CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

Sasa unataka tukusadiaje ndugu yetu?
Kwenye siasa hakuna urafiki wala uadui wa kudumu,bali maslahi ya kudumu.

Na hivyo simbaya binadamu kujirudi anapoona anayotenda hayapendezi jamii.Chadema ni chuo cha kuwarudisha waliopotea kwenye line.
 
oh yes..naweza elewa machungu yako..si wewe peke yako utakayejisikia umechagua upande mbaya wa historia.W
 
Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.

Cha ajabu mini?¿ Hata Musa alilelewa na firaun, jee kumpokea kama Mtume ni unafiki? Acha kijiba cha roho! Unafiki ni pale unaposhindwa kusherehekea wakati yule anaye kuchukuliaga mkeo kagongwa na gari kafa wee eti una huzunika na kulia her?..sherehekea kwa laga na kitimoto bro...
 
Nimepata hofu kubwa na hawa CHADEMA, kumbe wako tayari kufanya lolote, ama kushirikiana na yeyote kwa ajili ya kupata nafasi ya kutuongoza. Watu hawa ni hatari kama walivyo wenzao wa CCM. Tena hawa wanaweza kuwa hatari zaidi.
Unadhani ulianza kuongea leo kw akutumia ile sehemu ya kunya?Maccm siku zote ni km wanyama wapumbavu wapo tayari kuongea lolote kwa manufaa ya muda mfupi...sasa kaskazini wa ccm wameshuhudia mlichosema kwa upuuzi wa wale reject ktk watumwa.
 
Lowassa alianzia kanda ya ziwa kutafuta wadhamini.Ndiko ccm itaanzia kukata roho
CCM walikuwa wakichekelea wakidhani baadae watampora wafuasi wake?Km Jk alipoingia na kukuta mkapa kakausanya kodi akaanza yagawa kwa rejects ktk watumwa..sasa zikaisha,wakaanza lia kuwa wanahujumiwa.
 
Chilli;

Kwanza mimi napenda niongeze neno Sauce mbele ya jina lako ili lisomeke Chilli-sauce ile tunayotumia tunapokula chips mayai. Ulichoongea hapa hakina mashiko asilan. Usifikiri kuwa kuanza na gea ya habari za Mtume Mohamed(SAW) basi watu watakubaliana na wewe. Huo ni upuuzi.

CHADEMA hawajafanya kosa lolote katika kuwapokea wimbi la wana-CCM wanaohamia CHADEMA kwa sasa siyo Monduli tu baali nchi nzima baada ya kuona kuwa CCM imeshindwa kufuata misingi na haki kulingana na kanuni za chama katika kuteua mgombea wa Urais. Hakuna dhambi wala kuvunja taratibu na sheria kulingana na Katiba unapompokea mwanachama toka chama kingine au anapohama. Baba wa Taifa aliwahi kusema CCM SI BABA YAKE kwa hiyo swala la kuhama chama liko wazi na huru kwa yeyote na wakti wowote.

Swali dogo kwako Bwana Chillisauce. Je, umewahi kuwauliza hao Vigogo na Wazee wako wa CCM waliokata jina la Lowassa walikuwa na maana gani walipowatangazia Wana-CCM kwamba watachagua jina la mgombea ANAYEKUBALIKA NDANI NA NJE YA CCM? Walikuwa wanamdanganya nani? Yaelekea bado kuna wapuuzi ndani ya chama chenu wanaofikiri Watanzania wa sasa ni sawa na wale wa miaka ya 19 kweusi! Sahau hilo.

Lowasa ana haki ya kutafuta chama kingine chochote anachoona kina sera nzuri kama CHADEMA ili aendeleze mapambano yake akiwa nje ya CCM. Ukweli utabaki kwenye historia kuwa Edward Ngoyayi Lowasa amenyang'anywa haki yake ya kuwa mgombe ndani ya CCM kwa sababu ya mizengwe ya kijinga ya watu kutaka kuweka mtu wao asiyekubali ndani wala nje ya chama. Nani hajui kuwa Lowasa alikuwa anakubalika ndani na nje ya chama? Je, unataka kutuambia Mapombe na Mende walikuwa wanakubalika ndani na nje ya CCM kama siyo uhuni???

Naomba unisikilize kwa makini bwana Chilisauce, kwamba kuhama chama au kurudi kwenye chama siyo kosa wala dhambi.Tofautisha mtu anayefanya UHAINI au USALITI ndani ya chama kama alivofanya rafiki yako Zito Kabwe wa kutaka kupindua uongozi uliopo na kuchukua madaraka pasi kufuata taratibu za chama. Huyu havumiliki lazima atimuliwe. Hapa hakuna cha unafiki. Labda nikukumbushe kuwa haya yanafanyika hata ndani ya chama Twawala CCM.Mifano hai ni kama ya kina Mzee Nassoro Moyo sliyefukuzwa juzi pale Unguja na Mahafidhina wa CCM kwa vile tu alikuwa akitetea maslahi ya Wazanzibar. Wakamtimua.

Lakini pia kuna Vigogo wa CCM ambao wamewahi kuhamia vyama vya upinzani na bado wakarudi CCM na kupokelewa kama mashujaa na hivi juzi walikuwa ni moja ya wanaotangaza nia ya kuingia Ikulu. Kwa uchache ni Steven Masato Wassira na Makongoro Nyerere waliowahi kutimkia NCCR wakapewa Ubunge na baadaye kurudi CCM walipopewa Ubunge na Uwaziri na juzi wakaruhusiwa kuchukua fomu za kuwania kuingia Ikulu. Je, hapa nani mnafiki zaidi ya CCM?

Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu. Bado kuna msemo unaosema ALIYE UPANDE wetu ni mwenzetu. Ssa kama Lowasa na Kingunge pamoja na wafuasi wao wameamua kuahmia CHADEMA ili waendeleze mapambano nje ya CCM ni ruksa. Tatizo lako ni kwamba kufikiri kwako na uwezo wa kuchanganua mambo ni mdogo sana na shida ni kwamba nyie watu mnaoegemea sana mafundisho ya SAW kwa elimu ya Madras huwapotosha sana na kuwafanya mzidi kuwa watu wa kupiga hadithi maana mafundisho kwenye vitabu vyenu kumejaa hadithi tupu na hakuna ukweli wowote.

Pole sana.
 
huyo mtume si wa wote we ndo unamwamini si tunamwamini Kristo nae ana yake ya kutufunza tofauti na hayo bwana asifiwe sana hallelujah

Hii nchi udini hautakaa uishe. Yani huyo mchangiaji amepata like 11 kwa kuwa tu amejibu nukuu aliyoweka mwanzisha uzi akimnukuu mtume Muhammad (SAW)! Wakati hiyo ilikuwa nukuu tu wala sio main topic kwenye huu uzi!
 
Nadhani Kilichochambuliwa ni sahihi kabisa najua hata moyoni mwako hilo unalijua, ila kwa kuonesha ushabiki utakataa. Lazima chama kifike pahala kiwe na msimamo ili wapiga kura waelewe. Na cdm wasipokuwa makini 2015-2025 watapotea. Kumbuka kauli ya Mh. Zitto aliwahi kusema jamani cdm tusilaluane na kufukuzana tunadhoofisha upinzani, kwani kujenga upinzani inachukua miaka mingi mno, sasa ndicho kitatokea cdm, wewe subirini
I see hadi huruma naona umeumia sana.Chama kinachopotea ni chama ambacho kinaingiza wanachama au chama kinachopoteza wanachama?!! Kwa kweli kihoro ni shida sana duuuh....!&? Kwa kasi hii ya kuondokewa na wanachama CCM wasipokuwa waangalifu huu ndo utakuwa mwaka wao wa mwisho, hata ACT yako nayo itaenda na baba yake kaburini.
 
Kamwe ni ndoto cdm kuingia ikulu. Kwa wabunge watapata. Bado hawana uongozi mathubuti. Mwenyekiti wao amejaa ukanda mno, pia wapo kimaslahi sana na waongo kweli kweli.
thanks. maneno machache lakini yaliyobeba ujumbe mzima. hawa kadima wasifikiri watanzania ni mabwe'ge kiasi hicho. waache tukutane october.
 
Mpwa tulia kwanza, Chadema tunataka kura, CCM wao wanaiba sisi tunapewa na wananchi wakiwemo wana CCM, sasa kosa ni nini??

chadema mmefilisika tatizo la cdm ukabila umewajaa wabunge wengi wa viti maalumu ni chaga sasa tutwaamini vipi tukiwapa nchi si mtahamisha ikulu iende moshi au Arusha nyie

ndigu watanzania epukaneni na chama cha ukoo hicho
 
Kamwe ni ndoto cdm kuingia ikulu. Kwa wabunge watapata. Bado hawana uongozi mathubuti. Mwenyekiti wao amejaa ukanda mno, pia wapo kimaslahi sana na waongo kweli kweli.

Kwa taarifa yako mojawapo ya vitu alivyo angusgwa navyo Lowasa ni siasa za Ukanda . Riz alisema rais hawezi kutoka Kaskazini je ile ni Ukanda na siasa ndani ya CCM au hata hujui siasa za Ubaguzi zilvyo jaa CCM ?
 
Panga pangua ccm wameshikwa pabaya mtauliza maswali meeengi ya ili tu kuwachangaya wananchi suluhisho kaeni naye mpate suluhisho ama sivyo itakula kwenu.
Kwa hiyo Lowassa siyo fisadi tena ni mtu makini anayeuchukia ufisadi anataka kuwakomboa Watazanzia?
 
Kama mnasema mnataka kubadili mfumo wa CCM na wakati huo huo mnawapokea watu waliokuwa sehemu ya mfumo huo kandamizi. Mnadhani mna lipi jipya la kuwaambia watanzania?
Mchuzi ule ule kwenye bakuli jipya.

Haihitajiki PhD kujua hili,kama 80% percent ya watanzania walikuwa kwenye mfumo mbovu wa CCM kwa kushiriki kupigiwa na kupigia kura ili kuusimika madarakani,na kuutoa pia itahitajika upate percentage ya kutosha ili kuwatoa madarakani.
Kwa hiyo unaupata wapi kama siyo hao hao baada ya kuona makosa yao wamebadilika.

Hivi hufuatilii nchi za wenzetu, kama Republican America wakati wa George Bush walikuwa madarakani baadae Democratic kupitia Obama wakawatoa,unamaanisha walizaliwa wengine kuja kupiga kura? ni RAIA wale wale,kwa sababu hakuna adui wa kufumu wala rafiki wa kudumu kutaka Siasa. Unataka kutuambia once CCM forever CCM? Your lost buddy! wote waliokuws upinzani wengi once walikuwa CCM, ni sababu moja ama nyingine iliyosababisha wahame, na hawa wa umepata sababu ya kuhama,kwa hiyo unataka kije kizazi kingine ndiyo Wewe wapinzani? you have lost it
 
Sisi tunaanza na MUNGU na tunamaliza na MUNGU, mtu akiwa CCM lazima awe mchafu na lazima tumseme sana ili atoke jalalani, akishatoka jalalani na kujisafisha tunamkalibisha sebuleni kama mwana mpotevu aliyerudi kundini,

Madiwani wa monduli wamegundua CCM hakuna haki ccm hakuna demokrasia na sio hao tu, hata Nape akigundua ukweli na anataka kuwa mwadilifu milango ipo wazi
 
Mtume Mohammad (SAW) katika moja ya hadithi zake aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

Tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka CCM Monduli.

Madiwani hawa wametoka CCM kufuatia kukatwa jina kwa Waziri mkuu 'mstaafu' Edward Ngoyai Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia CCM.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati Zitto Kabwe akiondoka/ akiondolewa CHADEMA tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani Edward Ngoyai Lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa CHADEMA. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa CHADEMA wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama CHADEMA? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa Lowassa walikuwa wachafu walipokuwa CCM lakini wakiwa CHADEMA ni wasafi? Hivi mtu akija CHADEMA anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita CUF kila jina baya mara CCM B, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda UKAWA. Mlimfukuza Kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae UKAWA huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na ACT ili tu mtimize malengo yenu.

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.

wewe jamaa naona unamatatizo, kinachofanya watu waibe ni mfumo mbovu wa kiutawala. kuwapokea watu mimi sioni kama ni kosa, watajifunza philosophy mpya.
 
Back
Top Bottom