CHADEMA & Kushindwa: The Future!

- kuhoji unaposhindwa tu kwa chama kikubwa cha siasa kama cha chadema, inaleta maswali mengi sana kuliko majibu on nia na madhumuni yao kwa taifa!

William.
malecela naona bado una stress za mamilioni uliyo yatoa uliushinde ubunge wa afrika mashariki.. Je unataka chadema kihoji hata pale haki inapotondeka? Au unataka tuandamane kuwa pongeza noooooooooo ni jukumu lao kuhakikisha haki inatendeka na si vingevyo halafu kumbuka chadema ni chama cha siasa, ukitaka kuona utumbo unaofanywa na mahakama zetu chukua hukumu ya godblless lema na ya huyo mwizi mwezeko, nikuhakikishie kati ya kesi zilizo kuwa wazi kabisa ni ya huyu fisadi mwenzako ni afadhali sumbawanga mngetuchakachua......
 
Katika nchi nyingi za kibeberu ambazo vyombo vya sheria viko chini ya serikali mara chache sana vyombo hivi vikatenda haki! Mfano ni Ivory Coast ambako mahakama kuu ilimuidhinisha Bagbo dhidi ya Wade kama rais wa nchi hiyo kinyume na matokeo halisi ya uchaguzi.

Mfano mwingine ni hapa kwetu kuhusu swala la mgombea binafsi! Pamoja na kwamba jopo la majaji wa mahakama ya rufaa ikiongozwa na Jaji mkuu A. Ramadhani kuona ukweli iliamua kutuzuga kwa kualika marafiki wa mahakama akina Prof. Kabudi ili kulisaidia jopo hilo kufanya uammuzi!

Hivyo hadi hapo mahakama zetu zitakapokuwa huru maamuzi yake mengi yatakuwa yanahojiwa na wananchi na hasa ukizingatia kuwa wananchi wengi hivi sasa wana uelewa mpana zaidi.
 
And now you can tell why Kabudi na Ramadhani wamewekwa kwenye tume! Paying back? You cant tell me Kabudi is the best of all lawyers in matters of constitution! We know why they are in!
 
Tatizo kwa Chadema ndio hilo, nimeliona na linanikera, huwezi kuendesha nchi kwa kulazimisha mambo, na kuwa na mitazamo ya kudhulumiwa kila wakati..sioni sababu ya kuandamana wakati kuna room for appeal..inafikia wakati siasa ziwekwe pembeni wa watu tu argue on facts..hii nchi ipo kama vile uchaguzi bado unaendelea wakati ulishamalizika 2010 na Rais tumeshampata..

Mimi naomba watu tufanye kazi za kujenga taifa letu..kuna mambo ya msingi mno ya kuyafanyia kazi kuliko kuandamana kila siku..inatia aibu chadema sometimes..kila siku mikutano ya kisiasa..upande wangu mimi..naona serikali yetu iwe serious nayo japo kidogo..

Hivi majuzi..tumeambiwa kuwa kule kagera kuna wahamiaji haramu kutoka Uganda zaidi ya 30,000 lakini serikali ipo kimya..hawa jamaa wanatafuna rasilimali zetu bila aibu..nenda mahospitalini..kunanuka..vitanda vimechakaa..dawa hakuna..hakuna mashine za vipimo vikubwa ..hali ni mbaya mnoo..naipenda ccm..lakini kwa staili hii ya kuendesha nchi sio kabisa..kuna ulazima gani wa kuwa na magari ya milioni 200 wakati kunayo magari mazuri tu kama rav 4 ambazo zingeweza kutumika na mawaziri..posho za safari na vikao..

Kila siku semina kwenye mahoteli makubwa makubwa..fedha zinapelekwa kwenye semina badala ya kujenga shule na kuchimba visima..mnatupeleka wapi..kwangu mimi..nabakia ccm kwakua bado sijapata mbadala wake , maana chadema are very naiive and only seeking for public liniency rather than being a real option for ccm, i believe we can make necessary changes in our party if and only if..watu kama sisi ambao hatuna majina ya mwisho kama yenu tutapewa kuleta some impact in our country..

LET US BUILD OUR BELOVED COUNTRY and not only chasing women and drinking beers!!
 
WEWE ULITUAMBIA UCHAGUZI WA EAST AFRIKA ULITAWALIWA NA RUSHWA NA KWA VILE WEWE ULIKUWA MGOMBEA MAANA YAKE KILA ATAKAYEFUNGUA KESI MATEGEMEO YETU ATASHINDA.
KUHUSU USHAHIDI NA NINI HAPO NI KUWA HATA KAMA HAUJAWASILISHWA KIUMAKINI TUNA HAKI YA KULALAMIKA.

ccm haiwezi kushinda uchaguzi wowote bila rushwa,mfano kuna picha inamwonyesha kikwete akigawa pipi kwa watoto wakati wa kampeni kwa hiyo kama rais alikuwa anaruhusiwa kufunguliwa kesi tulitegemea kwa ile picha ya pipi tu ushindi wake ulishatenguliwa.
 
Wanabodi siyo kila thread inayoanzishwa na William ni Nzuri. kwanza huwa zinatia hasira ambayo mwishoni inapelekea kupata ban nakama hamjagundua hawa magamba nia yao kubwa ni waitawale JF kwa kupunguza wachangiaji wa CDM kwani wengi wao watakuwa wamepata ban kutokana na hayo mathread yao yanayo kasirisha nafikiri ifikie wakati thread kama hizi tuzidharau na kupita tu ili zisifike mbali
 
- Kuhoji unaposhindwa tu kwa chama kikubwa cha siasa kama cha Chadema, inaleta maswali mengi sana kuliko majibu on nia na madhumuni yao kwa Taifa!

William.

Unataka wahoji nini kwenye ushindi uliowazi, unategemea chadema wangeshinda kesi yoyete kama wangekuwa wamepata ushindi wa magumashi kama ilivyo kwa CCM? Hata jamii inaridhika na ushindi wa chadema ndiyo maana hamna anayeona haja yakuhoji pale mahakama inapotupilia mabali madai ya CCM.

Hebu tuambie wewe kama mwanajamii ya kitanzania kutoka ndani ya moyo wako pasipo kumshirikisha shetani kwenye hili kuwa ni jimbo gani ambalo unaweza kutuambia chadema walishinda kwa magumashi kama CCM? Sote tunakumbuka majimbo yote haya ya chadema washindi walitangazwa kwa nguvu ya umma huku tume haitaki. halfu leo unakuja kutuambia mahakama inaweza kutengua matokeo ya wanyonge na wasiseme chochote kisa wao ni mahakama? Mahakama ni ya watanzania haohao na hao ndo asilimia kubwa wanalalamika kuonewa.

Labda ni weke wazi kuwa MAHAKAMA AMBAYO UAMUZI WAKE UNAPINGWA NA WALIO WENGI KWENYE JAMII HUSIKA, HAIWEZI KUWA YA WANAJAMII HUSIKA BALI ITAKUWA NI YA WANAKIKUNDI KIDOGO TU KINACHOWAKANDAMIZA WALIO WENGINE. UAMUZI WA MAHAKAMA YA WATU NI LAZIMA UUNGWE MKONO NA WALIO WENGI ILI HAKI IONEKANE IMETENDEKA.
 
Tatizo kwa Chadema ndio hilo, nimeliona na linanikera, huwezi kuendesha nchi kwa kulazimisha mambo, na kuwa na mitazamo ya kudhulumiwa kila wakati..sioni sababu ya kuandamana wakati kuna room for appeal..inafikia wakati siasa ziwekwe pembeni wa watu tu argue on facts..hii nchi ipo kama vile uchaguzi bado unaendelea wakati ulishamalizika 2010 na Rais tumeshampata..

Mimi naomba watu tufanye kazi za kujenga taifa letu..kuna mambo ya msingi mno ya kuyafanyia kazi kuliko kuandamana kila siku..inatia aibu chadema sometimes..kila siku mikutano ya kisiasa..upande wangu mimi..naona serikali yetu iwe serious nayo japo kidogo..

Hivi majuzi..tumeambiwa kuwa kule kagera kuna wahamiaji haramu kutoka Uganda zaidi ya 30,000 lakini serikali ipo kimya..hawa jamaa wanatafuna rasilimali zetu bila aibu..nenda mahospitalini..kunanuka..vitanda vimechakaa..dawa hakuna..hakuna mashine za vipimo vikubwa ..hali ni mbaya mnoo..naipenda ccm..lakini kwa staili hii ya kuendesha nchi sio kabisa..kuna ulazima gani wa kuwa na magari ya milioni 200 wakati kunayo magari mazuri tu kama rav 4 ambazo zingeweza kutumika na mawaziri..posho za safari na vikao..

Kila siku semina kwenye mahoteli makubwa makubwa..fedha zinapelekwa kwenye semina badala ya kujenga shule na kuchimba visima..mnatupeleka wapi..kwangu mimi..nabakia ccm kwakua bado sijapata mbadala wake , maana chadema are very naiive and only seeking for public liniency rather than being a real option for ccm, i believe we can make necessary changes in our party if and only if..watu kama sisi ambao hatuna majina ya mwisho kama yenu tutapewa kuleta some impact in our country..

LET US BUILD OUR BELOVED COUNTRY and not only chasing women and drinking beers!!

Unapoona hili la kwenye red basi ujuwe watu hawakuwapata viongozi waliowachagua bali waliuziwa mbuzi kwenye gunia, kumbe ni fisi!

Mkuu hatuwezi kuleta maendeleo pasikpo kuwa na HAKI kwanza, tafuta kote duniani nchi iliyoendelea huku ikikanyaga haki za watu wake. Watu wakipata HAKI zao, maendelao ni rahisi sana mkuu. Hebu fikiria pale unapokuwa na ma fly-over,umeme wa uhakika, gas,maji ya kumwaga,na kadharika lakini hakuna HAKI!
 
Wanabodi siyo kila thread inayoanzishwa na William ni Nzuri. kwanza huwa zinatia hasira ambayo mwishoni inapelekea kupata ban nakama hamjagundua hawa magamba nia yao kubwa ni waitawale JF kwa kupunguza wachangiaji wa CDM kwani wengi wao watakuwa wamepata ban kutokana na hayo mathread yao yanayo kasirisha nafikiri ifikie wakati thread kama hizi tuzidharau na kupita tu ili zisifike mbali

Mkuu umenena, nadhani ni kuwapotezea hawa!
 
... the most cunning balancing-act and distributive approach to administration of justice at work at its best. Eti kwa kuwa tumewaumiza pale tulipo na maslahi nayo sana kichama sasa tukawapooze tena na hukumu ghiliba kule kwingineko pembezoni.

Tena huyu Lissu ndio msimguse kabisa maana pale hakutokucha ila hili lingine lisumbufu tukaliondoe tu maana tutawashinda na mantiki ya kuwapa jimbo moja au mbili hivi lakini lazima kukatafute kupunguza nguvu za CHADEMA kwa kutumia Mahakama maana huku kwenye kupiga kura ndio hivo haiwezekani tena Dr Slaa na yule jamaa wa M4C tayari wameshaloga kila kona ya taifa hili. Jamaa hawa tuwabane humu humu mahakamani; hakuna kufanya uchaguzi mdogo hapa.

Williamu, nadhani itakua ni jambo la busara tukakuachie japo kijinafasi kupona makovu ya kinyanganyiro cha ubunge Afrika Mashariki kabla ya kubadilishiwa kazi ubalozini hapo baadaye kidogo.
 
Mkuu mbona wewe ulivyoshindwa kule EAC ulilalamika sana??

Mara ooooh watu wanakula rushwa??

Mara sijui nini!!

Tutaacha kulalamika pale tu ambapo tutakuwa na mihimili mitatu huru katika nchi hii!! Yaani Serikali, Bunge na mahakama!

BTW, najua hata wewe ulisikitika sana mahanga kushinda kwani ulienda pale ukiamini atashindwa na wewe utagombea kupitia magamba, pole mkuu naona miti yote inaendelea kuteleza.

Fahamu tu kulalama ni hulka ya mwanadamu yoyote yule hasa anapokuwa hana imani na vyombo husika, ushauri wako ni mzuri ila umejaa double standards!
 
ndugu william uliyoyasema hapo kuna baadhi nakubaliana nayo, kuna wakati kweli naonaga cdm wakishinda basi kila kitu kilienda vizuri wakishindwa wanalalamika wameonewa bt hiyo sio tu kwa cdm hata ccm pia ndio maana hata na wao wako mahakamani wanapinga baadhi ya matokeo.

Ukifuatilia kesi za ubunge mahakamani ni kwamba zile cdm wanazolalamika ni kwa kua kulikua na rushwa wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi...wakati ccm wakienda mahakamani wanalalamika kua wagombea wa cdm walitoa matusi na kuongea vitu wakati wa kampeni ambavyo havikua vya ukweli na viliwadhalilisha...Umeona tofauti hapo Mheshimiwa??

Sijawahi kusikia ccm inalalamika kua cdm imeshinda uchaguzi kwa sababu walitoa rushwa kwa wapiga kura..but ccm kila uchaguzi ndio hivyo inavolalamikiwa...kwa hiyo inajenga imani kua CCM bila rushwa haiwezi kushinda uchaguzi... na kuna baadhi ya majimbo ambayo mpaka mahakama imekubali kua rushwa ilitendeka na wabunge wa ccm wamepigwa chini.

2015 waambie viongozi wako wa ccm kua for the first time ever wasichakachue kura, hakuna rushwa..hakuna kugawa baiskeli, pikipiki, khanga, vinoti ya 10000 kwa walala hoi wala nini...pandeni jukwaani..toeni sera zenu waiteni akina mkapa, lowassa na wengineo wajinadi...msitoe rushwa kabisa acheni kura za wananchi zifanye kazi na tume ya uchaguzi ifanye kazi yake bila kuingiliwa... Kama mkishinda uchaguzi bila kufanya niliyoyataja hapo juu...nina kuhakikishia hakuna atakayeenda mahakamani..maana kama ulivyosema asiyekubali kushindwa si mshindani na wakati mwingine kushindwa ni kushinda!!!:cool2:
 
- Waheshimiwa Zitto, Januari, na Mbowe walisema maneno kama yangu, je na wao walishindwa ubunge wa EAC? I mean where is a common sense japo kidogo tu?

William.

Walichokizungumzia kina Mbowe ni wagombea wa CCM kugawa rushwa kwa wabunge wa CCM.Upo???
 
Bora ulivyowapa ukweli, Wameshushuka. Shuuuuu!. Mkishindwa mahakamani si mjipange tena kukata rufaa?. Mnalalama ili iweje?

Hakuna ukweli wowote hapo. Ukweli ni kuwa CCM imekuwa ikitumia vyombo vya dola na mahakama kwa ajili ya maslahi ya mafisadi. Mfano polisi imekosa heshima mbele ya jamii kwa sababu ya CCM Mafisadi. Mahakama nayo haina uhuru kwa sababu baadhi ya majaji ni makada CCM au wanatumiwa na CMM. Ni mahakimu na majaji wachache ambao huzingatia maadili ya kazi yao. Sasa hapo CDM watakubalije hukuma inayotolewa bila kufuata sheria?

Shame on you CCM aka Magamba..... 2015 is very close. Hamtaweza kuishinda nguvu ya umma tena.
 
- Wengi wetu tunaotaka mabadiliko ya kweli kwa taifa letu, huwa tunawachukulia Chadema seriously kama chama as the best alternative from CCM, lakini pole pole au kwa kasi sana wamekuwa wakijenga imani potofu sana among wananchi kwamba kila wanaposhindwa, either iwe uchaguzi au kesi za uchaguzi, basi haki inakuwa haikutendeka na kwamba nchi haiwezi kutawalika.

- Imean, kwenye kila ushindani kuna kushinda na kushindwa, depending on how much politics you have in you kushindwa kunaweza kuwa ni kushinda, lakini unapoanza kujenga mazingara ya kwamba ukishindwa tu haki haikutendeka na hasa kwenye siasa, unajenga a very fragile political base, ambayo Mungu jalia ukija kushika madaraka itakuja kukumiza wewe mwenyewe, maana itawaruhusu uliowashinda ku-claim your conflict theory ya kutokea kwamba haki haikutendeka!

- Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba some of us are taking you very serious, sasa huu msingi mnaoujenga wa haki kutendeka pale tu mnapokuwa mmeshinda, ni hatari sana kwa siasa za mbele kwa taifa, jaribuni kuweka taifa mbele kama sisi wengine.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM City!

Lee Mutuz chama chenu HAKIAMINIKI TENA kwa wananchi tuliowengi (Au wenye ufahamu wa nini kinachoendelea), tunashangaa hata ninyi vijana bado mnakipigia chapuo hicho chama. Ushauri wangu tumieni majina ya baba zenu (msitumie tu kwenye kupata vyeo na umaarufu ndani ya chama) kukisafisha hicho chama kurudishe imani yetu otherwise hameni njooni tusaidiane kuikomboa nchi yetu
 
Common sense is for common people, we need to think critically and not otherwise..
 
Tatizo kwa Chadema ndio hilo, nimeliona na linanikera, huwezi kuendesha nchi kwa kulazimisha mambo, na kuwa na mitazamo ya kudhulumiwa kila wakati..sioni sababu ya kuandamana wakati kuna room for appeal..inafikia wakati siasa ziwekwe pembeni wa watu tu argue on facts..hii nchi ipo kama vile uchaguzi bado unaendelea wakati ulishamalizika 2010 na Rais tumeshampata..

Mimi naomba watu tufanye kazi za kujenga taifa letu..kuna mambo ya msingi mno ya kuyafanyia kazi kuliko kuandamana kila siku..inatia aibu chadema sometimes..kila siku mikutano ya kisiasa..upande wangu mimi..naona serikali yetu iwe serious nayo japo kidogo..

Hivi majuzi..tumeambiwa kuwa kule kagera kuna wahamiaji haramu kutoka Uganda zaidi ya 30,000 lakini serikali ipo kimya..hawa jamaa wanatafuna rasilimali zetu bila aibu..nenda mahospitalini..kunanuka..vitanda vimechakaa..dawa hakuna..hakuna mashine za vipimo vikubwa ..hali ni mbaya mnoo..naipenda ccm..lakini kwa staili hii ya kuendesha nchi sio kabisa..kuna ulazima gani wa kuwa na magari ya milioni 200 wakati kunayo magari mazuri tu kama rav 4 ambazo zingeweza kutumika na mawaziri..posho za safari na vikao..

Kila siku semina kwenye mahoteli makubwa makubwa..fedha zinapelekwa kwenye semina badala ya kujenga shule na kuchimba visima..mnatupeleka wapi..kwangu mimi..nabakia ccm kwakua bado sijapata mbadala wake , maana chadema are very naiive and only seeking for public liniency rather than being a real option for ccm, i believe we can make necessary changes in our party if and only if..watu kama sisi ambao hatuna majina ya mwisho kama yenu tutapewa kuleta some impact in our country..

LET US BUILD OUR BELOVED COUNTRY and not only chasing women and drinking beers!!

Tuanze na red ya mwanzo.. unakishutumu CDM kwa kulazimisha mambo kwa kuandamana na kudai haki yao halafu unaendelea kukisema chama chako kwamba kimepoteza dira kwa kukaa kimya.. Unakiri kwamba unakipenda chama chako bt kwa style hii ya kuendesha nchi siyo kabisa..! Na unauliza kabisa chama chako kinawapeleka wapi..!

Mkuu naamini wokovu kwako uko karibu.. Hawa unaowaona huku CDM wametoka huko kwenye chama chako.. Waliyaona haya na kutahadharisha.. Mbali ya kutahadharisha walijitahidi kupambana na hayo maovu kwenye chama chako bt mwisho wa ciku walishindwa.. Maana chama chako kimeshikwa na wenye hela.. Matajiri.. Wafanyabiashara.. Mafisadi.. Walipiga makelele mwisho wakaamua kutoka na kwenda kuanzisha chama mbadala.. Nadhani unaona sasa CDM wanavyopeleka kesi za serikali ya chama chako kwa wananchi.. Na unaona jinci wananchi wanavyotoa adhabu kwa chama chako ambacho badala ya kujirekebisha.. ndio kinazidi kuwa katili.. Kama utakumbuka kauli ya Jaji Mkuu hivi karibuni.. Alisema mahakama za Tanzania haziko huru.. `Tafakari kwa kina kisha chukua maamuzi..
 
Ahahaaaaaaaa dunia bana ..wanaokandamiza wanasema si vizuri anayekandamizwawa kulalama chombo fulani kikisema hajakandamizwa.Kujiahalalishia ukandamizaji....

Ni other words kukimwona mtu anakuibia ukawa maishaihidi pia ila chombo fulani cha dola kikisema hukuibiwa basi inakuwa haki imetendeka na hutakiwi kulalama...
 
hakuna ubishi kuwa kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa uchaguzi,wizi wa kura na shahidi zipo za kutosha za kielectronic nk
naona mahakamA zetu bado ziko nyuma ktk tecknolojia ya ICT katika kuadmit electronic eevidence
jaji makini haangali sheria peke yake lazima angaliE pia teknolojia ya sasa ili kutenda haki kwa pande zote
majaji hao hao hawataki kusoma ili kuendana na mfumo mpya wa ICT. kwa wanaojua ICT KUNA MODEL LAW INAITWA UNICTRAL inasema nchi isikatae kupokea ushahidi wa kielectronic kwa kisingizio chochote kile.tanzania naona hatujaridhia hii model law ambayo kwa kiasi kikubwa nchi za Ulaya na Marekani wanafuta hii model.
Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo majaji wake bado wanaandika ushaidi kwa mkono na hata ukirekodiwa bado hawauamini,
naamini hukumu ilikuwa wazi imethibitishwa pasi mashaka kama angetumia vigezo hivo
ILA HAKUWA NA JINSI ALIAMUA KUFUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE KUFICHA AIBU YA WAZIRI
NA PIA KWA KISINGIZIO CHA KUSAVE COST.
 
Back
Top Bottom