CHADEMA & Kushindwa: The Future!

Kwa hiyo nyinyi CDM mkishinda mmetendewa haki,mkishindwa hamkutendewa haki mtasubili sana! KIDUMU CHAMA TAWALA CHA CCM.

Hata mimi nimekuwa na nitaendelea kuwashangaa sana hawa vilaza wa Chadema, yani wao sijui wanataka washinde tu hata sehemu ambayo wameshindwa. Safi sana Le Mtuz kwa uzi bomba uliotulia.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
William,
1. Acha kujenga hoja zako kwa kisingizio cha kukaa nje! Sana sana unawakera watanzania maana im sure in one way or another its our taxes which sent you there!

2. Instead of that, show us achievements you have gained in those thirty years in exile!

3. If you really want to be a politician in the future, stop raising unreasonable issues here. Stop utilizing your time here, go out there do something tangible. Unless unataka uwe mbunge kupitia JF! Kwanza nini kimekotoa huko nje ulipokaa 4 30yrz?
 
- Yale yale mkuu jaribu kuwa na jipya, haki imetendeka kama haikutendeka hukumu ni mkusanyiko wa FACTS and EVIDENCE, muhimu ni kuwahi kukata rufaa kwenye Sheria sio kulalama kwenye public, hailisaidii Taifa in the future!, kwa sababu unajenga mazingara ya wananchi kutokubali kushindwa na wewe utakapokuja kushinda utaaambiwa exactly what you have planted yaani theory ya haki haikutendeka, ni waste ni paralysing ni very unproductive kwa taifa!

- Ni muhimu sana Chadema wakaacha hiyo tabia sasa mapema sana!

William.

Wewe nadhani unaichukulia sheria ni rocket science kwamba majaji na mahakimu wanafanya maamuzi ya kisayansi ambayo watu wakawaida hawapashwi kuyahoji maana hawajui theory ya maamuzi hayo.

Historia ya kuwa na vyombo vya mahakama na majaji ilianza tu kwa sababu jamii zilihitaji waamuzi katika jamii husika. Kigezo hakikuwa elimu bali ilikuwa ni busara na logic tu( kamasome mfalme seremani kwenye bible alivyoweza kuamua ile kesi ya wanawake wawili waliokuwa wanagombea mtoto baada ya mtoto mwingine kufa kwa kulaliwa na mwanamke mmojawapo).

Haki hatolewi kwa kutumia theory za kisayansi, bali inatolewa kwa kulinganisha uzito wa ushahidi na kwa manufaa ya wanajamii waliowengi. Haki haiwezi ikawa imetendeka(na hasa kwenye kesi ya madai) ikiwa sehemu kubwa ya jamii husika haitakubaliana na maamuzi yale. Haiwezekana asilimia 90 ya jamii nzima wawe kinyume na maamuzi ya jaji halafu badotuseme maamuzi ya jaji ni ya haki na yaheshimiwe ila unaweza kukaa kimya na kufuata ngazi za rufaa.

Mahakama ni kwa ajaili ya jamii na jamii inayomamlaka ya kukemea na kuiambia mahakama kuwa inachokifanya si kwa faida ya jamii hiyo ila ni kwa faida ya kikundi kidogo cha watu kwenye jamii hiyo. Haina maana kukakaa kimya eti kwa kufanya hivyo utakuwa umewaprovoke watu wengine wasiheshimu maamuzi ya mahakama! Hii si kweli maana mahakama ni ya wanajamii husika hivyo wanayomamlaka ya kusema haitendi haki kwa walio wengi hivyo ni lazima ijirekebishe lasivyo watu wataacha kwenda mahakamani na kutafuta njia zingine za kupata haki zao.

Suluhisho la haya manung'uniko ni kwa mahakama kutenda haki to the expectation of the majority of the society full stop! Sheria siyo science kwamba ni watu wachache tu ndo wenye uelewa wa theory zake, bali sheria ni kitu ambacho kila mtu anaweza akasoma na kuelewa vizuri tu na ndiyo maana kila mtu anatakiwa kuzisoma na kuzielewa sheria zinazotumika kwenye jamii yake ili asitende makosa. N si utetezi mahakamani kutenda kosa kisa hukujua sheria husika!

Nadhani umenielewa!
 
Kweli Magamba ni Magamba tu, hata uyapake rangi vipi yataendelea kuwa Magamba! Hivi wewe unadhani kama kungekuwa hakuna kubebana ungefika kote huko? Sasa unatoa wapi ujasiri wa kujitapa hapa? Unadhani angekuwa mtoto wa Mkulima japo kakaa Tz miaka 30 Chama cha Magamba kingem-shortlist? Wewe shukuru tu kuwa kubebana kwa Magamba ndio kulikufikisha hatua hiyo, ila kwakuwa HUNA SIFA HATA MOJA ndio maana Bungeni ukaangukia Pua. Yaani kwa mtazamo huu heri ungefikiria kimasaburi kuliko kigogo! Mpuuuuzi kweli wewe!

- I understand ha! ha! ha! kwamba waliogombea wote mpaka mwisho walikuwa watoto wa Viongozi wa CCM, I mean this is incredible! ha! ha!

William.
 
Kawaida mahakama kibongo bongo zipo chini ya CCM lakini hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha eti...
 
- Wengi wetu tunaotaka mabadiliko ya kweli kwa taifa letu, huwa tunawachukulia Chadema seriously kama chama as the best alternative from CCM, lakini pole pole au kwa kasi sana wamekuwa wakijenga imani potofu sana among wananchi kwamba kila wanaposhindwa, either iwe uchaguzi au kesi za uchaguzi, basi haki inakuwa haikutendeka na kwamba nchi haiwezi kutawalika.

- Imean, kwenye kila ushindani kuna kushinda na kushindwa, depending on how much politics you have in you kushindwa kunaweza kuwa ni kushinda, lakini unapoanza kujenga mazingara ya kwamba ukishindwa tu haki haikutendeka na hasa kwenye siasa, unajenga a very fragile political base, ambayo Mungu jalia ukija kushika madaraka itakuja kukumiza wewe mwenyewe, maana itawaruhusu uliowashinda ku-claim your conflict theory ya kutokea kwamba haki haikutendeka!

- Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba some of us are taking you very serious, sasa huu msingi mnaoujenga wa haki kutendeka pale tu mnapokuwa mmeshinda, ni hatari sana kwa siasa za mbele kwa taifa, jaribuni kuweka taifa mbele kama sisi wengine.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM City!

Kiongozi hii hahiiitaji kutumia akili ndefu. Politician yeyote anaishi kwa hope and fear. Na kama wewe ni Mtanzania utakuwa unajua party dominance ya ccm hapa Tanzania na kuna mifano mingi ya kugeuza ukweli ili iendelee kuwa madarakani. Itafanya mengi madudu ili kujilinda. Turudi nyuma wakati CCM inamuondoa Imrani Kombe mzee wako alikuwa madarakani au bado. Muulize vizuri chanzo cha mauaji yale. Chenge alimuua mtu kwa kumgonga (akiwa kwenye bajaji )unajua kesi yake ilikuwaje? Ditopile alipomtandika mtu risasi alifungwa miaka mingapi? Stan katabaro alipoandika kuhusu Loliondo alifanywaje? Ni kwamba CCM siku zote inajitahidi kuficha ukweli na kupindisha haki ili iendelee kuwa madarakani. Pia kumbuka hicho ndo chama tawala. Kitafanya mbinu zozote kuwahadaa watu. Usijifanye hujui. Muulize mzee wako CCM imepindisha haki na kuua watu wangapi ili iendelee kujilinda.

Kama kuna kushinda na kushindwa mbona uliposhindwa ubunge ukasema kuna rushwa imetembea? Ungekaa kimyaaa.
 
Ndugu yangu Malecala we ni ndumina kuwili tatizo unasahau haraka thn unakurupuka bila kuwaza maneno kama haya ulishawai kulalamika juu ya chama chako na wizi na ununuzi wa haki kwa kutumia pesa leo unaanzisha uzi ambao unawasafisha hao hao mafisadi walio kuibia mda si mrefu.

Kati ya watu aliosema mh Filikunjombe kwamba ni waoga na wanaojipendekeza ndani ya CCM nawe ni mmoja wao.

Wewe ni mnafiki na unajipendekeza uwe kati ya warithi ndani ya chama ambacho kwa kauli ya walio makini walishasema sio baba yao wala mama yao ila wewe CCM ndo wazazi hasa unapoona mzazi anakosa kwa kuwa ni mzazi basi yote sawa.

Kwa hili na jinsi ulivyojibu hoja ya kutia sahihi kama ungekuwa mbunge walai hufai kuwa kiongozi wa umma. Unataka ushahidi wa aina gani ndo uamini kuwa nyie ni wezi, mafisadi??????
 
William,
1. Acha kujenga hoja zako kwa kisingizio cha kukaa nje! Sana sana unawakera watanzania maana im sure in one way or another its our taxes which sent you there!

2. Instead of that, show us achievements you have gained in those thirty years in exile!

3. If you really want to be a politician in the future, stop raising unreasonable issues here. Stop utilizing your time here, go out there do something tangible. Unless unataka uwe mbunge kupitia JF! Kwanza nini kimekotoa huko nje ulipokaa 4 30yrz?

- Hakuna baharia anayepelekwa nje na hela za kodi ni simply, nonsense! ha! ha! ha! ha!

William.
 
- Waheshimiwa Zitto, Januari, na Mbowe walisema maneno kama yangu, je na wao walishindwa ubunge wa EAC? I mean where is a common sense japo kidogo tu?

William.

Mkuu hao ndio watanzania, WANAONGOZWA NA HISIA NA UPENZI SI MANTIKI KATIKA KUHOJI UKWELI WA MAMBO, pole sana! Nadhani hata Slaa hapendi watu kama hao, ni sumu katika chama.
Mungu wetu anaita!
 
- Wengi wetu tunaotaka mabadiliko ya kweli kwa taifa letu, huwa tunawachukulia Chadema seriously kama chama as the best alternative from CCM, lakini pole pole au kwa kasi sana wamekuwa wakijenga imani potofu sana among wananchi kwamba kila wanaposhindwa, either iwe uchaguzi au kesi za uchaguzi, basi haki inakuwa haikutendeka na kwamba nchi haiwezi kutawalika.

- Imean, kwenye kila ushindani kuna kushinda na kushindwa, depending on how much politics you have in you kushindwa kunaweza kuwa ni kushinda, lakini unapoanza kujenga mazingara ya kwamba ukishindwa tu haki haikutendeka na hasa kwenye siasa, unajenga a very fragile political base, ambayo Mungu jalia ukija kushika madaraka itakuja kukumiza wewe mwenyewe, maana itawaruhusu uliowashinda ku-claim your conflict theory ya kutokea kwamba haki haikutendeka!

- Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba some of us are taking you very serious, sasa huu msingi mnaoujenga wa haki kutendeka pale tu mnapokuwa mmeshinda, ni hatari sana kwa siasa za mbele kwa taifa, jaribuni kuweka taifa mbele kama sisi wengine.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM City!

William my friend, just to paint the picture for you, watu wapo wanaoichukulia CDM seriously, pia wapo wanaoiangalia the opposite or very normal.
Kwa kuwa tumekuwa na CCM kwa muda mrefu na watu walikuwa wakidhani kuwa ni the only party matokeo yake CCM wame betray matumaini na hisia za wananchi.
Sasa hivi unachokihofia ukidhani ni 'seriousness' ya watu kuwa CDM ndiyo chama mbadala, hiyo ipo kinyume sana .....hicho ni kielelezo kuwa watu wamechoshwa na CCM na propaganda zake na wapo tayari kwa negatives or positives, lakini si kusikiliza lolote toka CCM wala kukaa nao tena meza moja hata wajiapize kwa mizimu ya aina gani.
CHADEMA kama ilivyo CCM wana mapungufu yao, hilo lipo wazi, tofauti ni kuwa CCM imeshapewa nafasi na nafasi nyingine nyingi ikajipa yenyewe sasa tunataka dhaifu mwingine naye aje ajaribu mapungufu yake, then from that point tunaweza tukajumuisha mapungufu yetu na kutengeneza wayfoward.....so vumilia tu mkuu, sasa hivi hakuna suluhu ya kisiasa tunahitaji tujaribu kundi lingine la watanzania no matter wanaongelewaje au wana uwezo gani, kuliko kuchagua kuwa ving'ang'anizi
 
Wewe Wiliam ni kijana kiumri, lakini akili yako inazeeka kwa kasi kuliko Babako John. Hata yeye aliwahi ropoka kuwa ccm itatawala miaka 100 toka 1995, lakini baadae alikuja badili kauli yake na kukiri kuwa sasa ccm ni taabani. Wewe unaangalia, lakini huoni kabisa yanayotendeka utadhani uko marekani vile. A gentleman changes his mind sometimes a fool never. Chunga kijana!
 
Wewe nadhani unaichukulia sheria ni rocket science kwamba majaji na mahakimu wanafanya maamuzi ya kisayansi ambayo watu wakawaida hawapashwi kuyahoji maana hawajui theory ya maamuzi hayo.

Historia ya kuwa na vyombo vya mahakama na majaji ilianza tu kwa sababu jamii zilihitaji waamuzi katika jamii husika. Kigezo hakikuwa elimu bali ilikuwa ni busara na logic tu( kamasome mfalme seremani kwenye bible alivyoweza kuamua ile kesi ya wanawake wawili waliokuwa wanagombea mtoto baada ya mtoto mwingine kufa kwa kulaliwa na mwanamke mmojawapo).

Haki hatolewi kwa kutumia theory za kisayansi, bali inatolewa kwa kulinganisha uzito wa ushahidi na kwa manufaa ya wanajamii waliowengi. Haki haiwezi ikawa imetendeka(na hasa kwenye kesi ya madai) ikiwa sehemu kubwa ya jamii husika haitakubaliana na maamuzi yale. Haiwezekana asilimia 90 ya jamii nzima wawe kinyume na maamuzi ya jaji halafu badotuseme maamuzi ya jaji ni ya haki na yaheshimiwe ila unaweza kukaa kimya na kufuata ngazi za rufaa.

Mahakama ni kwa ajaili ya jamii na jamii inayomamlaka ya kukemea na kuiambia mahakama kuwa inachokifanya si kwa faida ya jamii hiyo ila ni kwa faida ya kikundi kidogo cha watu kwenye jamii hiyo. Haina maana kukakaa kimya eti kwa kufanya hivyo utakuwa umewaprovoke watu wengine wasiheshimu maamuzi ya mahakama! Hii si kweli maana mahakama ni ya wanajamii husika hivyo wanayomamlaka ya kusema haitendi haki kwa walio wengi hivyo ni lazima ijirekebishe lasivyo watu wataacha kwenda mahakamani na kutafuta njia zingine za kupata haki zao.

Suluhisho la haya manung'uniko ni kwa mahakama kutenda haki to the expectation of the majority of the society full stop! Sheria siyo science kwamba ni watu wachache tu ndo wenye uelewa wa theory zake, bali sheria ni kitu ambacho kila mtu anaweza akasoma na kuelewa vizuri tu na ndiyo maana kila mtu anatakiwa kuzisoma na kuzielewa sheria zinazotumika kwenye jamii yake ili asitende makosa. N si utetezi mahakamani kutenda kosa kisa hukujua sheria husika!

Nadhani umenielewa!

- Kuhoji unaposhindwa tu kwa chama kikubwa cha siasa kama cha Chadema, inaleta maswali mengi sana kuliko majibu on nia na madhumuni yao kwa Taifa!

William.
 
Wewe Wiliam ni kijana kiumri, lakini akili yako inazeeka kwa kasi kuliko Babako John. Hata yeye aliwahi ropoka kuwa ccm itatawala miaka 100 toka 1995, lakini baadae alikuja badili kauli yake na kukiri kuwa sasa ccm ni taabani. Wewe unaangalia, lakini huoni kabisa yanayotendeka utadhani uko marekani vile. A gentleman changes his mind sometimes a fool never. Chunga kijana!

- Ukishaanza na baba tu, maana yake huna hoja nakupotezea!, kamsome Mwanakijiji kwanza uone kama huwa ana hoja za baba wa members wengine, uko shallow sana bro sio siri1 ha! ha! ha! ha!

William.
 
Tunamuiga baba yako aliyelalamika:

"Mimi CCM inanitumia kama tingatinga. Likishamaliza kutengeneza barabara aliruhusiwa kupita katika barabara hiyo kwa madai kuwa litaibomoa".

Jiulize kwa nini mzazi wako (mkongwe wa siasa) alilalamika, ndipo utarudi kukikosoa CHADEMA.
 
- Hakuna baharia anayepelekwa nje na hela za kodi ni simply, nonsense! ha! ha! ha! ha!

William.

You really like 'non sense' enh? Does it mean ulizaliwa baharia wewe? Hukusoma? Hukutibiwa tanzania wewe? Huko ulipokwenda ulianza tuu? Baba yako hakukusurpport enh? You cant run away from that! Trying to do that is nonsense as well! And don be evasive in your response, substance matters!
 
hukumu ni mkusanyiko wa FACTS and EVIDENCE, muhimu ni kuwahi kukata rufaa kwenye Sheria sio kulalama kwenye public, hailisaidii Taifa in the future!
We are the public and very much proud of Chadema. If that hurts, sorr! I am much worried about your IQ. That's complete insane brother.
 
Willium

Ni vema tukawa wakweli kwa nafsi zetu, Mahanga yeye ndio alianza kujitangazia ushindi akiwa Arusha siku Nne kabla ya hukumu kutolewa na ushahidi upo, sasa tujiulize yeye hizo taarifa alizipata wapi???? nachojaribu kusema hapa ni kwamba kwenye mahakama zetu hakuna haki hususani kama umetofautiana na watawala kama Mpendazoe.. Tunatambua jamaa anaonewa kwa kitendo chake cha kuondoka CCM. hilo halina ubishi hata kiodgo

Kuhusu mafanikio yako, sidhani kama unaitendea nafsi yako haki uliingia kwenye kinganganyiro ili ushinde na sio ushindwa hii ilikuwa strategy yako tangu mwanzo.. Unaposema mafanikio wakati ulishindwa na kambi yako ilikuwa inalalama kwamba kuna wabaya wako kisiasa walitumia pesa nyingi ili ushindwe mie sikuelewi kabisa

Sikujuwa kuwa kujadiri issue na William ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Hana tofauti na magamba mengine.......... Walau alipokuwa NY alikuwa anajaribu kuwapiga vijembe magamba wenzake kama akina EL. Sasa karudi home ground naona kisha fyata mkia!!! Tatizo alidanganywa na Nape kuwa akirudi huku atapa post.......... ndani ya CCM. Tatizo hajui kuwa familia yao ilishakuwa out of favour ndani ya CCM tokae enzi za G55!! Bora ajaribu kumrithi baba jimboni!!
 
You really like 'non sense' enh? Does it mean ulizaliwa baharia wewe? Hukusoma? Hukutibiwa tanzania wewe? Huko ulipokwenda ulianza tuu? Baba yako hakukusurpport enh? You cant run away from that! Trying to do that is nonsense as well! And don be evasive in your response, substance matters!

jamaa naye eti alikuwa anataka ubunge.
 
- Wengi wetu tunaotaka mabadiliko ya kweli kwa taifa letu, huwa tunawachukulia Chadema seriously kama chama as the best alternative from CCM, lakini pole pole au kwa kasi sana wamekuwa wakijenga imani potofu sana among wananchi kwamba kila wanaposhindwa, either iwe uchaguzi au kesi za uchaguzi, basi haki inakuwa haikutendeka na kwamba nchi haiwezi kutawalika.

- Imean, kwenye kila ushindani kuna kushinda na kushindwa, depending on how much politics you have in you kushindwa kunaweza kuwa ni kushinda, lakini unapoanza kujenga mazingara ya kwamba ukishindwa tu haki haikutendeka na hasa kwenye siasa, unajenga a very fragile political base, ambayo Mungu jalia ukija kushika madaraka itakuja kukumiza wewe mwenyewe, maana itawaruhusu uliowashinda ku-claim your conflict theory ya kutokea kwamba haki haikutendeka!

- Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba some of us are taking you very serious, sasa huu msingi mnaoujenga wa haki kutendeka pale tu mnapokuwa mmeshinda, ni hatari sana kwa siasa za mbele kwa taifa, jaribuni kuweka taifa mbele kama sisi wengine.

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William @DSM City!

Kitu ambacho hatuwezi kukubaliana nacho kamwe ni ccm kutumia mahakama kuhalalisha wizi wa kura na uporaji wa haki ya kidemokrasia ya wananchi kuchagua viongozi wake. Kwamba mtu anafanya uchakachuaji wa uchaguzi, anakamatwa na masanduku ya kura, matokeo ya baadhi ya vituo yanapotezwa, baadhi ya watu wanakamatwa na karatasi feki za kupigia kura, msimamizi wa uchaguzi anashinikizwa kutangaza matokeo bila taratibu za kisheria kukamilika na baada ya kesi kufunguliwa mahakamani na ushahidi wote huo kuwasilishwa mahakamani lakini jaji anafumba macho na kushindwa kuuona ushahidi huo.

Ukizungumzia hukumu za singida, ccm walishindwa kuthibitisha udanganyifu uliofanyika na kwa bahati mbaya kwao mashahidi waliowapeleka ndio waliwaumbua mahakamani kwamba walikuwa wamefundishwa kwenda kutoa ushahidi wa uongo. Kwahiyo jaji anayetumia weledi wake vizuri asingeshindwa kuzingatia ushahidi huo wa kutengenezwa ili tu kumpotezea muda mbunge, hakuna shahidi aliyethibitisha udanganyifu zaidi ya kuwaumbua, pamoja na njama ilizofanya ccm kwa kushirikiana na mrema wa tlp.
Sumbawanga mahakama ilithibitishiwa bila shaka namna ccm walivyotoa rushwa kwa wapiga kura. Sasa kwa jaji anayetumia weledi wake vizuri asingeweza kufumba macho na kutoona ushahidi wa mabati yaliyowasilishwa mahakamani kama "kizibiti".

Mifano hiyo miwili ni dhahiri kwamba majaji walizingatia ushahidi uliotolewa mahakamani, sasa inapotokea jaji profesa juma anafumba macho kuona ushahidi dhahiri kama huo ni lazima watu watalalamika. Na kwa taarifa yako tu mgombea mtarajiwa wa segerea ni kwamba hata wananchi wasiokuwa wanachadema ambao walishihidia mahanga akikimbia na masanduku ya kura, ambao walikuwa wakifuatilia mwenendo wa kesi hii ya mahanga, wamestaajabishwa na hukumu iliyotolewa. Kama hukumu hiyo ingekuwa ya haki wananchi wengi wasingestushwa hata kidogo.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom