Chadema kumfikisha mahakamani Nape Nnauye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema kumfikisha mahakamani Nape Nnauye

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyakatari, Aug 26, 2012.

 1. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kufuatia madai ya uzushi na uongo aliyoyatoa tarehe 12 Agosti 2012 kuwa anao ushahidi kwamba CHADEMA kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili kutoka nje.

  Izingatiwe kuwa matamshi yake yalitangazwa na vyombo vya habari vya kielekroniki ikiwemo vituo vya televisheni, radio na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 12 Agosti 2012 na katika kurasa za mbele za magazeti mbalimbali tarehe 13 Agosti 2012.

  Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA iliagiza wanasheria wamwandikie barua ya kumtaka kukiomba radhi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia njia ile ile aliyotumia kufanya propaganda chafu za kuikashifu na kuifitisha CHADEMA kwa umma wa watanzania ikiwemo kuzusha kuwa upo uwezekano wa CHADEMA kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani.

  Tayari ameshaandikiwa barua ya kisheria tarehe 24 Agosti 2012 ya kumtaka aombe radhi na kulipa fidia ya bilioni tatu kwa matamshi hayo ya uzushi na uongo yenye maana ya kuwapotosha waliyoyasikia na kuyasoma kuwa CHADEMA kinawalaghai wananchi, kina viongozi wasio waaminifu na kwamba kiko tayari kuuza nchi wa uroho wa madaraka.

  Kipaumbele cha CHADEMA katika suala hili ni kuombwa radhi hata hivyo kiwango cha fidia ya fedha kwa fedheha kilichotakiwa ni fundisho kuwa uzushi na uongo unagharimu.

  Ikumbukwe kwamba tarehe 12 Agosti 2012 nilitoa kauli ya awali baada ya mkutano Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine nilieleza kwamba tutatoa tamko la kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa kamili aliyoitoa.

  Katika kauli hiyo nilitoa mwito kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kueleza watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake; hivyo ukimya wake mpaka sasa kuhusu matamshi hayo inakifanya CHADEMA kuwa na imani yenye shaka (benefit of doubt) kwamba Nape hakutumwa na chama chake kutoa matamshi aliyoyatoa.

  CHADEMA inachukua fursa hii kuutaarifu umma kwamba asipotekeleza matakwa hayo ndani ya siku saba kuanzia tarehe hiyo aliyopokea barua hatua nyingine ya kumfikisha mahakama kuu zitaanzishwa ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi.

  Pamoja na kuchukua hatua za kisheria, CHADEMA kinaendelea kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa pamoja na mikakati mingine kutekeleza operesheni ya vuguvugu la mabadiliko nchini (M4C) na tunawashukuru wananchi kwa kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kwa hali na mali katika maeneo mbalimbali nchini.

  Imetolewa Tarehe 26 Agosti 2012 na:

  John Mnyika (Mb)

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Asante mastermind of the parliament jj mnyika
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nape kwenye hili utabaki peke yako....umeingia choo cha kike. Nape kwenye hili naweza kukufananisha na ua linaloota kwenye chupa.
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  kimenuka!
   
 5. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ataacha tu kuropoka ropoka kwake
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kumbe mkuki ni kwa nguruwe tu ee?mbona mnyika na chadema wote kila siku wanazusha,wanaongea uongo,wanawapotosha wananchi au ndio ile nyani haoni kundule?
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ivi mnyika walimalizanaje na mwigulu,alimlipa fidia au alimwomba radhi.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wangemwacha alivyo, asije jikuta na mastress kibao katika umri mdogo
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  kulikuwa hakuna haja kumpa siku zote hizo huyu dawa yake ilikuwa kumburuza mahakamani straight amezidi upuuzi katibu muenezi badala ya kueneza sera za chama chako unakurupuka kushambulia CDM kila kukicha mbona sisikii ukiisemea CCJ siku hizi inaitwa CCK hamia huko maana wenzio wanakaribia kukutimua wewe huijui ccm!!
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Maelezo aliyotoa Mnyika na vielelezo spika alilimaliza kimya kimya style alivomaliza lile la kamanda Lema na Pinda!!
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  CCM hawakunyimwa kuishitaki CHADEMA, sasa wanafundishwa walichotakiwa fanya.Pia ufahamu kwa tabia ya CCM walio tayari kuhatarisha amani kwa ushindi wa muda mfupi(wakitumia kitu hata hatari kama udini,ukabila) wasingeshindwa kuwahi mahakamani ili kukibomoa CDM ila kama wamepiga silence walihofia kupata hasara kubwa zaidi
   
 12. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kwa nini nao wasishtakiwe na hao wanaoathirika na kauli hizo?
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ivi mnyika walimalizanaje na mwigulu,alimlipa fidia au alimwomba radhi.
   
 14. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Ongea kama upo kwenye jukwaa la watu wanaofikiri na kuwaza,(great thinkers) ainishi uongo ulioongelewa na CDM taja aina ya uongo, taja aliyeutoa wapi na lini usitoe tu mambo ya jumla jumla Mnyika aliwahi kusema Mwigulu alihusika EPA akamwaga vielelezo umelisikia tena? Lema alisema Pinda alisema uongo bungeni kuhusu Machafuko ya Arusha akatoa vielelezo kimyaa! Slaa alitaja list of shame akiwepo mwenyekiti wa chama chako na rais wetu dhaifu umesikia aliyehoji?? CDM wanasema mambo na vielelezo sasa kama upo uongo unaoujua wewe weka hapa tujadili
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Safi sana Mnyika.Ni lazima ifike mahali watu wajue kuropoka hovyo kama mwendawazimu kunagharimu.
   
 16. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maskini Nnauye Jr! Hasara yote hii nani atalipa?. Na kibaya zaidi naskia ile taarifa aliitoa bila baraka za Sekretarieti ya CCM! Kwa maana hiyo ni tamko lake, si tamko la CCM!

  TUMBIRI (PhD - In Progress at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form six National Exams).
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 17. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hawa siku zote wanaongea ukweli mtupu, ndiyo maana wahusika huwa hawaendi mahakamani kwa kuwa wanafahamu fika kwamba CDM hawaongei pasi na ushahidi.
   
 18. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hamjawahi nyimwa kuwapeleka mahakamani.Basi wamewaonyesha njia
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mbona mnyika alibanwa na mwigulu akashindwa kuongea
   
 20. gulio

  gulio JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  fanyeni kweli kujihakikishia ubingwa
   
Loading...