CHADEMA & Kushindwa: The Future! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA & Kushindwa: The Future!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 3, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  - Wengi wetu tunaotaka mabadiliko ya kweli kwa taifa letu, huwa tunawachukulia Chadema seriously kama chama as the best alternative from CCM, lakini pole pole au kwa kasi sana wamekuwa wakijenga imani potofu sana among wananchi kwamba kila wanaposhindwa, either iwe uchaguzi au kesi za uchaguzi, basi haki inakuwa haikutendeka na kwamba nchi haiwezi kutawalika.

  - Imean, kwenye kila ushindani kuna kushinda na kushindwa, depending on how much politics you have in you kushindwa kunaweza kuwa ni kushinda, lakini unapoanza kujenga mazingara ya kwamba ukishindwa tu haki haikutendeka na hasa kwenye siasa, unajenga a very fragile political base, ambayo Mungu jalia ukija kushika madaraka itakuja kukumiza wewe mwenyewe, maana itawaruhusu uliowashinda ku-claim your conflict theory ya kutokea kwamba haki haikutendeka!

  - Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba some of us are taking you very serious, sasa huu msingi mnaoujenga wa haki kutendeka pale tu mnapokuwa mmeshinda, ni hatari sana kwa siasa za mbele kwa taifa, jaribuni kuweka taifa mbele kama sisi wengine.


  MUNGU AIBARIKI TANZANIA!  William @DSM City!
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hivi nyinyi bila kuiba mnaweza kushinda?
  Namnukuu Ndesambulo,"Nilishamuambia Kikwete mwaka jana CCM bila wizi wa kura hawawezi kushinda"
  Mwisho wa kunukuu....
  Hatuna imani na nyinyi CCM tena kwa kuwa ndio imekuwa tabia yenu ila mwisho wake unakaribia
   
 3. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sie MSAMIATI wetu; mahakama ni chombo cha HAKI pale maamuzi yanakuwa na faida kwetu na si vinginevyo;

  Tumeshuhudia tukitendewa haki; Singida, Biharamuro, Mbozi

  Tumeshuhudia tukinyimwa haki; Arusha Mjini, Shinyanga Mjini, Segerea
   
 4. H

  Hingi Jr Senior Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo nyinyi CDM mkishinda mmetendewa haki,mkishindwa hamkutendewa haki mtasubili sana! KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM.
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wewe Malecela tumia akili yako, najua dhamira hasa ya kuanzisha uzi huu inatokana na hukumu ya jana ya kesi ya Makongoro Mahanga. NI kweli haki haikutendeka na kama ningelikuwa mimi ni aheri CCM isingemvua ubunge Aeshi - Sumbawanga Mjini lakini ikamvua Makongoro kwa sababu kesi yake ilikuwa ipo wazi sana. Naamini ni tecknolijia tu inayotuponza kuweza kuweka ushahidi wazi zaidi kama nchi zilizoendelea.

  Back to the point, theory hiyo unayodai inakuwa postulated na CDM inaweza ikarudi haina mashiko endapo CDM ikishika madaraka itaacha kuingilia mihimili mingine ya maamuzi na kupunguza manung'uko kama ya sasa hivi yanayoendelea.

  Inapoonekana haki ipo ndipo CCM inapoipoteza na inapoonekana haipo ndipo inapopatikana!!!! Hii yote inatokana na mfumo unaoitafuna CCM wa kubebana.

  Ni mpaka pale CCM itakapooacha kuingilia mihimili mingine ya maamuzi hasa mahakama na tume ya taifa ya uchaguzi ndipo haki itaonekana kutendeka na malalamiko yatapungua kama si kukoma kabisa.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu William tatizo ni pale inapoonekana wazi haki imeporwa.Kwa mfano hata mtu ukiwa punguani huwezi kukubaliana na jaji aliyetengua ubunge wa Godbless Lema.Huo ni mfano mmoja tu.
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hata mahakama nayo haiaminiki na wananchi coz imekuwa ni ya CCM tu
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mfano mwingine ni ule wa jana wa Makongoro Mahanga. Naye alikuwepo na Makongoro ni rafiki yake amuombe hukumu aisome na aone kama haki imetendeka au alibebwa tu.

   
 9. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni kwamba nyie magamba hamwaminiki tena! hata ukimfuata mtoto mdogo ukimuuliza kama anawajua CCM atasema eeeeh si wale mafisadi? Yan kila kitu kweli ni magumashi tu, sasa hata ukiwa mkweli (hata mi siamini kama mnaweza mkawa wakweli) basi tunajua mnadanganya tu.

  Si unaona wewe hapa, umeongea angalua kitu cha maana kwa leo, ila watu hawakuamini, hata ukija na zuri kiasi gani. Wanajua wewe mnafiki tu, utawajeuka wakati wowote. yan ni kama unafuga nyoka bila kumng'oa meno ujue siku moja atakudunga meno yake tu hata kama umemzoea kiasi gani. Nyie ni nyoka mwenye meno, ukija kwetu hatukucheleweshi, tunaponda kichwa tu na hoja zako.

  Unatakiwa uyaseme haya ukiwa nje ya CCM la sivyo tunakula kichwa.

  Na wewe safari hii mmmh? soma alama za nyakati bana 2015 siyo mbali!!!!
   
 10. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mbona hakukuwa na malalamiko thidi ya ushindi wa Lyatonga Mrea @ Vunjo. Au CHADEMA walikuwa wameshinda kule, ukiona watu wamelalamika tena na tena ujue kuna jambo.

  BTW: Heshima hujengwa kwa muda mrefu sana, ila kinyume chake ni dakika sifuri, WATCH OUT DUDE!
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Ongea kwa mifano ili tujadili vitu halisi, sivyo nitakuona mfamaji tu!
   
 12. Kyaiyembe

  Kyaiyembe JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 1,569
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hata serikali ya kibaguzi ya Afrika kusini wakati inamhukumu N. M. Madiba ilikuwa imetenda haki kwa mtazamo wako. Kwasababu mahakama ilifanya kazi yake.
  Je Zombe naye unamwongeleaje?. Kuna msemo unahusu "Nyani na Ngedele" kama unaujua basi majibu unayo.
   
 13. Optic Density

  Optic Density Member

  #13
  May 3, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora ulivyowapa ukweli, Wameshushuka. Shuuuuu!. Mkishindwa mahakamani si mjipange tena kukata rufaa?. Mnalalama ili iweje?
   
 14. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Malecela, kwa hoja yako hii, naamimi sasa kuwa ukiwa CCM akili yote hupotea na ubongo unakuwa giza giza fulani hivi. Umeshindwa kugundua hata kwa kutumia common sense, ukiukwaji mkubwa sana uliotendeka kwenye kesi ya Arusha na Segerea? Tuache mambo ya ushabiki pembeni. Na bahati nzuri kwa sababu CCM sasa inachungulia kaburi, imefikia hatua ya nyie wenyewe kunyukana bila kujali kuwa vita vya panzi furaha ya Kunguru? Siri zote tunazo jinsi CCm walivyolumbana na kutofautiana kuhusu kesi ya Lema pale Arusha.

  Please come out of that box called CCM, come out and think critically as "Msomi" instead of just bringing "a layman's hypothesis". Shauri lako, utajuta muda si mrefu
   
 15. S

  STIDE JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwahiyo haki ispotendeka CDM wakae kimya kwakuwa na wao yatajawakuta baadae!!??

  Siamini kama haya yanasemwa na mtu mwenye upeo!! Tafakari upya!!
   
 16. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  magamba wanabaka uhuru wa mahakama na bunge. Tunakumbuka vyema kesi ya mch. Mtikila dhidi ya mgombea binafsi
  kila mwenye macho alijionea wazi jinsi gvt ilivyoingilia uhuru wa mahakama. Magamba hupindisha sheria ili kukidhi matakwa yao mfano ni yale maandamano ya aliyekua mwkt wa UVCC arusha - Millya . Tafadhali acha kufikiria kwa masaburi
   
 17. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Ndugu Willium

  Najua ulivyokuwa unaandika haya maoni yako ulijua fika unachokiandika SIO KITU CHA KWELI na wala hakina uhalisia wowote. Wewe haihitaji uwe na elimu ya sheria kujua kwamba Mpendazoe kaonewa na hizo chuki ni muendelezo wa kumuadhibu tangu atoke CCM. Hii kesi Mahanga alikuwa anajua nini kinaendelea tangu ile siku ushadidi ulipofungwa kusikilizwa, sasa wewe unachokuja kukisema hapa unamaanisha nini?

  wewe tu mtoto wa mteule uliposhindwa ubunge wa africa mashariki mlilalama na nape Umedhulumiwa,,, mpenda zoe akilala mika kwa uonevu dhahiri unamtetea rafiki yako Mahanga, nani ambaye hajui uhusiano wa familia yako na ya mahanga????

  Kumbuka heshima ya MAHAKAMA NDANI YA JAMII NA HATA MACHONI PA JAMII YA KIMATAIFA IMESHUKA TENA MNO,
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  May 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,642
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  - Yale yale mkuu jaribu kuwa na jipya, haki imetendeka kama haikutendeka hukumu ni mkusanyiko wa FACTS and EVIDENCE, muhimu ni kuwahi kukata rufaa kwenye Sheria sio kulalama kwenye public, hailisaidii Taifa in the future!, kwa sababu unajenga mazingara ya wananchi kutokubali kushindwa na wewe utakapokuja kushinda utaaambiwa exactly what you have planted yaani theory ya haki haikutendeka, ni waste ni paralysing ni very unproductive kwa taifa!

  - Ni muhimu sana Chadema wakaacha hiyo tabia sasa mapema sana!


  William.
   
 19. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #19
  May 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WJM,

  Mahakama zinachukuliwa kama chombo cha kutoa HAKI, lakini kumbuka kuwa mahakama zinasimamiwa na watu ambao kwa namna moja au nyingine wana uhusiano wa karibu na chama kilichopo madarakani kwa maana ya CCM. Utoaji HAKI unatakiwa uende sambamba na kuonekana wazi HAKI ikitendeka bila kujali nani ana uhusiano na nani, hadhi au nafasi ya mtu serikalini na madhara ya hukumu kwa chama kilichopo madarakani.

  Kwa upande wa kesi zilizovuta hisia za watu wengi sana hapa nchini, ni kesi ya Mahanga na Lema. Ukiziangalia vizuri hizo kesi utagundua zina walakini kutokana na ushahidi uliotolewa na bila shaka utagundua kuwa kuna tatizo katika system za mahakama zetu. Kama ulifatilia vizuri Arusha utakumbuka hakuna ushahidi wa kueleweka uliotolewa mpaka kusababisha Lema kuvuliwa ubunge, lakn kwa upande wa Mahanga ushahidi wa kutosha ukihusisha video na vithibitisho mbali mbali vilitolewa lakini hukumu ikawa tofauti.

  Bila kujali itikadi za vyama, kiukweli mahakama zetu hazipo HURU ingawa kuna baadhi ya majaji wapo HURU na wapo tayari kusimamia HAKI muda wote katika kazi zao.
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu huwezi kuniambia mtu kakamatwa na masanduku ya kura alafu mahakama imwalalishe mshindi kwa kitu ambacho hata mtoto mdogo asiyejua chochote atafanya maamuzi ya haki na yenye kuwa na maana na ikaonekana haki imetendeka!
   
Loading...