CHADEMA itashinda kwa kishindo Arumeru - Dr Slaa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba chama hicho kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika hivi karibuni.Dr Slaa amesema chama chake kina nguvu kubwa jimboni humo na katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 chama chake kilifungua matawi 69 yaliyo hai mpaka leo katika kila kona ya jimbo hilo.
Dr Slaa amesema CHADEMA ilijifunza mengi katika jimbo la Igunga na kutahadharisha vitendo vya ugawaji rushwa kurubuni wapiga kura kamwe havitavumiliwa Arumeru.Pia alisema chama chake kimejipanga kutoa elimu kubwa ya uraia kwa wananchi wa Arumeru mashariki kupitia kampeni mara zitakapozinduliwa.Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu.

SOURCE:MTANZANIA
 
Tuna mwamini sana Dr Slaa!
Wameru ni wajanja sana kwa mambo mengine, sidhani kama wanaweza kuendelea kuiamini ccm, ambayo kadiri siku zinavyosonga mbele inazidi kuhitaji oxygen zaidi ya kuipa uhai!
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba chama hicho kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika hivi karibuni.Dr Slaa amesema chama chake kina nguvu kubwa jimboni humo na katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 chama chake kilifungua matawi 69 yaliyo hai mpaka leo katika kila kona ya jimbo hilo.
Dr Slaa amesema CHADEMA ilijifunza mengi katika jimbo la Igunga na kutahadharisha vitendo vya ugawaji rushwa kurubuni wapiga kura kamwe havitavumiliwa Arumeru.Pia alisema chama chake kimejipanga kutoa elimu kubwa ya uraia kwa wananchi wa Arumeru mashariki kupitia kampeni mara zitakapozinduliwa.Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu.

SOURCE:MTANZANIA

Nimeipenda hii inayosema ''Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu''
Inabidi vyama vyote vitoe ahadi hii,ule ****** wa Igunga usijirudie tena!!
 
Sisi yetu macho lakini Slaa, asijiaminishe sana na ushindi Arumeru.
 
Niseme hivi, kama kuna mti kakwamba kumalizia ka-kibanda kake pengine mabati yamepungua au hela ya koleo imekuwa tabu basi apige kambi Arumeru Mashariki mapema! Zitamwagwa hela za kufa mtu pale.

Na ningependa sana kuamini Dr Slaa anajua sakarasi zinatakavyochezwa. Kama 2010 Sumari alishinda bila ya kufanya campaign yeye binafsi leo hii mwanae itakuwaje? Hii ngoma bana itakuwa ngumu sana na ukiingiza vile vita vya kimeru ndio kabisa.
 
Nguvu ya umma, chadema iko juu..CCM wangeacha kuweka mgombea wao maana wataaibika safari hii..Sumari mwenyewe alichakachua kura za 2010
 
Sisi yetu macho lakini Slaa, asijiaminishe sana na ushindi Arumeru.

Mkuu mshindi anatakiwa apatikane katika uwanja wa haki.Ule ****** nilioshuhudia Igunga na Uzini unaogawa watu kwa misingi ya udini unapaswa utokomezwe.Tutalibaka Taifa letu bila sababu kwa siasa za kihuni kama hizo za Udini
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amewahakikishia wapenzi na wanachama wa CHADEMA kwamba chama hicho kitashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika hivi karibuni.Dr Slaa amesema chama chake kina nguvu kubwa jimboni humo na katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 chama chake kilifungua matawi 69 yaliyo hai mpaka leo katika kila kona ya jimbo hilo.
Dr Slaa amesema CHADEMA ilijifunza mengi katika jimbo la Igunga na kutahadharisha vitendo vya ugawaji rushwa kurubuni wapiga kura kamwe havitavumiliwa Arumeru.Pia alisema chama chake kimejipanga kutoa elimu kubwa ya uraia kwa wananchi wa Arumeru mashariki kupitia kampeni mara zitakapozinduliwa.Dr Slaa ameahidi kampeni safi na za kistaarabu.

SOURCE:MTANZANIA

well said dr. Chakuongezea this time hakuna kugawa mahindi ya njaa.
 
Hata Uzini Slaa alisema CDM itashinda kwa kishindo!!!
Labda nako CCM walichakachua matokeo!!
 
Sisi yetu macho lakini Slaa, asijiaminishe sana na ushindi Arumeru.

Mkuu, Comment yako inaonyesha unaamini CDM wanaweza kuliotea hilo jimbo, ingawa unatoa tahadhari kwao.
Kwa mbali unaonekana kuwa muumini wa demokrasia, ni miongoni mwa masalia wachache ktk CCM.
 
Back
Top Bottom