CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
asante ya nini ? kwani mshapata solusheni ya matatizo ndani ya chama chenu au ??

KadaMpinzani,

Mimi kama Mtanzania asiyekuwa na Chama, nadhani CHADEMA haijawa na matatizo mpaka sasa!!! Ingawa nakubali kwamba hii ndio mitihani ya kukifanya chama kiwe imara zaidi,pale wanapoishinda...

Na kwa kweli CHADEMA haijapata mitihani ya kutosha ya kukifanya kipewe alama halali za ukomavu zaidi. Nafikiri haka ni kama kajaribio tu!

Kwa sasa mimi nawatakia Mkutano Mwema, kwa kuwa CHADEMA imara ni muhimu kwa mustakabali ya Taifa letu!
 
Sioni kwa nini Zitto ajitoe.....
Kwa mtazamo wangu hapa Zitto amechaguliwa kama Zitto na sio kama CHADEMA. Na hili ni suala la kitaifa sio about CCM or CHADEMA.
 
Sioni kwa nini Zitto ajitoe.....
Kwa mtazamo wangu hapa Zitto amechaguliwa kama Zitto na sio kama CHADEMA. Na hili ni suala la kitaifa sio about CCM or CHADEMA.

Mama

Ingawa nakuunga mkono Zitto asijitoe kwa sasa ili aingie ndani na kujua ufisadi wao akiwa ndani, sikubaliani nawe kuwa Zitto hakuchaguliwa kama CHADEMA. Zitto angekuwa CCM asingechaguliwa kwa kuwa Rais alisema anaingiza wapinzani kwenye kamati, na Zitto ametambulishwa katika kundi la kutoka upinzani. CHADEMA inawachama wengi naamini katika chama chao lakini Zitto atakuwa ameteuliwa kutokana na matokeo ya sakata la Buzwagi. Kwa hiyo Zitto sio kama Zitto hapo, Zitto ana WANANCHI na CHADEMA. Lazima yote hayo yazingatiwe katika mjadala huu, akiaabisha au akiabika kuna watu na taasisi zitaaibika naye. Ulikuwa wa wapi Mama, nimekumiss?

Dada Asha
 
No wonder mtabakia wapinzani forever!
FD,
Naona taratibu umeanza kua mtazama upande mmoja wa shilingi.
Kwa mtazama pande zote tungetarajia atupe faida na hasara za uteuzi huu kwa Zitto binafsi, CHADEMA na Taifa kwa ujumla.
Ni kukumbushana tu mkuu!
 
Hivi kweli watu nyie mnakaa na kuanza kubishana na Kada ? Kada is the guy ambaye yeye ni kushabikia na kungojea kasoro za Upinzani aseme . Hana mwelekeo wala si mkata issue ila huleta vijineno vya kitoto siku zote .Yeye ni nazi na mnazi wa CCM kwisha kazi yeye tanzania na watanzania si kitu kwake . Kwa mara ya kwanza ama pili naona kaleta mada ya ku copy magazetini huku akiwa anajua kwamba CCM wanataka pa kutokea so the way forward ni kujaribu ku create chaos kwa gharama yeyote ile . Hili halitafanikiwa .
 
Kada na wanazi wenzie wanashangaa kuona CHADEMA wanaitana kujadili mawazo yao tofauti kinyume na walivyozoea ndani ya CCM ambako wale miungu watu wakishatamka kitu ndio imetoka hiyo hakuna kupingana kimawazo. Kuleta tofauti ya mawazo kwao ni kuwa "SIO MWENZETU".
Jambo hili la Zito na kamati ya madini jinsi linavyochukuliwa ndani ya CHADEMA ndio njia sahihi inayotakiwa kwani kila mtu ndani ya kamati kuu atatoa mawazo yake kisha watatoka na msimamo mmoja. Huu ndio ukomavu unaotakiwa na inaonyesha hakuna mwenye miliki binafsi ndani ya hicho chama kuweza kuagiza atakacho kifanyike.
Tunakitakia kheri kikao chao,na kama ilivyo kawaida ya CHADEMA tunajua busara na maslahi ya taifa ndiyo yatakayopewa kipaumbele.
 
Upinzani wa Tanzania bado haujakomaa kisiasa, nilishasema hili na nitarudia. Zitto kujitoa haitoathiri CHADEMA, bali itaathiri Watanzania. Zitto ni muwakilishi wa walalahoi, nasio muwakilishi wa Tundu Lissu au Mbowe. Kwenye nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida wapinzani na chama tawala kuunda tume kwa mafanikio ya nchi.

Hizi propaganda kwamba Mbowe arudi kutoka masomoni, sijui nani asema nini ni BS. Hii inaonyesha ni jinsi gani Mbowe na wenzie hawajakomaa kisiasa. This shows the weakness with in CHADEMA. Poor strategy with in CHADEMA will put CCM on map again, Hiki chama kinaonyesha hakina washauri wa kisiasa, na kinajali faida binafsi na sio faida ya Tanzania.

This is a litimus test kwa CHADEMA, and CCM is watching them kwa karibu sana.
 
KADA MPINZANI! Acha uvivu wa kufikiri, tazama dunia kwa mapana na marefu, jifunze namna ya kusoma alama za nyakati, Jivunie kuwa mzalendo wa nchi yako na uwe tayari kuitetea na kuipigania, usikubali kupewa kipande cha muhogo ukatoa maamuzi yenye kuangamiza jamii yako!!
Gday!
 
Mimi nafikiri hakuna haja ya Zitto kujitoa kwani upinzani unaitaji kushirikiana na serikali kuokoa mali za Watanzania wao wakiwa msitari wa mbele.
Sioni tatizo la final report ikisuport mikataba kwani Zitto kama Zitto kama hakubaliani na final report anaweza kuwasilisha ya kwake nafikiri taratibu zinaruhusu kufanya hivyo.
Hii ni nafasi ya pekee kwa Wapinzani kuonyesha jinsi gani wanaweza kutetea Watanzania.
Sidhani kama Mheshimiwa Zitto ana njaa ya posho za vikao, ila ansukumwa na masilahi ya Tanzania.

Kada mpinzani yeye amebobea kwenye CCM anasahau hata watanzania wenzake, kwa kuleta ubishi ambao haujengi nchi yetu.
 
So far naona hapa we are trying to create something out of nothing. Mzee Mtei keshamaliza yote hapa kwa msimamo wake. Uteuzi wa Zitto kwanza mi naupongeza na hii inaonyesha kwamba at long last viongozi wetu wanaamka, though siyo kwa spidi ambayo mimi na wewe tungependa.

Hii ni kamati na sijui wanafanya kazi kivipi ie by concensus or by voting, lakini what is clear ni kwamba Zitto ataweka mchango wake na msimamo wake kwa wenzake, na Iam sure hawezi kulazimishwa kutoa msimamo ambao haukubaliani nao, kama akitofautiana na wanakamati wenzake wakati wa kuandika report ataeleza hivyo, itakuwa ni juu ya mwenyekiti kuamua kuyaweka mawazo ya mjumbe Zitto au laa! (after all hata mahakamani majaji wanaandika dissenting opinions!) na at the end of the day kwa sababu Zitto ni upinzani I STRONGLY BELIEVE outcome ya hii report wananchi tutaambiwa (maana JK anajua wazi, asipotwambia Zitto na mzee Mapesa watatwambia) na sisi wananchi ndo tutachambua pumba na mchele! Zitto atatwambia recommendations zake zilikuwa zipi na sisi tutaamua, after all si aliweka msimamo wake wa Buzwagi, na ni sisi wananchi ambao tulikwenda nyuma yake na kumsupport?

Hivyo basi, mimi nina imani kabisa huu ueuzi ni safi na wa maslahi kwetu sisi wananchi! Maana naamini huyu bwana Zitto atatuwekea hata hii report hapa JF kama ikiwezekana, maana yeye habanwi na EL NA JK na akiona ni report inabanwa na inaweza kuwa political capital, Iam sure Zitto hatasubiri kushauliwa kuiweka hadharani maana as any politican anataka catalyst ya kumpeleka mbele kisiasa, na hii report ya madini is one of them.

Swala kwamba Kamati haina nguvu, bado naamini ni hoja ya msingi lakini wajumbe (hata kama sio wote) watatwambia kama walipewa ushirikiano na habari walizokuwa wanazihitaji kukamilisha uchunguzi wao, na kama walinyimwa, ni sisi wananchi tutakao amua!

So all in all, I think Zitto should be proud to be in this Kamati na after all, yeye kama mpinzani anawakilisha mtizamo mwingine wa shillingi. Chadema wanaweza kuwa na wasi wasi, lakini mi nawashauri wakubaliane walione hili kama swala la kitaifa na wajue kwamba Zitto hata kama ni mwanachadema anawakilisha mawazo ya waliompigia kura na wale walioupigia kura upinzani!

So far naamini Zitto atakuwa na mchango mkubwa sana katika hii Kamati na sisi wananchi tutajua what transpired as long as he is in! Hata kama atajiuzuru in the process, atatwambia kwa nini alijiuzuru an we wananchi we shall play our role as a responsible JURY!!

All the best Hon. Zitto!
 
Si chochote si lolote, chadema itaendelea kuwa imara. Naamini wajumbe wa mkutano wa chadema wataruhusu Zitto kuendelea na kamati ya uchunguzi wa mikataba. Na pia na hakika zitto atakifanya kile alichokisema kuwa "amejiandaa vema kutekeleza majukumu yake kwenye kamati kwa niaba ya chama chake na waTanzania", Huu ni wakati muafaka kwa chama chake kumuunga mkono. Kitendo cha kujitoa kitaipa nafasi serikali kutoka kifua mbele na kuueleza umma kuwa mikataba ni safi. Nivema akawa kwenye kamati ili apate nafasi kuichungulia mikataba na kuona uozo ili aje atufahamishe watanzania kupitia hapa JF. Hata kama mapendekezo ya kamati hayatachukuliwa hatua basi sisi tutaendelea kumkoma nyani....
 
Hivi chadema wamerogwa???? Mbona Mnaanza ubishi wa simba na yanga?@^$#$%#.

Naanza kupata wasiwasi kuwa Chadema wanaogopa kuumbuka!! Kwamba wasiwasi wao Sio kuwa kamati haitafanya kazi vizuri, bali ikifanya kazi yake vizuri itapelekea umma wa watanzania kujua ukweli kuwa maswala ya madini si tatizo la kitaifa kama chama hicho kinavyojaribu kuwalisha wananchi. Kina mzee slaa kila wakiangalia ni kuwa wameshakula kingi ya watanzania wengi kwamba madini ni janga la kitaifa ambalo innji imeingizwa na serikali ya CCM, kwa hiyo kwa kujulikana ukweli waTZ watang'amua uzushi wao.

Unajua wale jamaa wanasema nini moyoni kwa ubishi wa Zitto kung'ang'ania kamati HUYU BWANA MDOGO HAJUI MADHIRA YATAKAYOTUPATA CHADEMA KAMA CHAMA CHA SIASA UKWELI KUHUSU MIKATABA YA MADINI UTAKAPOKUWA WAZI KWA WA-TZ, NDIO TATIZO LA KUSHIRIKISHA WATOTO KTK SIASA!!!

Nawashauri watu wanaoweka mbele maslahi ya vyama vyao vya siasa, kuepukana na utumwa huo na badala yake walitumikie taifa.

ZITTO endelea dogo wangu, kesho unaweza usiwe chadema lakini siku zote utakuwa Mtanzania!!! MASLAHI YA TAIFA KWANZA!!!
 
Upinzani wa Tanzania bado haujakomaa kisiasa, nilishasema hili na nitarudia. Zitto kujitoa haitoathiri CHADEMA, bali itaathiri Watanzania. Zitto ni muwakilishi wa walalahoi, nasio muwakilishi wa Tundu Lissu au Mbowe. Kwenye nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida wapinzani na chama tawala kuunda tume kwa mafanikio ya nchi.

Hizi propaganda kwamba Mbowe arudi kutoka masomoni, sijui nani asema nini ni BS. Hii inaonyesha ni jinsi gani Mbowe na wenzie hawajakomaa kisiasa. This shows the weakness with in CHADEMA. Poor strategy with in CHADEMA will put CCM on map again, Hiki chama kinaonyesha hakina washauri wa kisiasa, na kinajali faida binafsi na sio faida ya Tanzania.

This is a litimus test kwa CHADEMA, and CCM is watching them kwa karibu sana.

Mwenzetu tunakuvumilia mawazo yako lakini haya unayoandika yanaonyesha ushamba wako. Lazima ujue kuwa kutofautiana mawazo ni sehemu nyeti na ya msingi katika jamii ya kidemokrasia. Wewe unawaza kutokana na athari za uzoefu wa uozo wa CCM waliolishwa wananchi wengi.

Mbowe kurudi kufanya kazi yake ni jukumu lake, na huo ndiyo unaitwa uongozi. Ulitaka JK ndiye aje kuongoza vikao vya kamati kuu ya Chadema? Usisahau pia kwamba JK alipomteua Zitto alikuwa na sababu zake za kisiasa, ndiyo maana wapo wanaosema Zitto ameingizwa mkenge ili aumbuke...Tazama muundo wa kamati yenyewe...CCM watupu (na Cheyo ni mmoja wao), isipokuwa Zitto. Haya ndiyo maslahi ya taifa?

Wako wapi wataalamu na wanasheria wa madini walio independent? Yako wapi mashirika yasiyo ya kiserikali? Wako wapi wawakilishi wa madhehebu ya dini? Mbona kamati nzima na CCM tu? Kwa nini wananchi washindwe kuona kwamba Zitto kawekwa ili kusindikiza na kupiga mhuri maamuzi ambayo huko mbele ya safari akiyapinga yatatumika kummaliza?

Hivi kuzingatia maslahi ya taifa ni kufanya kazi katika kamati yenye muundo wa kiutata eti kwa vile imeundwa na rais?

La msingi, tujpe muda tuone matokeo ya kikao cha kamati kuu ya chadema. Hii inaonyesha chama kinaendeshwa kwa vikao sio matamko ya barabarani...
 
Kidumu Chama cha Chadema!

Wanaoneana wivu nini kwa "ulaji" wa Zitto?! kwi kwi kwiiiiii

wewe ndio una wivu hapa kwa kuona chadema wakijadiliana na wala sio mambo ya ndio mzee mnayofanya huko ccm every other day.

Hii kitu ya Chadema kutofautiana imewaweka ccm kwenye spotlight maana wao huwa wanakubali tu nchi ikiuzwa nahakuna anayesubutu kupinga otherwise wakubwa wanamkolimba mara moja!
 
Ninaamini kuwa baada ya mjadala huu ambao ni funzo kwa vyama vingine Chadema itaweza kuzungumza kwa kauli moja na hivyo kuonesha kuwa tofauti ya maoni ni jambo zuri na la kiafya la chama chochote kile. Tusubiri tuone. Inashangaza wote tumesahamu kina Machunde na mama Kejo tumemshupalia Zitto.. well.. miye nawatolea uvivu hao wawili..
 
Jk anafanya uchambuzi na kisha anaamua kumteua mtu kama Zito Kabwe kuwa katika kamati muhimu kama hii.Bila shaka JK anataka kupata matokeo mazuri katika ripoti yatume kwani Zito ni makini na ameshajitokeza kama mtu anyepigania maslahi ya kitaifa.Pamoja na wajumbe wengine watafanya kazi yao kwa maslahi ya Taifa.Sasa kelele za na hamnazo za nini hapo?
 
Jk anafanya uchambuzi na kisha anaamua kumteua mtu kama Zito Kabwe kuwa katika kamati muhimu kama hii.Bila shaka JK anataka kupata matokeo mazuri katika ripoti yatume kwani Zito ni makini na ameshajitokeza kama mtu anyepigania maslahi ya kitaifa.Pamoja na wajumbe wengine watafanya kazi yao kwa maslahi ya Taifa.Sasa kelele za na hamnazo za nini hapo?

Siasa ni kama Chess, you make your move and they make their move.. tatizo ni kuwa usipoangalia utajikuta kwenye check mate na hautajua ulifika fika vipi hapo. Zitto made his Move (kwenye Buzwagi), Rais made his move (kwa kumteua Zitto).. sasa Zitto need to make their move.. one of them will find himself kwenye check mate.. siku si nyingi..
 
It is all abouit posho! Zitto hawezi kujitoa kwa sababu kuna mshiko wa vikao mengine ni zugu tu...

The best atakachofanya kuwa laghai wadanganyika ni kuja na "dissenting views report" akisahau kuwa report itakuwa ya tume yote!

Bwana mdogo Zitto janja ya nyani hiyo tumestuka! Hata hivyo kakamua hivyo viposho pia poa... kanyaga twende mwanangu..
 
It is all abouit posho! Zitto hawezi kujitoa kwa sababu kuna mshiko wa vikao mengine ni zugu tu...

The best atakachofanya kuwa laghai wadanganyika ni kuja na "dissenting views report" akisahau kuwa report itakuwa ya tume yote!

Bwana mdogo Zitto janja ya nyani hiyo tumestuka! Hata hivyo kakamua hivyo viposho pia poa... kanyaga twende mwanangu..

Tatizo hapa ni mama kijo na huyo Machunde (na sio Zitto) ambao ccm hawataki kabisaa waongelewe uhusiano wao na Karamagi na ufisadi wao kuanzia iptl hadi leo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom