CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuwavuta wasanii kujiunga na chama hicho, ambapo sasa wasanii wanne wa muziki wa kizazi kipya, maarufu Bongofleva na filamu, wanatarajiwa kutangazwa kuhamia chama hicho wiki hii.
Afande Sele alikana kujiunga na chama hicho na kusemao
tena hata vijana wengi na baadhi ya wazee wamenitaka nigombee ubunge kwa kupitia CHADEMA lakini nimekataa. Pia Sugu ni mshikaji wangu na anapokuja Morogoro, vijiwe vyake ndio vyangu naye vijana wameshamfuata wakimwambia anishawishi nigombee ubunge kupitia CHADEMA, amekuwa akiniambia vijana wananitaka lakini mimi sitaki, sijawahi kujiunga na chama chochote na naona mbunge wa sasa (Abdulaziz Aboud) anafanya kazi nzuri.
Vilevile amekanusha kushawishiwa na viongozi wa kitaifa wa CHADEMA au wabunge, ingawa amekiri kuna wabunge wa chama hicho kuwa ni marafiki zake wakiwemo Mbilinyi na Zitto. Kwa upande wa Jaydee alisema hafuati itikadi ya chama chochote cha siasa na hapendi siasa kutokana na imani kuwa siasa ni uongo na yeye hapendi uongo. Alisema hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa wala kugombea ubunge kupitia chama chochote.
JB alikana na kusema; mimi na siasa ni vitu tofauti, sijawahi kufuatwa na mtu wa CHADEMA na angalau kungekuwa na dalili basi uniulize, hiyo ni taarifa ya kutengenezwa na wewe ndiye uliyetengeneza hakuna aliyekupa ni udaku huo.
Kwa upande wa Mkoloni, alisema hajawahi kufuatwa wala kushawishiwa kujiunga na chama chochote, isipokuwa ni mwanachama wa muda mrefu wa CHADEMA na amekuwa akishiriki kampeni, mikutano ya hadhara na matukio yote ya uhamasishaji ndani ya chama hicho. . Sijawahi kuombwa nigombee jimbo, na kuhusu nia ya kugombea, ni mapema mno kuzungumzia suala hilo sasa na hata kanuni za chama...
Source:HabariLeo