijana wana harakati wa kukijenga CDM, hasa kupitia jumuiya ya CHASO ambayo Mwampamba ni mwasisi wake.

Kijana huyu alivyo maliza masomo yake akaacha vyote, na kwenda kukitumikia CDM makao makuu, hii sacrifice sio ndogo mkuu.

Pale makao makuu, alikuwa chini ya uangalizi wa Lwakatare katika majukumu yake, pia alikuwa mtu wa muhimu sana kwa Dr Slaa hasa katika masuala ya intelligence.

Mkuu, hapa bado ujaona nafasi ya huyu kijana ilivyo nyeti na muhimu kwa chama?
Ilikuwaje akamuuza msimamizi wake? Kumbe CCM ni wabaya sana!
 
Hoja nyingine bwana; Utata mtupu!! tafadhali do the right thing, achana na hadithi za kilio cha samaki, Ludo anavuna alichopanda; kijana mdogo mwenye akili timamu akarubuniwa akakubali kurubunika!! wasiliana na hao waliomrubuni wajitokeze wakamsaidie sio CDM tena.

Ludo alipashwa kujua kwamba CHOICES HAVE CONSEQUENCES!!; it is payback time boyo!
 
Kama Mwigulu a.k.a savimbi aliweza kumpa elfu hamsini baada ya kufanya kazi yake, inakuwaje ashindwe kumdhamini ili aweze kuwasaidia kwenye ushahidi wake. Hayo ndiyo matarajio yake aliyotegemea baada ya kazi zake za YUDA ISKARIOTI.
 
Mkuu, hiyo iwe fundisho kwa vijana wengine walio bega kwa bega na CDM, kwani hawawezi kujua hamta yao wenda yaweza kuwakuta haya haya Ludo.
Kwani ile 50000 aliyotuma Mwigulu kupitia M-pesa kwenda kwa Ludo ilikuwa ya nin vile,mwambie bi shoza na mwampamba Nchemba anatafuta choo cha kuwaweka,Ludo keshapata..
 
Usijifanye kutia watu woga wewe Mwigulu, wala usijali Chadema wanataka hiyo kesi iende mahakamani na mkileta majaji wenu wa kupandikiza tunawakataa kisha anateuliwa ambaye hajui kupindisha sheria na hapo ndio tutakuona kama utakuja kuleta ule ushahidi unaojifanya kuwa unao huko bungeni na kwenye media. Kwanza tunaona kama siku zinachelewa za hiyo kesi. Mbona watanzania wanaojitambua wameshawashtukia wanangoja tu muuingie kwenye anga zao
duh!!!!! do i sound like MWINGULU NCHEMBA???? hebu nitake radhi dada yangu.
huyo mwingulu ni kidume kwa wanachadema ila kwangu mimi sio lolote sio chochote. simchukulii kama mwanasiasa hodari ila namchukulia kama jibu sahihi kwa sisa za kijinga za chadema.... LOL
 
Am serious, huyu anapata hukumu yake hapa hapa Duniani, kwanza ashukuru hata hiyo dhamana kuwa wazi ni kazi ya timu ya Mawakili wa Chadema.

Swala la mtu kuwekewa dhamana ni la kifamilia zaidi na kirafiki, ndio maana nimekuuliza swali rahisi sana j kina Maggid Mjengwa wako wapi?

Tuasume kwamba Chadema imetelekeza what is plan B kwake? mtu mwenye Connection na watu wakubwa na wazito kama Mwigulu ni kwa nini akae jela wakati dhamana iko wazi? shirikisha ubongo wako kuna kitu marafiki zake wanakijuwa na Maggid Mjengwa atakuwa anajuwa zaidi.

Usilete siasa uchwara kwenye fact kama hizi, changudoa tu Lulu baada ya kukubaliwa dhamana amedhaminiwa mara moja why not Ludovic?
Kama swala la dhamana ni la kifamilia mbona lwakatare ambaye walipanga pamoja na lwakatare yeye lwakatare kahangaikiwa na chadema.

Anyefaa hukumu hapa duniani ni lwaka kwa unyama aliotaka kufanya kwa msack lakini ludo hana dhambi.
 
Watarudishaje moyo nyuma wakati unakaa kifuani upande wa kushoto..

NattyDread,

Hahaha... mkuu unanichekesha wakati nipo katika hali ya huruma na masikitiko makubwa kwa kijana Ludo?

Basi ngoja niseme watafute nafasi kwenye mioyo yao (popote ilipo) ya kuweza kumsaidia kijana Ludo kwa dhamana.

Hii itasaidia kukipa CDM heshima kubwa na itafanya kudhihirisha ukomavu wa viongozi wa CDM hususani katika kutatua matatizo.
 
Last edited by a moderator:
Nenda kamtoe wewe mama au mumeo mwigulu nchemba akamtoe..nyie si mlimtumia kwenye mpango mzima wa kuratibu huo upuuzi.kazi mnayo maccm
 
Kwani ile 50000 aliyotuma Mwigulu kupitia M-pesa kwenda kwa Ludo ilikuwa ya nin vile,mwambie bi shoza na mwampamba Nchemba anatafuta choo cha kuwaweka,Ludo keshapata..
Hoja ambazo hazina uthibitisho unachukua maneno ya lisu ndiyo udanganye nayo lisu mwenyewe yawezekana siku hiyo ulikuwa mwezi mchanga kwake.
 
Back
Top Bottom