CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

CHADEMA, Ludovick Rwezahula anaangamia mahabusu, utu uko wapi?

Status
Not open for further replies.
Tupo imara tunajenga taifa letu tumethubutu,tukaweza,tunazidi kusonga mbele,kwa jinsi slaa alivyo na chuki na kwa vile ludovick aliibua uozo wao slaa hataruhusu kijana yule atoke but all in all yai litawatobokea tu.

mkuu kimya kitambo! bt kimya chako hakina mshindo nakushauri ukipewa kazi kama hii na mwigulu usiifanye hata chembe. namwonea kijana huruma sana na nahisi anajuta na atajuta kushirikiana tena na mwigulu ktk harakati kama hizi. hiv kes yake dhamana ya 48,500 inafaa? maana ndio ujira aliopewa
 
Kijana wa Bavicha katelekezwa, Chadema mna jopo la wanasheria msaidieni huyu kijana.

Na wewe msengerema unaongea nn unadhan Chadema ni wapumbavu kama babayo aliyeweka mtwara rehan kwa wachina ili kuku okoa na kitanzi ulipokamatwa na madawa nchini kwao?subir na wewe dawa yako iko jikoni,mwenzako akinyolewa zako tia maji ngurue pori wewe.
 
Labda nikuulize tu swali dogo, ni nini nafasi ya Ludovick Chadema pengine sielewi

Mkuu, binadamu apaswi kuhukumu hivyo. Sisi wote ni wakosefu, ni Mungu tu ndiye alietakasika. Kwanini binadamu tuwe na jeuri ya kuhukumu kwa namna hiyo?

Ndio maana Kikwete kwa kutambua hilo, a-support suala zima la hukumu ya kifo. Ndio maana ameweka kauzibe kwenye kusaini ili wahukumiwa kuuwawa wasifanywe hivyo.

Huu sio udhaifu, bali ni utu.
 
Hilo liwe ni fundisho kwa wote wanaokubali kutumika na kuuza utu wao kwa ajili ya tamaa ya pesa.
 
Bun ndio tunda gani wewe mbulula!! nenda shule badala ya kukimbilia hapa JF kueneza umbeya wakati hata kuandika hujui, hebu wahi kule jukwaa la elimu panakufaa ukishaelimika ndio uje hapa.
Mkuu ulizaliwa kwenye mtalo wa maji machafu? Jaribu kujitazama tatizo lenu bavicha mnatumika mpaka hamjitambui mtakufa kwa kutumika.
 
kama HUyu jamaa hata ndugu zake hawa mmind, sasa Dr. afanyie nini?

Mkuu,

Hiyo siyo maana yake, ndugu zake hawaendi mahakamani sio kwamba hawam-mind, hapana, ila wengi wao wapo Bukoba na wana hali mbaya kimaisha.

Unatarajia wataweza kusimamia dhamana kweli? Dr Slaa alirudishe moyo wake na akumbuke fadhira za kijana Ludo katika kukijenga chama. Haya yote amejisahaulisha?
 
Mkuu HAMMY-D, ingekuwa CDM wamekurushia wewe 50,000/- ili umrekodi Mwigulu, by now ungekuwa huna kucha ,huna meno ya mbele na pengine ungekuwa ushatumbukizwa kisimani!
 
mkuu kimya kitambo! bt kimya chako hakina mshindo nakushauri ukipewa kazi kama hii na mwigulu usiifanye hata chembe. namwonea kijana huruma sana na nahisi anajuta na atajuta kushirikiana tena na mwigulu ktk harakati kama hizi. hiv kes yake dhamana ya 48,500 inafaa? maana ndio ujira aliopewa
Mkuu yeye hakupenda uharifu uliokuwa unafanywa na chadema.

kitendo cha kudhuru watu hakikubariki kijana ni mzalendo anateswa na uzalendo wake lakini haya yanamwisho mungu atamwinua tu.
 
Mkuu ulizaliwa kwenye mtalo wa maji machafu? Jaribu kujitazama tatizo lenu bavicha mnatumika mpaka hamjitambui mtakufa kwa kutumika.

1016130_616543391703911_1333343654_n.jpg
 
Mkuu,

Hiyo siyo maana yake, ndugu zake hawaendi mahakamani sio kwamba hawam-mind, hapana, ila wengi wao wapo Bukoba na wana hali mbaya kimaisha.

Unatarajia wataweza kusimamia dhamana kweli? Dr Slaa alirudishe moyo wake na akumbuke fadhira za kijana Ludo katika kukijenga chama. Haya yote amejisahaulisha?
Mkuu huyu kijana alienda kuombwa kwao na lwakatare na akaja kukabiziwa kwa slaa.

jamii yote inafahamu kuwa yupo mikononi mwa chadema ,dhambi hii chadema hawataikwepa.
 
Labda nikuulize tu swali dogo, ni nini nafasi ya Ludovick Chadema pengine sielewi

Ok, Ludo kipindi yuko UDSM-DUCE alikuwa ni miongoni mwa vijana wana harakati wa kukijenga CDM, hasa kupitia jumuiya ya CHASO ambayo Mwampamba ni mwasisi wake.

Kijana huyu alivyo maliza masomo yake akaacha vyote, na kwenda kukitumikia CDM makao makuu, hii sacrifice sio ndogo mkuu.

Pale makao makuu, alikuwa chini ya uangalizi wa Lwakatare katika majukumu yake, pia alikuwa mtu wa muhimu sana kwa Dr Slaa hasa katika masuala ya intelligence.

Mkuu, hapa bado ujaona nafasi ya huyu kijana ilivyo nyeti na muhimu kwa chama?
 
Na unaweza kutueleza yeye na Maggid Mjengwa wana uhusiano gani au alikuwa anafanya nini na Maggid?
 
Mkuu HAMMY-D, ingekuwa CDM wamekurushia wewe 50,000/- ili umrekodi Mwigulu, by now ungekuwa huna kucha ,huna meno ya mbele na pengine ungekuwa ushatumbukizwa kisimani!

Kwa haya maelezo yako ina maana ile video ni ya kweli?

Ina maana ni kweli Lwakatare alipanga mbinu haramu dhidi ya wana habari?

Hii inaelekea patamu mno, maana naona hata wana CDM mmeanza kuliona hili.
 
Ludovick ni miononi mwa vijana wenye uzalendo wa hali ya juu sana ni mfano wa kuigwa.

haijawahi kutokea mtenda haki na mzalendo akaachwa na mungu lazima mungu yuko na yeye.
 
Na unaweza kutueleza yeye na Maggid Mjengwa wana uhusiano gani au alikuwa anafanya nini na Maggid?

Sasa mkuu utafananisha shughuli za blog na chama?

You can't be serious!
 
Mkuu,

Hiyo siyo maana yake, ndugu zake hawaendi mahakamani sio kwamba hawam-mind, hapana, ila wengi wao wapo Bukoba na wana hali mbaya kimaisha.

Unatarajia wataweza kusimamia dhamana kweli? Dr Slaa alirudishe moyo wake na akumbuke fadhira za kijana Ludo katika kukijenga chama. Haya yote amejisahaulisha?
kujenga chama si hoja, siunajua umammruki? umewasahau juliana mwambapa? wanafiki ni wakarim kuliko watu wema.
Mzee kama unahuruma naye kamtoe, lakini kama haupendi usaliti mwache aendelee kun debe! sasa tunataka tuwe na watanzania wenye watu wa nia njema
 
Loh! naona leo mlikuwa na kikao cha kipropaganda kuhusu ludovik, mnampenda kuliko hata wa CDM wenyewe, hii inatia shaka.
Hayo ni malipo ya usaliti, na zaidi baada ya 2015 watu wengi zaidi watajuta kwa wanayo yafanya sasa na kujificha nyuma ya serikali
 
WanaJF!

Leo ni siku ya kesi ya bwana Lwakatare kusikilizwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini kesi imehairishwa mpaka July 22, 2013.

Pamoja na hayo, mshitakiwa na.2 bwana Ludovick Rwezaura ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokamilika kwa nyaraka za dhamana, ingawa dhamana yake iko wazi kabisa.

Bwana Ludovick akiwa nje ya mahakama, ameonekana akiwa mnyonge na alikuwa akilia sana kwa uchungu huku akilalamika ndugu zake (ambao hawakufika mahakamani) hawafatilii dhamana yake.

Kwa hali kama hiyo, kijana Ludovick anaendelea kusota gerezani na kuzidi kuangamia, kwani wote sisi ni wanaadamu na tunajua makali ya maisha ya gerezani.

Rai yangu kwa CHADEMA; haijarishi kijana Ludovick kama alikuwa mwajiriwa wa CHADEMA kimkataba ama alikuwa volunteer, jambo la msingi ni kwamba alikuwa ana kitumikia CHADEMA kwa moyo wake wote na nguvu zake zote. Ludovick alijitoa kwa CHADEMA kwa namna yake, ni kijana ambae alikuwa bega kwa bega na Dr Slaa kiutendaji na vile vile alikuwa kama mtoto kwa Dr Slaa.

Katika hali kama hiyo sikutarajia kama CHADEMA kinaweza kumtema na kumkataa kabisa bwana Ludovick Rwezaura. Kwani wote tunafahamu kuwa, kosa aliadhibiwi kwa ubaya, bali kosa dawa yake kukosolewa. Sasa kwanini CHADEMA wana muadhibu kijana Ludovick kwa ubaya? kwanini wasimsaidie hata kwa dhamana ili aweze kutoka kwenye 'jehanamu' ya duniani?

Maamuzi haya ya kumtupa mkono kijana Ludovick katika hali hii mbaya inayo mkabili, inajenga wasiwasi mkubwa kwa vijana wengi walio CHADEMA juu ya hatma yao endapo wakikosea jambo. Je, chama kitawasaidia kwa lolote? Ni wakati vijana wakawa makini sana na namna ambavyo CHADEMA na viongozi wake wana shughulikia nidhamu na makosa ya wanachama wao, hiki anacho fanyiwa Ludovick, hakina tofauti sana na walicho fanyiwa Juliana Shonza na Mtela Mwampamba.

View attachment 101283Kijana Ludovick akionekana amenyong'onyea leo mahakamani, pembeni yake ni bwana Lwakatare wakiwa na askari magereza.

ni guts gani utakazo tumia kumsamehe msaliti?popote pale duniani adhabu ya msaliti ni kifo,muache ajifie taratibu kwani kinafsi ameshakufa na kilichohai ni kiwiliwili tu,unazungumzia kumtendea haki ndugu ludoviki,kumuonea huruma,mbona yeye hakuwa na huruma kwa Lwakatare na CDM kiujumla?kama yeye alishindwa kutuonea huruma kivipi sisi tumuonee huruma mkuu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom