Chadema kumfikisha mahakamani Nape Nnauye

CCM Wana tabia ya kuropoka bila ya ushahidi sasa yanawatokea puani kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Professor Safari kapata deal nyingine. Chama cha mabwepande kimezeeka akili hakitaki kuachia vijana.
 
Ni fursa adimu kwa Nape kuja na ushahidi wa tuhuma nzito.Sidhani kama ataomba radhi kwakuwa alikuwa anasubiri opportunity kama hii amwage mchele wote.

Usiombe radhi Nape tukutane mahakamani utubwage na ushahidi wako mzito.
 
Hivi huyu nape anapojitokeza na kuropoka mambo kama haya huwa anashauriana na viongozi wenzake ama anajitokea tu, kama anashauriana na viongozi wenzake basi ccm hekima na busara hakuna
 
Way to go, so we can get to the bottom of the matter.

Kauli zinaumba! uongo usipokanushwa au kumalizimisha mnenaji athibitishe kauli zake kunaweza kuwafanya wananchi waamini ngonjera hizo.
 
Hakika hii itakuwa fundisho tosha kwa Viongozi wa Magamba kuacha kuropoka hovyo hovyo na kwa DHAIFU kukaa kimya inadhihirisha moja kwa moja Vuvuzela la Magamba lilitoa hisia zake mwenyewe na kuziita ni za chama. Viva Chadema Viva!


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
[h=2][/h] Jumatatu, Agosti 27, 2012 06:35 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

*Ni baada ya kusema CHADEMA inafadhiliwa mabilioni
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kitamburuza mahakamani, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema Nape atafikishwa mahakamani baada ya kukituhumu chama hicho kuwa, kinapokea mabilioni ya fedha za misaada kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi.

“Agosti 12, mwaka huu, Nape alisema sisi CHADEMA tunapokea misaada ya fedha kutoka kwa wafadhili walioko nje ya nchi.

“Kutokana na kauli yake hiyo ambayo ilitangazwa na vyombo mbalimbali vya habari, tunaamini Nape ana ushahidi wa kutosha juu ya hilo.

“Kwa hali hiyo, bodi ya udhamini ya Chadema, imetutaka kufanya kikao na kutoa maagizo kwa wanasheria wetu kuanza mchakato wa kumshtaki Nape.

“Katika kutekeleza jambo hili, Agosti 24, wanasheria wetu wamemwandikia barua Nape na kumtaka kuomba radhi ndani ya siku 7, kwa uzito ule ule kupitia vyombo vya habari sambamba na kulipa fidia ya Sh bilioni 3 kutokana na kusema uongo.

“Kauli yake hii ya propaganda chafu za kuikashifu na kuifitisha CHADEMA kwa umma wa Watanzania, ikiwamo kuzusha kuwa upo uwezekano wa chama chetu kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani, tutataka athibitishe.

“Eti Nape, alisema CHADEMA inawalaghai wananchi, sisi tuna viongozi wasio waaminifu na kwamba tuko tayari kuuza nchi kwa uroho wa madaraka, sisi tunasema kamwe hili hatuwezi kumvumilia kwa uongo wake huu.

“Kipaumbele cha CHADEMA katika suala hili ni kuombwa radhi ingawa pia kiwango cha fidia ya fedha tunachokitaka kitakuwa ni fundisho kuwa uzushi na uongo unaolenga kuchafua watu bila sababu za msingi,” alisema Mnyika.

Mkurugenzi huyo wa Habari, alisema kuwa, baada ya kutolewa kauli hiyo na Msemaji huyo wa CCM, alimtaka Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, kuwaeleza Watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake lakini hakufanya hivyo.

“Ukimya wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, unamaanisha kwamba, Nape hakutumwa na chama chake kutoa matamshi aliyoyatoa bali alifanya hivyo kwa matakwa yake.

“Kwa maana hiyo, Chadema inachukua fursa hii kuutaarifu umma, kwamba Nape asipotekeleza maagizo hayo ndani ya siku saba kuanzia tarehe hiyo aliyopokea barua, hatua zingine ya kumfikisha mahakamani zitaanza,” alisema Mnyika.

Pamoja na kudhamiria kuchukua hatua za kisheria, alisema CHADEMA inaendelea kusisitiza kwamba, ni chama imara, kitaleta uongozi bora, kina sera imara na hakuna sababu ya kukihofia.

Nape alipotakiwa kuzungumzia kauli hizo za CHADEMA, alisema atazitolea ufafanuzi leo.

“Ndugu yangu naomba uniache, hayo madai ya CHADEMA nitayatolea ufafanuzi mzuri kesho (leo), katika mkutano ambao nitafanya na waandishi wa habari,” alisema Nape kwa kifupi.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
mbona mnyika alibanwa na mwigulu akashindwa kuongea
Mwigulu ambane Mnyika!!! Mwigulu piga ua hajui kuwabana watu wanaojua vitu, atawabana mambumbumbu wanyiramba na wanyaturu wenzake. We kila siku mfumuko wa bei unaongezeka halafu anajigamba kwamba ni mchumi daraja la kwanza huyo mtu hayupo makini kabisa ndiyo maana ili aweze kufanikisha ushindi wa chama chake lazima ulaghai utumike kama ilivyofanyika Igunga sasa nafikili kilichotokea unakijua. Mwigulu hayupo makini anataka cheap popularity ndiyo maana anafanya siasa za maji taka.
 
Huyu hapa

223330_213225672032187_3304863_n.jpg
 
hakuna kesi hapa! Nijuavyo mimi hakuna hela ambayo nchi au chama cha chochote kile au NGO itapewa bila mkataba au makubaliano fulani. Sasa Mnyika unamshitaki Nape kwakua hamkua na mkataba au makubaliano yoyote na wale wajerumani?
 
Hata ndani ya ccm wapo wengi wanaochukizwa na mwenendo wa Nape, makamanda fanyeni kweli hili vuvuzela litupwe cell maana mpira aliokuwa anaushabikia umeisha.Hana adabu kwa wazee wala vijana wenzio kisa analindwa na mkuu!
 
ivi mnyika walimalizanaje na mwigulu,alimlipa fidia au alimwomba radhi.
Walimalizana kama ifuatavyo 'ulikua ni uzushi na uongo wa ndugai ndio maana hakuweza kumpa mnyika badala yake akapeleka suala kamati ya maadili.

2.Bunge limemalizika bila ya kamati ya maadili kutoa adhabu yoyote kwa mnyika, ingekuwa ana makosa wangewahi kumpa adhabu.

3. mnyika hajawahi kusema uongo wowote bungeni.

4. hivyo ccm wasijifiche kwenye kivuli hicho, mzushi nape aombe radhi na kulipa fidia kwa uongo wake.
 
Nape kwenye hili utabaki peke yako....umeingia choo cha kike. Nape kwenye hili naweza kukufananisha na ua linaloota kwenye chupa.


Hao magwanda hawana lolote,wanataka kujikosha tu,watakaa kimya had hizo siku walizoweka zikiisha.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom