CHADEMA kuna tatizo kama ni kweli

CHADEMA kuna tatizo kama ni kweli

Mmawia sikutegemea andiko kama hili toka kwako mtu mwenye wealth of experience kwenye siasa za nchi hii.
Hivi hujui huyo mchome alipangishiwa nyumba na msajili mikocheni na kuzua madai ya kutoutambua uongozi wa sekretiati il8yoteuliwa na Lissu?
Yaani huoni kabisa juhudi za Shosty Nyahoza kuihujumu Chadema kwakutumia kina Mchome na Saidi na jaji wa mchongo Mwanga?
Huoni msajili anavyozuia ruzuku ya Chadema.
Kwa kazi wanayofanya viongozi walioko nje kuna pesa gani kufananisha na ruzuku ya bilioni moja ya ccm? Ni hii ya tone tone?
You are big disappointment bro.
Mkuu nia yangu ilikuwa ni kujenga wala siyo kubomoa Na kwa hili bandiko watu wengi wameni PM juu ya hili bandiko.

Naomba tuendelee kama kawaida na mapambano yetu
 
Umeanza siasa za majungu na kitoto? Yaani matatizo yenu ya ndani ya chama yajadiliwe huku jf? Halafu huyo unayetaka tuhuma zake zijadiliwe kila siku anapambania kuhakikisha hicho chama kinakufa!
Mkuu naamini wewe unanifahamu sana kwenye itikadi sahihi.
 
Kumekuwa na shutuma nyingi sana juu ya uongozi wa juu wa chama.

Shutuma za ubadhilifu wa rasilimali fedha ndani ya chama.

Huu ni ushuhuda kutoka kwa mmoja wa viongozi wa chama mkoa wa Kilimanjaro.

Tujadili wana Jf

View attachment 3624857

---------------

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mwanga, Mkoani Kilimanjaro Lembrus Mchome ametoa tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, akidai kuwa amekuwa akikusanya fedha kutoka kwa wadau, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali kwaajili ya shughuli za chama lakini fedha hizo hazijafikishwa kwenye mifuko rasmi ya chama.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mchome amedai kuwa suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema na kusababisha mvutano miongoni mwa viongozi, akimpongeza Godbless Lema kwa kile alichodai kuwa ni alisimama kidete kutaka fedha hizo ziwekwe wazi na kuwajibishwa kwa waliohusika.

"Tumekuwa na Makamu Mwenyekiti ambaye amekuwa akichukua fedha kutoka kwa wadau mbalimbali lakini zimekuwa hazifiki ndani ya chama. Ndio maana juzi kwenye Kamati Kuu wamegombana. Nimpongeze sana Godbless Lema kwani alisimama kidete kutaka fedha hizi zirudi, lakini haikuwezekana kwani Makamu Mwenyekiti alidai kuwa ameshazitumia na nyingine amenununulia vyombo vya muziki vya chama," alisema Mchome.

Mchome amebainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliowasiliana na Uongozi wa Chadema kupitia Kamati kuu iliyoketi Mkoani Kigoma walithibitisha kuwa walitoa michango kwa Heche kwaajili ya kukisaidia chama. Pia alidai Heche alisafiri hadi Afrika Kusini kwa lengo la kupokea fedha kutoka kwa wadau, akitoa rai ya wanachadema kumshinikiza Heche kujiondoa kwenye uongozi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

"Sasa niwaombe wanachama wa Chadema tushikamane kumtaka John Heche atupishe kwanza kwaajili ya uchunguzi. Chama hiki kinaamini katika misingi ya haki na kupinga ufisadi, kwa hiyo kwanini leo tumfumbie macho Heche?" alisema Mchome.

Katika hatua nyingine Mchome amemtuhumu Heche kunufaika kisiasa na hali ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kuwa gerezani, akisema amekuwa akijijenga kisiasa pamoja na kutumia mwanya huo kuweza kufanya ubadhirifu kwa


Chanzo: Michuzi TV
Mchome amemtuhumu Heche "kunufaika kisiasa na hali ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kuwa gerezani", kwahiyo Mchome anataka Heche aache kukiendesha chama kwa nafasi yake ya umakamu mwenyekiti! Chama kisimame mpaka Liss atakapotoka gerezani!
 
Mkuu Mmawia naamini unao uwezo wa kuchanganua mambo, yaani umeshindwa kujua aliyewasilisha hizo tuhuma anayo background gani?

Angalia hii post , kajamaa kalituaminisha magari yameuzwa vipuri na hayatotembea chama kikitoka kifungo haramu ,kichekesho ni kaliposema ni habari ya kuaminika kabisa je magari yalishindwa kutembea baada ya chama kufunguliwa kutoka kifungo haramu?


View: https://x.com/i/status/2038158815338664131

Hii ni project part II baada ya ile ya msajili kufeli hizi tuhuma iweje kamati kuu ikae kimya eti wanaozifahamu wawe wanachaumma waliohama baada ya kugaragazwa katika box la kura kwa haki na uwazi Yericko Nyerere na Mchome ndio wawe wanazijua tuhuma hizi halafu viongozi walioko kamati kuu wawe kimya?

Ninapinga wizi , ufisadi hivyo kama kuna mtu asiye na makando kando ya project hizi kutoka Lumumba kwa kivuli cha CHAUMMA akiziwasilisha kwa uwazi mimi sitomtetea Heche kama atakua ameiba ila kwa hawa watu wawili kulivalia njuga hili suala akili yangu wala haihangaiki nao maana najua wametumwa kivingine baada ya kufeli awamu ya kwanza.

Ni Yericko Nyerere huyu huyu jana ameshikishwa tiketi feki ya KLM akadanganywa Heche ametorokea Nairobi kwenda Ubelgiji , mtu huyu mwenye uwezo duni ameshindwa kuverify tiketi ile tu kwa namba ya ndege na hata tarehe kwamba KLM hawakua na safari kutokea route hiyo kaibeba nzima nzima kabandika mtandaoni ndio useme nimuamini?


GrdjneFX0AAnofj.jpg
 
Wanamtumia Lisu kama msukule kupiga hela.

Wanamuita Mandela wao wapo makwao wanachoma kitimoto tu.

Sad.
Heche ndio alimpeleka Lissu gerezani?

Heche ndio anayezuia hata wageni kuja kumuona Lissu gerezani[ haya malalamiko aliyatoa Lissu wazi mahakamani]

Heche ndio anayehairisha kesi bila sababu za msingi kwa siku 139?

Heche ndio anayewaambia maaskari wanaolinda gereza kusikiliza maongezi ya Lissu na mawakili wake kinyume na taratibu?

Heche ndio aliyetengeneza mashahidi wa siri kwa lengo la kuchelewesha kesi ?
 
CHADEMA hapati ruzuku hata 100.

Sasa hiyo ubadhirifu ni wa nini??

Msituletee vijistori uchwara vya wapare makande kama vile ni taarifa kuuuuubwa sana.
Kwa hiyo ubadhirifu ni kwenye ruzuku peke yake? Ni vigumu sana kufanya ubadhirifu kwenye ruzuku maana matumizi yake yanakaguliwa na CAG. Ndio maana juhudi za wakina Lijualikali kuichafua CDM zilikwama baada ya kupata hati safi. Ubadhirifu ni rahisi zaidi kwenye michango isiyo rasmi kama ya Tone Tone, ya wadau mmoja mmoja n.k. Ndio maana Chadema walipaswa kuwa makini kwenye masuala ya pesa kwa sababu wabaya wao wanatafuta upenyo wa kuwaumiza. Waliahidi kuwa watakuwa wanatoa hesabu za mapato na matumizi yao lakini hawafanyi hivyo. Wangefanya hivyo haya yote yasingejitokeza.

Amandla...
 
Kwanini amuite Mandela wakati sio.
Maswali yangu umeyaona au hujayaona?

Kwani Sunday Manara alivyoitwa Computer miaka ile alikua Computer kweli?

Mimi sijawahi kumtaja Lissu kama Mandela , amtajwa vile kama mfanano wa Mandela kushikiliwa gerezani na makaburu kwa tuhuma feki walizoshindwa kuzithibitisha ili wamtie hatiani kama ambavyo Lissu anashikiliwa kwa tuhuma feki ambazo jamhuri kila siku wanapiga sarakasi na mahairisho yao yasiyo na tija, jibu maswali ya msingi acha gimmicks hizo .
Muda huo huo anakusanya michango kwa ajili ya Mandela.
Nani kakusanya michango?

Weka hapa kiasi alichokusanya tukione .
 
Wewe unatumika kuhujumu chadema Kwa kujua au kutokujua

Huyo mchome unajua historia yake ???
Hata saa mbovu inapatia saa mara mbili kwa siku. Badala ya kujikita kwenye kumshambulia, jibuni hoja zake. Kwa kufanya hivyo ndio mtaonyesha nia yake ovu. Kukwepa kujibu shutma ni dalili kuwa kuna kitu kinafichwa.

Amandla...
 
Hivi kwanini chadema linapokuja suala la honesty na transparency kwenye masuala ya kifedha mnawahi kujitetea kwa kuita watu mamluki..?

Kwanini msiweke hesabu zenu vizuri zamapato na matumizi kwa umma..?

Nyie mtaweza kulinda rasilimali za nchi kama tuu hizo hela za chama zinawatoa kamasi
 
Kwa hiyo ubadhirifu ni kwenye ruzuku peke yake? Ni vigumu sana kufanya ubadhirifu kwenye ruzuku maana matumizi yake yanakaguliwa na CAG. Ndio maana juhudi za wakina Lijualikali kuichafua CDM zilikwama baada ya kupata hati safi. Ubadhirifu ni rahisi zaidi kwenye michango isiyo rasmi kama ya Tone Tone, ya wadau mmoja mmoja n.k. Ndio maana Chadema walipaswa kuwa makini kwenye masuala ya pesa kwa sababu wabaya wao wanatafuta upenyo wa kuwaumiza. Waliahidi kuwa watakuwa wanatoa hesabu za mapato na matumizi yao lakini hawafanyi hivyo. Wangefanya hivyo haya yote yasingejitokeza.

Amandla...
Tone tone inatumwa kwenye account za chama.

Inakaguliwa na CAG.

Halafu Heche hana njaa hizo za kuiba Tone Tone.

Huu ni usenge tu.

Angekuwa nanjaa, wangekuwa wmaeshauza chama kwa mabingwa wa MAUAJI na wizi Kina Samia Abdul
 
Huyu alishafukuzwa na wana mwenyekiti mwingine, huyu ni lile kundi la G55 waliokimbilia CHAUMMA, hakuna asiyejua hilo kundi kazi yao ilikuwa nini
itakuwaje wamuondoe kwenye uenyekiti wa CDM mtu ambae wanajua ni mwanachama wa Chaumma? Tafuteni uongo mwingine.

Jibuni shutma za mwanachama wenu. Chaumma wana matatizo yao na haya ya mwanachama wa CDM hayawahusu.

Amandla...
 
Back
Top Bottom