Hawathubutu,tusubiri kuwafikisha kwenye mkono wa sheria maana wao wako madarakani na mfumo wetu jinsi ulivyo,tunashindwa kuwawajibisha kama inavyotakiwa.Ndo maana unaona kesi za mahakamani zinamalizwa kisiasa,na ndiyo maana rais wa nchi anathubutu kuja na kusema hakukuwepo na rushwa kwenye issue ya radar.Ndo maana hata aliyekuwa mwanasheria mkuu alisema pesa za rushwa I million dollars ni vijisenti kama ukilinganisha na zile ambazo wenzake wanazo.Na huo ndo ukweli kwasababu keshasafishwa na mkuu wa nchi,pengine mkuu huyo akiogopa asije mwaga mboga.Ufisadi unalindwa na ofisi ya juu kabisa nchini.Hayo mengine yote ni mazingaombwe tu,hakuna aliyewajibika na hakuna atakayewajibishwa kama wataendelea kuwepo madarakani.
Kweli mkuu.
- Ndo sababu Nape anazunguuka sana kukitakasa chama
-Sijajuwa mpaka sasa zambia, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda ni sample tu kama vyama vilivyo pigania uhuru nakuupata bado viko madarakani - Kwa nini? mi sijui na ukiona mwenzio ananyolewa wee mwagia maji kichwa chako ujuwe kinafuatia
-Kule misri, saudi arabia hata iliyo kuwa ussr inatupa historia nzuri sana ya kwamba ccm watabakia wakitawala mpaka siku ya kiama kwa maono yako. Mim nimetia miwani ya mbao naona break even point inapita, point of distortion wameikamilisha wenyewe ccm kwa kutuingizia sum ya kubaguana kilicho baki ni breaking poin only.
-Hata kule walikoanzisha utawala wa vyama vingi hakuna anayedumu, siamini huyu ccm na matatizo yote haya atadumu vipi.
Ukiona wazee wanalalamika ujuwe hali si shwali, na unapokuwa madarakani we iba unavoweza, lakini wee siku ukishushwa ni kama gbagbo, charles teror, nk Kwani unadhan hata wakoloni wako uk walipenda kuondoka ah haya bwana.
Cdm wametangaza nia ya kumshitaki Nape rasmi, sasa tunasubili na wao ccm watangaze nia na kuitekeleza, kama sisi huku wapinzani hatujawagawana wanachama wa ccm kwa, hasira watakihama chama wakisikia, wakatajwa majina na kuambiwa shida mnazopata ni kwasabab ya hawa jamma na kufahamu hayo mapesa yalivoibiwa na kufichwa huko wakati tunaambiwa serikali haina fedha.
cdm, nccr na cuf wanangoja kwa hamu kugawana wanachama hata kama kesi mtajishindia lakin mioyo ya watanzania itakuwa imeujuwa ukweli na kufanya maamuzi sahihi.