CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

Mkuu Kwanza nikupongeze kwa kuwasilisha na kuchanganua mawazo uliyonayo. Binafsi baada ya kuyasoma nami naomba pia niwasilishe mawazo yangu. Siku zote nguo inapochafuka inahitaji maji safi na sabuni ili iweze kufuliwa na kutakata. Nije sasa kwenye mada, kuhusu kilichotokea Monduli ambapo madiwani wa ccm wamerudisha kadi zao. Tukio hili lilitokea pale chadema walipokuwa kwenye harakati za kutokomeza ccm kaskazini. Hivyo basi, baada ya kusikiliza sera za Chadema na kujiona wao ni wachafu kama nguo zinazohitaji maji Safi na sabuni ndio maana walichukua hatua ya kufanya hivyo. Kuhusu unafiki sijaona kama Kuna unafikiri wowote maana kila mtanzania ana haki ya kuhamia chama chochote akipendacho ili mradi tu atimize haja yake ya kisiasa. Nawasilisha.

Kwanza hongera kwa kutoa hoja yako kistaarabu, hila shaka hapo BAVICHA utakuwa unategemewa sana.
Back to the topic, hawa jamaa ni jana tu walikuwa wanaitwa wezi, nyang'anyi, jambazi. Leo wanaitwa makamanda kisa tu taratibu zilizotumika kumtoa mtu wao hawajakubaliana nazo, huoni huu kama ni unafiki mkubwa. Halafu tusidanganyane, hawa jamaa hawajakubaliana na sera zozote za CHADEMA, hawa ni majeruhi wa kisiasa hawahitaji sera wanafhoangalia ni maslahi.

CHADEMA mmekuwa mstari wa mbele kupinga "umalaya" wa kisiasa, nikikumbuka kipindi cha Zitto, Kafulila na hata juzi juzi kwa Mzee Arfi, huoni kwamba kuwakupokea hawa jamaa kwa mbwembwe hivi ni kula matapishi yenu??

Edward Lowassa, mmekuwa mkimwita mwizi na fisadi, je hawa jamaa wameshawaeleza kama Bwana wao alishaacha huo wizi na ufisadi?

Unajua kinachotuchosha wengi sio nyinyinkuongeza wanachama bali ni aina ya wachama mnaowaongeza, kumbe hata "shetani" akiwa na uwezo wa kuwapeleka ikulu nyinyi mko tayari kuungana nae??
 
Jamani wana CCM Tulieni WEMBE uingie vizuri ndio mtaujua moto wa UKAWA.
Bado tunachukua majembe kuunganisha nguvu ili kuliondoa joka la kijani. Huku Wilayi Kahama leo tunampokea rasmi aliykuwa Mbunge wa jimbo la Kahama Mzee James Lembeli (JEMBE) anakuja CDM na lazima tuchukue Jimbo la Kahama Mjini ( La pili kwa Mapato kitaifa baada ya ILALA) pamoja na jimbo jipya la USHETU. Pia tumemkaribisha Dada yetu Esta Bulaya kule Bunda ili atuondolee yule sokwe Mtu pale. Karibu sana Kange Rugora tunakungoja kwa hamu na wengine wote maana mwisho wa ccm umefika maana matokeo ya Ubunge yatakuwa UKAWA = 70%, CCM= 25% na OTHERS= 5%.. Kazi Ipoooooo............................
 
Ila CCM kuwapokea wanachama waliofukuzwa kwa mbwembwe hilo halina tatizo,tunahitaji kura nyingi, kumbuka baraza la mawaziri la UKAWA lipo tayari tunasubiri liapishwe baada ya October ,hao wahamiaji ni wapiga kura tu,NA BADO!!!!!!
 
Mkuu Chilli sio kwamba hawajakuelewa, wamekuelewa vizuri sana kilicho najisi kwa CCM kwa CHADEMA ni halali kabisa.
 
Lengo Kuu ni kuingo'a CCM. The End justifies the Means, au?

That is verbal engineering. I wrote "the end does not justify the means", but you have removed the "does not" from your quotation. That is blatantly unfair. It smacks of intellectual dishonesty.

It is clear that the end does not justify the means. It means that you may not do a bad thing in order to achieve a good result. For example, we want to see CCM consigned to the dustbin of history, but we may not physically eliminate them.
 
Kamwe ni ndoto cdm kuingia ikulu. Kwa wabunge watapata. Bado hawana uongozi mathubuti. Mwenyekiti wao amejaa ukanda mno, pia wapo kimaslahi sana na waongo kweli kweli.
ki ukweli vyama vyote vimejaaa uongo, CCM CDM CUF maana hata makanisani na misikitini huko nako uwongo upo, ila itabidi tuangalie upi ni uongo nafuu.... nadhani CDM wana uwongo nafuu kuliko chama kongwe CCM..
 
Sasa imejidhihirisha wazi kwamba mbowe ni mtu wa aina gani, hana soni, hana aibu, anaangalia maslahi yake na chama chake. Haangalii maumivu ya watanzania anachotaka ni kuingia ikulu tu. Watanzania mkataeni mbowe na chadema yake na lowassa wao. Hana nia ya kuwakomboa.
 
Back
Top Bottom