CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

hiyo ndio "SI HASA" ambayo siku zote huitwa "SIASA" huwa hakuna ADUI ama RAFIKI wa kudumu SIASA NI UNAFIKI MTUPU
 
Kwenye Siasa Hakuna Rafiki/Adui wa Kudumu. Politics is the matter of calculation. If you calculate well then everything goes well, miscalculation leads to political suicide.
 
Nyie mmekata jina mnamfuata fuata Wa nini? Mbona NAPE alizunguka nchi nzima anadai lowassa avue Gamba Chadema kumchukua roho inawauma?
 
Hivi cha kushangaa nini hapo. yule Mbunge ni mwizi na jambazi sasa kama atakukula matapishi yake kuwapokea watu aliowaita wezi na mafisadi unashangaa nini hapo? wanaongeza idadi ya wezi kwenye chama chao. pia hamna manpower huko,siku zote hungoja makapi. tulieni vita ya ubunge huko.
 
mliaza na mungu kwa kumvua nguo lowasa na kumzalilisha mwembe yanga na mkapata umaarufu na mtamalizaia mwembeyanga kwa uonyesha unafiki wenu kwa watanzania wote,


Kama ume-surrender vile!!! Maneno yako haya yanaonyesha kile kinaitwa "Last kick of the dying horse"
 
Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu, na wala hakuna rafiki wa kudumu. Hivyo basi wanachokifanya Chadema ni Sehemu ya Siasa. Chama chochote kile kingefanya hivyo. Hata leo hii, Mbowe na Slaa wakiamua kurudisha kadi za CDM na kuchukua za CCM watapokewa kama wazalendo mashujaa kwa upande wa CCM, Lakini kwa upande wa CDM watakuwa ni wasaliti tu. Hali hii ipo katika kila chama, kwa hiyo ni ya kawaida kabisa.
 
Usishangae kesho huyo waliyemponda kweli kweli ndio wakamteua kuwa mgombea urais wao. Maana kama wamediriki kwenda kule kwa mbwembwe ni dhahiri wanayoyesema ni tofauti na matendo. Yaani ni bora ya CCM kuna vitu wanafanya, ingawa wao kazi yao ni kuponda tu, kuliko hao CDM mi nawahakikishia wapeni urais muone kama mtaona hata barabara ya changarawe ikijengwa
 
huyo mtume si wa wote we ndo unamwamini si tunamwamini Kristo nae ana yake ya kutufunza tofauti na hayo bwana asifiwe sana hallelujah

kwa hiyo kristo anakubali unafiki na uongo!? acha mihemko kisa katajwa mtume..BWANA asiwe sana!
 
lowasa ni yule yule tu fisad,akipitishwa chadema kama mgombea,nitapiga kampen ya kuikataa chadema. Mbowe acha Tamaa,this project will ruin you the reputation you have built for years
 
Mtume Mohammad (SAW) katika Quran takatifu aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.

Huzijui siasa vzr! HAKUNA ADUI WA KUDUMU WALA RAFIKI WA KUDUMU KTK SIASA!! lazima mazingira na wakati wake utumike ipasavyo!! fikiria vzr!!
 
Chili acha uongo chadema walikuwa wanaitukana CCM kupitia Lowassa je NAPE nae alivyozunguka nchi zima anamtaka avue Gamba mbona husemi? Bora chadema kuliko Nape kumsema kwanza ni baba take kiongozi mkubwa Wa nchi Na chama usipende kuupotosha umma
 
lowasa ni yule yule tu fisad,akipitishwa chadema kama mgombea,nitapiga kampen ya kuikataa chadema. Mbowe acha Tamaa,this project will ruin you the reputation you have built for years

CHADEMA need to learn how to walk the talk...
 
Kwenye Siasa Hakuna Rafiki/Adui wa Kudumu. Politics is the matter of calculation. If you calculate well then everything goes well, miscalculation leads to political suicide.
Shukran sana mkuu wengine hawalijui hilo kuwa siasa ni mahesabu, hata UKAWA wakikosea mahesabu itakula kwao na bahati huwa haiji mara mbili.
 
Mkuu mleta huu uzi naomba ifahamike kuwa anaeainisha katika Qur'an ni mungu kuja kwa mtume wake (SAW).Na haya ulioandika ni maneno ya mtume(hadiith).
 
Chadema ndo chamapekee ambalo nikimbilio LA wanyonge.CDM ni ant-virus, kilamwovu tunamkaribisha,ilakwanza lazima tutamscan, kumformat na kisha kum apdate.ilituwekitu kimoja ktk harakati
 
Chadema ndo chamapekee ambalo nikimbilio LA wanyonge.CDM ni ant-virus, kilamwovu tunamkaribisha,ilakwanza lazima tutamscan, kumformat na kisha kum apdate.ilituwekitu kimoja ktk harakati

Siasa ni kuviziana. Magamba mtakoma. Mnalalamika kwa nini watani zenu wanapikea wanachama wenu? Mlitakaje. Siasa ni kutumia kila opportunity inayokuja mnele yako kumshindwenzio. Unakumbuka alivyosema Mwandosya? Kwamba ilibidi wamtukane Warioba km mbinu ya kupata ushindi jtk bange la katiba? Vumilia tu. Hiyo ndiyo siasa Hakuna mambo ta Yesu waltume lwenye siasa. Kamanda hii mesage ni kwa hilo gamba lililoleta uzi huu.
 
Sasa hivi Watanzania tunataka mtu atakayeondoa mfumo mbovu wa ccm, awe fisadi au asiwe fisadi maana mfumo huu hata mtu awe na rekodi nzuri akishaingia kwenye ccm si mzuri tena.

Ndiyo maana unaona mtu akiwa ccm ni fisadi tu. Hata Lowasa kama anauwezo wa kuiangusha ccm tunamkaribisha upinzani ilimradi tu huu mfumo utoke kwanza tuanze upya.

Tumechoshwa na utawala wa kinafiki na kizandiki wa ccm na ndiyo maana mtu yeyote anayeweza kuitoa ccm hata kama ni Boko haram au al shababu tutamuunga mkono ilimradi tu huu utawala uende kuzimu.

Na huu ndio ukweli,cha msingi hapa ni CCM kutoka madarakani watanzania wameichoka CCM na wako tayari kutawaliwa na shetani kuliko CCM
 
Back
Top Bottom