CHADEMA kuzoa wasanii mastaa kugombea ubunge 2015

CHADEMA kuzoa wasanii mastaa kugombea ubunge 2015

Jembe la Chadema, linategewa kugombea ubunge Morogoro Mjini, teh teh teh.

CC; chama,

Kweli wana majembe chadema. Watakuwemo hata punda wa unga wasipoangalia.
 
Last edited by a moderator:
Hapo sasa ndio awe kiongozi wa nani??, Na ushauri wangu kuwa wasanii wasijifariji na umaarufu wao katika sanaa kwamba utawawezesha kupata ubunge hiyo ni ndoto na mtaangukia pua, Kiuhalisia Sugu ni mpiganaji na kapigana sana sasa msidhani mtasafiria nyota wa Sugu.

Ndo majembe tarajiwa wa chadema pamoja na punda wa unga
 
Sasa huu ni utani wa kisiasa, mambo yakiendelea hivi Bunge litakua zaidi ya Fiesta!!
 
Ni mapema mno! Kama ni kweli, Muda ukifika kila kitu kitajulikana. Msiogope, CHADEMA ni chaguo la kila Mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake.
Wenye sifa zifuatazo lazima waikane CHADEMA na hatuwataki
1. Wezi wote lazima waikane chadema. Maana Chadema hakuna Wezi.
2. Mafisadi wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Mafisadi.
3. Waongo wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Waongo
4. Wanafiki wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Wanafiki
Mwisho kabisa Nawaomba Lady JD, JB, Mkoloni na Afande Sele wasiwe na hofu kujiunga katika Chama Makini. Naamini wako makini ndo maana hawajakurupuka kuongelea jambo ambalo muda wake bado haujafika. Mwaka 2014/2015 kila kitu kitajulikana.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuwavuta wasanii kujiunga na chama hicho, ambapo sasa wasanii wanne wa muziki wa kizazi kipya, maarufu Bongofleva na filamu, wanatarajiwa kutangazwa kuhamia chama hicho wiki hii. Wasanii hao wanadaiwa tayari kukubali kuingia kwenye chama hicho na wanatarajiwa kutangazwa rasmi hadharani katika mkutano wa hadhara utakaofanyika jijini Dar es Salaam. Kukubali kwao kuingia katika siasa, kunatajwa kutokana na ushawishi mkubwa uliofanywa na wabunge vijana wa chama hicho, pamoja na Diwani wa CCM kutoka kata moja ya Wilaya ya Kinondoni, ili chama hicho kivune kura za vijana katika uchaguzi mkuu wa 2015. Wabunge hao wa Chadema na majimbo yao katika mabano ni Halima Mdee (Kawe); Kabwe Zitto (Kigoma Kaskazini); John Mnyika (Ubungo) na Joseph Mbilinyi, jina la kisanii Sugu (Mbeya Mjini).


Habari kutoka kwa watu wa karibu na wasanii hao pamoja na ndani ya CHADEMA, zinawataja wasanii hao kuwa ni wanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee na wa miondoko ya Hip hop, Selemani Msindi ama Afande Sele. Taarifa zinawataja wengine kuwa ni mwanamuziki Fredy Maliki maarufu Mkoloni na mwigizaji wa filamu, Jacob Steven kwa jina la kisanii JB. Inadaiwa wasanii hao lengo la kuingia katika siasa kupitia chama hicho, ni kuwania ubunge ambapo Jaydee anatajwa kutaka kugombea wilayani Musoma; Afande Sele Morogoro Mjini; Mkoloni Jimbo la Tanga na JB Jimbo la Mkoa wa Dar es Salaam. Hata hivyo gazeti hili lilipowatafuta kuzungumzia taarifa hizo wote walikana ingawa wapo waliokiri kushawishiwa kuingia kwenye chama hicho na viongozi wa CHADEMA na wananchi, ili wagombee ubunge.


Afande Sele alikana kujiunga na chama hicho na kusema hana taarifa hizo isipokuwa ni kweli ameshawahi kufuatwa na viongozi wa CHADEMA wa Mkoa wa Morogoro, wakimtaka ajiunge na chama hicho na agombee ubunge Morogoro Mjini. “Nimeshafuatwa na viongozi wa Chadema wa mkoa na kata nijiunge na chama hicho na nigombee ubunge …tena hata vijana wengi na baadhi ya wazee wamenitaka nigombee ubunge kwa kupitia CHADEMA lakini nimekataa. “Pia Sugu ni mshikaji wangu na anapokuja Morogoro, vijiwe vyake ndio vyangu naye vijana wameshamfuata wakimwambia anishawishi nigombee ubunge kupitia CHADEMA, amekuwa akiniambia vijana wananitaka lakini mimi sitaki, sijawahi kujiunga na chama chochote na naona mbunge wa sasa (Abdulaziz Aboud) anafanya kazi nzuri.


“Mimi sio mwanasiasa, lakini ni mwanaharakati kupitia muziki na mtandaoni na nimekuwa nikitoa maoni mengi na kukosoa lakini narudia si mwanasiasa na sijawahi kujiunga na chama chochote,” alisema Afande Sele. Vilevile amekanusha kushawishiwa na viongozi wa kitaifa wa CHADEMA au wabunge, ingawa amekiri kuna wabunge wa chama hicho kuwa ni marafiki zake wakiwemo Mbilinyi na Zitto. Kwa upande wa Jaydee alisema hafuati itikadi ya chama chochote cha siasa na hapendi siasa kutokana na imani kuwa siasa ni uongo na yeye hapendi uongo. Alisema hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa wala kugombea ubunge kupitia chama chochote.


Hata hivyo alipoulizwa iwapo atagombea baada ya Katiba kuruhusu mgombea binafsi, alisema kwa wakati huo atajua. Hata hivyo, Licha ya kuwaona wanasiasa ni waongo, anakiri wapo wanasiasa anawaamini kutokana na kazi zao na kumtaja miongoni mwao ni Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji. Mwanamuziki huyo alisema licha ya kuwa na marafiki wa CHADEMA na CCM kama Sugu na Profesa Jay wa CHADEMA na Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Magige na Bhanji wa CCM, hawajawahi kumshawishi kujiunga na vyama vyao. Mkoloni Akizungumzia taarifa hizo za kujiunga na Chadema, JB alikana na kusema; “mimi na siasa ni vitu tofauti, sijawahi kufuatwa na mtu wa CHADEMA na angalau kungekuwa na dalili basi uniulize, hiyo ni taarifa ya kutengenezwa na wewe ndiye uliyetengeneza hakuna aliyekupa ni udaku huo.”


Kwa upande wa Mkoloni, alisema hajawahi kufuatwa wala kushawishiwa kujiunga na chama chochote, isipokuwa ni mwanachama wa muda mrefu wa CHADEMA na amekuwa akishiriki kampeni, mikutano ya hadhara na matukio yote ya uhamasishaji ndani ya chama hicho. Alisema kuhusu kuombwa kuwania jimbo mkoani Tanga kwa tiketi ya chama hicho, alisema hajawahi kuombwa na chama hicho kufanya hivyo. “Sijawahi kuombwa nigombee jimbo, na kuhusu nia ya kugombea, ni mapema mno kuzungumzia suala hilo sasa na hata kanuni za chama changu haziruhusu labda uniulize swali hilo mwakani naweza kuwa na jibu,” alisema Mkoloni.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, alikataa kuzungumzia taarifa hizo akidai yuko barabarani na masuala yote yanayohusu chama hicho aulizwe Msemaji wa chama hicho. Hata hivyo msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alisema hana taarifa kuhusu kufanyika kwa mkutano wa chama hicho Dar es Salaam na kutaka apewe muda afuatilie taarifa hizo.

Source:HabariLeo

hapo ni hewa tupu
 
Wamo,
Judith Wambura (Lady Jay Dee) anaandaliwa jimbo moja Musoma,
Selemani Msindi (Afande Sele) anaandaliwa jimbo la Morogoro Mjini
Fredy Maliki (Mkoloni) anaandaliwa jimbo moja mkoani Tanga.
Jacob Steven (JB) anaandaliwa jimbo moja la jijini Dar es salaam.

Inasemekani ni kutokana na ushawishi wa wabunge vijana Halima Mdee, Zitto Kabwe, Joseph Mbilinyi na John Mnyika.

Chanzo Habari Leo.


HAWATUTISHI
SIE TUNA
KOMBA
VICKY KAMATA

NA TUNAWACHEZA DANCE WAZURI SANA AFRIKA MASHARIKI NA KATI



an9.jpg




pia tuna wapiga gitaa wakali dunia nzima hakuna

hata DIBLO DIBALA haoni ndani huyu hapa

15.+Nape+akichaza+vijana+jazz.jpg





hivyo hawatutishi wakitaka wawachukue hata

M2 THE P
 
Ni upuuzi kujadili upuuzi kama huu,ata mimi pia niliyesoma upuuzi huu ni mpuuzi vilevile.CDM ni chama cha siasa na si chama cha kutoa uongozi kama tuzo za KORA kwa wanamuziki.Hatuendi Bungeni kwa sababu ya umaarufu,CDM tunatakiwa tupeleke Bungeni watu wenye uwezo wa kujenga hoja ikifuatiwa na sifa ya kuwa na vision na mikakati ya kuitekeleza.
 
wamo,
judith wambura (lady jay dee) anaandaliwa jimbo moja musoma,
selemani msindi (afande sele) anaandaliwa jimbo la morogoro mjini
fredy maliki (mkoloni) anaandaliwa jimbo moja mkoani tanga.
Jacob steven (jb) anaandaliwa jimbo moja la jijini dar es salaam.

Inasemekani ni kutokana na ushawishi wa wabunge vijana halima mdee, zitto kabwe, joseph mbilinyi na john mnyika.

Chanzo habari leo.

wapewe na wasanii wanahitajika sana alianza sugu wengine watafuata ni kama india wasanii wanafanya kweli.
 
Sasa huu ni utani wa kisiasa, mambo yakiendelea hivi Bunge litakua zaidi ya Fiesta!!

Ndg kwani wasanii ambao ni mawaziri na wengine wabunge india wanafanya fiesta? Hapa ni kusimamia maslah ya taifa tu!
 
Mkoloni%281%29.jpg
Huyu nae msaidizi wa sugu anatajwa tajwa kugombea ubunge kwa tiketi ya Chadema
 
Ni mapema mno! Kamau ni kweli, Muda ukifika kila kitu kitajulikana. Msiogope, CHADEMA ni chaguo la kila Mtanzania mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake.
Wenye sifa zifuatazo lazima waikane CHADEMA na hatuwataki
1. Wezi wote lazima waikane chadema. Maana Chadema hakuna Wezi.
2. Mafisadi wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Mafisadi.
3. Waongo wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Waongo
4. Wanafiki wote lazima waikane Chadema. Maana Chadema hakuna Wanafiki
Mwisho kabisa Nawaomba Lady JD, JB, Mkoloni na Afande Sele wasiwe na hofu kujiunga katika Chama Makini. Naamini wako makini ndo maana hawajakurupuka kuongelea jambo ambalo muda wake bado haujafika. Mwaka 2014/2015 kila kitu kitajulikana.

Kugombea ni haki yao lakini hawana vigezo hao hata shule hawajamaliza wote hao tena kichefuchefu huyo afande ukimpitia karibu anatoa harufu kwakweli yani mchafu
 
Mnahangaika nini mbona huyo Sugu aliyekuwepo kule Mbeya hakuna alichokifanya, wameshamchoka 2015 anapigwa chini.
 
Namngojea the Prof Jizze a.k.a mzee wa mitulinga then tumalize na R.Mkatoliki
 
HAWATUTISHI
SIE TUNA
KOMBA
VICKY KAMATA

NA TUNAWACHEZA DANCE WAZURI SANA AFRIKA MASHARIKI NA KATI



an9.jpg




pia tuna wapiga gitaa wakali dunia nzima hakuna

hata DIBLO DIBALA haoni ndani huyu hapa

15.+Nape+akichaza+vijana+jazz.jpg





hivyo hawatutishi wakitaka wawachukue hata

M2 THE P

Ebwana Nape anatisha kuliko diblo?? Kie kie kie kie
 
Back
Top Bottom