CHADEMA inapokea ruzuku kama kawaida, hawajaigomea

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
Ule usemi wa kuwa boss hanuniwi unaendelea kudhihirika ndani ya Chadema. Ambao walisema hawautambui uchaguzi hivyo chochote wanachopata kutokana na uchaguzi huo hawatakipokea.

Lakini kwenye pesa imekuwa tofauti kwani hivi sasa wanawinda 109M kila mwezi toka November na hawajazikataa.
===
Miezi miwili baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, vyama sita vyenye sifa ya kupata ruzuku vimeanza kuneemeka baada ya kuingiziwa mgawo wa fedha na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Vyama ambavyo vimevuna fedha hizo za mgao wa ruzuku hiyo unaotokana na idadi ya wabunge, madiwani na kura za urais ni pamoja na CCM, Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, NCCR-Mageuzi na kile cha Democratic Party.

Kwa mujibu taarifa ambazo gazeti hili linazo, chama kinachoongoza kwa kuzoa ruzuku hiyo ni CCM yenye wabunge 354 ambacho kimepata zaidi ya Sh1.33 bilioni, Chadema ‘inayohesabiwa’ kuwa na wabunge 20 imepata Sh109.68 milioni, ACT Wazalendo yenye wanne kimepata Sh14 milioni na CUF yenye mbunge mmoja ikipata Sh5.7 milioni.

Vyama vingine vinavyopata ruzuku kwa idadi ya kura za madiwani ni pamoja na NCCR Mageuzi kilichoambulia Sh316,937, huku DP ikiambulia Sh63,387.


Screenshot_20210115-072105_Chrome.jpg
 
Wanachopata kutokana na uchaguzi! sasa uchaguzi umeisha wacha wapokee! kwani unafikiri wangenyimwa wangehoji?
 
Lissu kaitia hasara Chadema ilikuwa inapokea ruzuku milioni 300 kwa mwezi kuja Lisu imekuwa milioni 100 kaitia Chadema hasara ya milioni 200 kila mwezi ina maana kwa miaka mitano Chadema itakuwa imepoteza bilioni 6.

Lisu Katia hasara ya bilioni sita kwa kugombea kwake.

Lissu ueleze hiyo hasara utaifidiaje halafu ulikimbia ukakitelekezea chama madeni umemwacha Mbowe kwenye wakati mgumu hadi kakonda hadi macho sio vizuri ulichofanya.
 
Pesa za ruzuku ndio sabuni ya roho? Au ni mtego wa panya kuingiza waliomo na wasiohusika?

Pesa hiyo ndio kutambua uhalali wa akina Covid-19.

Njaa njaa ni adui wa haki.
 
Waliisema hswautambui uchaguzi ruzuku inayotokana na uchaguzi mbona wanaitambua?
Ahaa, sasa naona kauli inaanza kubadilishwa taratibu. Hapo tumeelewana. Hela hata kama ni za shetani zinapokelewa tu.
 
Back
Top Bottom