CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

CHADEMA kilichofanyika Monduli ni unafiki mkuu

Mtume Mohammad (SAW) katika Quran takatifu aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki....................................................................................................................

CHADEMA tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Unazungumzia siasa (politics) au dini/imani (religion/faith)? Naona unachanganya unayotegemea yatokee ktk siasa kwa kutumia misingi ya kidini. Hiyo haitawezekana hata siku moja.

Huko CCM umejiuliza kwa nini Wasira anapewa thamani? Mtu aliyehamia NCCR baadaye angestahili kupewa Uwaziri ktk CCM?

Hebu tujaribu kusumbua vichwa kabla ya kuandika mambo marefu kama haya.
 
sikiliza mkuu hapa ni vita na mpango ni kushinda vita upo mpaka hapo? lowasa ni askar wa upande wa adui anataka kulipiza kupitia chadema shida iko wap? lengo ni kumwondoa ccm madarakani kwa hyo chadema wako sahih. zito mpango wake ulikuwa kudhoofisha jeshi la ukomboz kwa kupeleka siri kwa adui yetu ndio mana cdm walimpiga chini nadhan umenielewa
 
mtume mohammad (saw) katika quran takatifu aliainisha tabia kuu tatu za mtu mnafiki.

Kwanza, mtu mnafiki akizungumza husema uongo.

Pili, mtu mnafiki akiahidi hatekelezi

tatu, mtu mnafiki akiaminiwa hufanya hiyana.

Chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kimetuonesha sifa hizi za mnafiki dhahiri kwenye sakata hili la kuwapokea kwa mbwembwe madiwani waliotoka ccm monduli.

Madiwani hawa wametoka ccm kufuatia kukatwa jina kwa waziri mkuu 'mstaafu' edward ngoyai lowassa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa kupitia ccm.

Kitendo cha kuwapokea madiwani hawa kwa mbwembwe tena huku pakitumika maneno kama "safari ya matumaini bado inaendelea" ni kitendo cha fedheha sana kwa chama.

Wakati zitto kabwe akiondoka/ akiondolewa chadema tuliona wale walioamua kuondoka nae walivyoitwa kila jina baya mitandaoni na hata baadhi ya viongozi walijitokeza kuwakandia waziwazi.

Tumeona namna gani edward ngoyai lowassa alivyotukanwa kila tusi na viongozi wa chadema. Ameitwa mwizi, fisadi, , mnyang'anyi na majina mengine mengi. Na hata wafuasi wake 4u movement tuliona walivyopewa maneno mabaya humu.

Tumeona viongozi wa chadema wakiponda tabia ya kupokea wanachama waliokimbia vyama kwa sababu ya migogoro ya kimaslahi mara kwa mara.

Kwa hayo machache najiuliza hivi yale maneno ya kuponda watu yalijitokeza sababu walihama chadema? Kumbe kuhama ni kosa lakini kuhamia ni sahihi? Kumbe hawa wafuasi wa lowassa walikuwa wachafu walipokuwa ccm lakini wakiwa chadema ni wasafi? Hivi mtu akija chadema anasamehewa dhambi??

Tabia ya kuyarudi maneno yenu imekuwa ya kawaida sana lakini kwa hili sasa mmejifedhehesha sana. Miaka michache iliyopita mliwaita cuf kila jina baya mara ccm b, mara vibaraka, mara mas**ga nk lakini baada ya muda mkaungana nao na kuunda ukawa. Mlimfukuza kafulila kwa mbwembwe lakini leo mpo nae ukawa huku mkimsifu.
Sitashangaa kesho mkiungana na act ili tu mtimize malengo yenu.

Chadema tambueni mlichokifanya ni kitendo cha hovyo mno, mmewaonesha watanzania mlivyo walaghai na opportunist wakubwa. Mmeonesha kila tabia za kinafiki na kizandiki na msivyo na msimamo.

Tabia kama hizi zitawafanya ikulu muisikie redioni tu na kuishia kulalamika kwamba mnaibiwa kura kumbe mnajihujumu wenyewe.
jibu ni rahisi ya kuwa wameingiingia kwenye "jahazi la uhakika".safari itakuwa nzuri.
 
Hizi shule zenu za siku hizi zitaua taifa. Jambazi habadiliki kwa kuhamishwa gereza.

Fisadi unataka akuletee mfumo gani tofauti na aliozoea? Ina maana sera zilizopo hazikizi haja ya kuongoza taifa mpaka mtumie na wezi juu. Najua hakuna kiongozi wa CDM ana akili kama hizi za mitandaoni.
Sasa hivi Watanzania tunataka mtu atakayeondoa mfumo mbovu wa ccm, awe fisadi au asiwe fisadi maana mfumo huu hata mtu awe na rekodi nzuri akishaingia kwenye ccm si mzuri tena.

Ndiyo maana unaona mtu akiwa ccm ni fisadi tu. Hata Lowasa kama anauwezo wa kuiangusha ccm tunamkaribisha upinzani ilimradi tu huu mfumo utoke kwanza tuanze upya.

Tumechoshwa na utawala wa kinafiki na kizandiki wa ccm na ndiyo maana mtu yeyote anayeweza kuitoa ccm hata kama ni Boko haram au al shababu tutamuunga mkono ilimradi tu huu utawala uende kuzimu.
 
Unajiita mchunguzi halafu hujui hata maana ya quotation? Shameeee!

Nadhani ujumbe wangu umeupata vizuri. Kwamba usitake tafsiri ya unafiki ktk vitabu vitakatifu itumike ktk siasa. Huo siyo mtazamo wa wana siasa. Nimekupa mfano wa wasira.

Zamani Mchezaji wa Yanga alikuwa hawezi kuhamia Simba na hata familia za mashabiki. Leo hii vipi?

Vipi, ulitaka nikuunge mkono? Never ever! Mimi hupiga like palipo na thinking. Ktk message yako sikuona thinking yoyote! Pole sana!
 
Kamwe ni ndoto cdm kuingia ikulu. Kwa wabunge watapata. Bado hawana uongozi mathubuti. Mwenyekiti wao amejaa ukanda mno, pia wapo kimaslahi sana na waongo kweli kweli.

simple mind lete hoja ukanda ndo nn?
 
Ccm naona wanapata shida sna wanavyoona madiwani wa monduli kuhamia chadema,na bado tulieni,mleta uzi naona kajifunzia siasa ukubwani,

Hata hivyo hajafaa kuitwa mwanasiasa.Na acha tu yeye kuwa mwanasiasa hata uwezo wa kushusha uzi unaojitegemea humu Jf.bado. Aendelee kusoma na kuchangia posts za wengine. Lazima aelewe kwenye siasa hayupo rafiki wala adui wa kudumu. Kwani huko kwao ugambani wanapowapokea wanachama wanaotokea upinzani huwapokea kimya kimya? Hazisikii nyodo za Nape anapowafuma kwenye mikutano ya hadhara?
 
"mwenyekiti anazo taarifa nyeti kuhusu lowasa ambazo haziwezi kuwekwa hadharani"........mkapa.
 
Shukran sana mkuu wengine hawalijui hilo kuwa siasa ni mahesabu, hata UKAWA wakikosea mahesabu itakula kwao na bahati huwa haiji mara mbili.
Lowassa ni bahati kwa Chadema daah!!! Sasa itakuaje kwenye ile orodha ya mafisadi ina maana Slaa muongo?
 
Siasa ni kuviziana. Magamba mtakoma. Mnalalamika kwa nini watani zenu wanapikea wanachama wenu? Mlitakaje. Siasa ni kutumia kila opportunity inayokuja mnele yako kumshindwenzio. Unakumbuka alivyosema Mwandosya? Kwamba ilibidi wamtukane Warioba km mbinu ya kupata ushindi jtk bange la katiba? Vumilia tu. Hiyo ndiyo siasa Hakuna mambo ta Yesu waltume lwenye siasa. Kamanda hii mesage ni kwa hilo gamba lililoleta uzi huu.

Mi nilidhani siasa ni ukweli na kuwaletea maendeleo wananchi kumbe nu kuviziana! siwaamini tena wapinzani.
 
Kwa hiyo Lowassa siyo fisadi tena ni mtu makini anayeuchukia ufisadi anataka kuwakomboa Watazanzia?

Hakuna mkombozi CHADEMA, lile ni genge la maoportunist wanaomendea kuiongoza hii nchi.
Nimewashushia heshima yangu yoote.
 
CCM itaangukia pua maeneo yenye nguvu ya Lowassa
- itashindwa vibaya Arusha na Manyara sababu ya influence ya lowassa
- itaangukia pua mkoa wa shinyanga sababu ya nguvu ya Hamis mgeja- muumini wa Lowassa
- itaangukia pua Simiyu kutokana na nguvu ya Nzoka ya Malyenge -Andrew chenge
-hali in mbaya Kagera sababu ya Karamagi na Tibaijuka
-hali tete Ruvuma nguvu ya nchimbi
Hali tete Geita kijana Msukuma amenuna

Endeleza orodha
 
chilli,nafikiri umesahau rais anapowapokea wanachama wa upinzani na MANENO yatamkwayo,Siasa siku zote ni maslahi hakuna kingine
 
chilli,nafikiri umesahau rais anapowapokea wanachama wa upinzani na MANENO yatamkwayo,Siasa siku zote ni maslahi hakuna kingine

Kwa nini mnachukulia matendo ya CCM kama mfano wa kuigwa?
 
Nasaha Kuntu kwa waliokuwa wapambe wa Lowasa: "Aman Abeid Karume, ambaye
alikuwa Rais wa Zanzibar,
anasemekana kuwa aliwaambia
wajumbe kwamba wafanye
mambo kama watu wazima, kwa
kuwa kuna mambo ya mtu
yanaweza kuzungumzwa
hadharani, lakini kuna mengine
yanahitaji staha ili kuepuka
kudhalilishana."

Source: Mwananchi news paper

Amri ya Mkapa ilivyozima vurugu NEC
 
Nimepata hofu kubwa na hawa CHADEMA, kumbe wako tayari kufanya lolote, ama kushirikiana na yeyote kwa ajili ya kupata nafasi ya kutuongoza. Watu hawa ni hatari kama walivyo wenzao wa CCM. Tena hawa wanaweza kuwa hatari zaidi.
 
Back
Top Bottom