CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

Chilli

JF-Expert Member
Jul 17, 2011
1,655
743
Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.
 
Ccm naona wanapata shida sna wanavyoona madiwani wa monduli kuhamia chadema,na bado tulieni,mleta uzi naona kajifunzia siasa ukubwani,
 
It's all business people, all about business. Bora jizi unolijua lenye hela kuliko usolijua tena fukara.
 
Nadhani ukikaa ukatulia viroba na hengiova ikaisha utaandika jambo lenye akili. Viroba vya idi bado vinakusumbua. Pata supu kwanza mkuu

Nadhani Kilichochambuliwa ni sahihi kabisa najua hata moyoni mwako hilo unalijua, ila kwa kuonesha ushabiki utakataa. Lazima chama kifike pahala kiwe na msimamo ili wapiga kura waelewe. Na cdm wasipokuwa makini 2015-2025 watapotea. Kumbuka kauli ya Mh. Zitto aliwahi kusema jamani cdm tusilaluane na kufukuzana tunadhoofisha upinzani, kwani kujenga upinzani inachukua miaka mingi mno, sasa ndicho kitatokea cdm, wewe subirini
 
Last edited by a moderator:
Mpwa tulia kwanza, Chadema tunataka kura, CCM wao wanaiba sisi tunapewa na wananchi wakiwemo wana CCM, sasa kosa ni nini??
 
.... acha kulaghai dini zetu, unamtanguliza mtume kwenye huu uchafu ulioandika? hebu tutake radhi .

Mbona hakakosea kabisa. Sema wewe ndiye unapaniki bure. Cdm ni wanafiki wakubwa. Hivi hao watu wakija then ikatokea wakanyimwa madaraka si watakimbia tena chama??? Ni bora anayejiunga kwa moyo wake lakini si mtu anayemshabikia fisadi
 
Mtakoma magamba hamjui kwenye msafara wa mamba na kenge wapo mnalo litawaganda mpaka october
 
Danstan Nicholaus Diwani wa Kamachumu na yeye kaenda CDM mkuu, Lembeli naye kafanya hivyo ndugu..Diwani wa Nata Nzega na yeye kaamua hivyo..Kangi Lugola na Dada wa bunda soon wanatika huko.So punguza povu dada angu maana Singida, Manyara na kwingineko wapo njiani...
Kigumu chama cha Mapinduzi.
 
Sasa hivi Watanzania tunataka mtu atakayeondoa mfumo mbovu wa ccm, awe fisadi au asiwe fisadi maana mfumo huu hata mtu awe na rekodi nzuri akishaingia kwenye ccm si mzuri tena.

Ndiyo maana unaona mtu akiwa ccm ni fisadi tu. Hata Lowasa kama anauwezo wa kuiangusha ccm tunamkaribisha upinzani ilimradi tu huu mfumo utoke kwanza tuanze upya.

Tumechoshwa na utawala wa kinafiki na kizandiki wa ccm na ndiyo maana mtu yeyote anayeweza kuitoa ccm hata kama ni Boko haram au al shababu tutamuunga mkono ilimradi tu huu utawala uende kuzimu.
 
Sasa hivi Watanzania tunataka mtu atakayeondoa mfumo mbovu wa ccm, awe fisadi au asiwe fisadi maana mfumo huu hata mtu awe na rekodi nzuri akishaingia kwenye ccm si mzuri tena. Ndiyo maana unaona mtu akiwa ccm ni fisadi tu. Hata Lowasa kama anauwezo wa kuiangusha ccm tunamkaribisha upinzani ilimradi tu huu mfumo utoke kwanza tuanze upya. Tumechoshwa na utawala wa kinafiki na kizandiki wa ccm na ndiyo maana mtu yeyote anayeweza kuitoa ccm hata kama ni Boko haram au al shababu tutamuunga mkono ilimradi tu huu utawala uende kuzimu.

Umeeleza vzr bosi,. Pamoja Sana hadi kieleweke
 
Wanaenda cdm ni wale tu waliokubali kuokoka na kutubu zambi zao na kuikubali katba ya cdm, kwahiyo hilo lisikushangaze ni kawaida
 
Mbona hakakosea kabisa. Sema wewe ndiye unapaniki bure. Cdm ni wanafiki wakubwa. Hivi hao watu wakija then ikatokea wakanyimwa madaraka si watakimbia tena chama??? Ni bora anayejiunga kwa moyo wake lakini si mtu anayemshabikia fisadi

Dear, umeona wapi CDM wakiwaomba wana-CCM kuhamia , madiwani 20 kahama ,25 Simiyu, Mbunge mara wanachuo , bahati nzuri leo ofisi hazijafunguliwa ungesikia Geita 40, Bagamoyo 43,Dodoma 88 tusubiri kesho mpaka saa saba mchana utalazwa hospital mpenzi
 
hakika ccm mnahaha kwani CDM mnayoisema kuwa ya ukanda,ndiyo hiyohiyo iliyotupatia rais wetu sisi huku mbeya aka sugu, acheni unafiki ninyi magamba
 
Back
Top Bottom