CHADEMA ina mtaji mkubwa kisiasa kuliko CCM na ACT wazalendo, ruzuku na madaraka visiwaondoe kwenye reli

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Siasa Ni mkakati, siasa ni kujua mapungufu ya mpinzani wako, siasa safi nikuweka wananchi mbele nakuzika matamanio binafsi kwa mgongo wa itikadi.

Tangu chadema watoe tamko lakuwafukuza viongozi na wanachama 19 mashambulizi toka ACT na CCM yamekuwa mengi sana.

Hakuna linalofanywa bila kuitaja chadema, adui wa ACT amekuwa ni Chadema na wananchi kwa ujumla na si CCM Tena.

Kauli mbiu iliyopo Sasa Ni umoja wa Taifa na Mambo ya Tanzania kujadiliwa Tanzania, ila hakuna anayesema wanajadili Kati ya Nani na Nani na hayo majadiliano yanafanywa wapi na wahusika ni wakina nani.

Ifike mahali tutambue wananchi Wana nguvu kuliko viongozi isipokuwa tu viongozi Wana nguvu ya dola. Chadema ina Mbunge mmoja tu bungeni lakini ina wabunge zaidi ya milioni 30 uraiani. Tunapokosa uhalali wakuongoza haimaanishi lazima tusiwe na wakuwaongoza ila lazima tusijiamini na wale tunaowaongoza.

Naamini msimamo wa chadema unafaida kubwa kisiasa kuliko msimamo wa ACT na CCM.....Wana watu nyuma yao wengine wana familia zao nyuma yao.
 
Hayo mambo ya Tanzania yanajadiliwa na nani?

Mwanzo walivyokuwa kwenye hiyo serikali walijadili nini mbona hakuna lolote la maana walilopata?

Mwisho wa siku wakatandikwa na polisi leo wamejirudisha tena kule kule kuogopa vile vipigo visiendelee.
 
Hii ndiyo gharama ya kuwa nyumbu, una mbunge mmoja tu lakini bado una ushawishi sana!!
Swali dogo lenye umuhimu: Ni tofauti ipi kimaisha u mehisi tokea tuambiwe tuko Uchumi wa kati ukilinganisha na Uchumi wa Chini tuliokuwa nao?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Chadema wawaambie wapenzi wao wawachangie! Kama waliwachangia 39m za kortini wakati ule katika 24 hours watashindwa nini kuwachangia ruzuku yote katika miaka mitano??? Watie tu tekephone number ya kywachangia!
 
Huwa najiuliza hivi Tanzania tungekuwa hatutumia Facebook na JF hivi hii chadema tungekuwa tunaiona kama tunavyoichukulia humu mitandaoni? Kwa maana huko mitaani chadema ingekuwa inazungumzwa kama ilivyo huku mitandaoni?
 
Huwa najiuliza hivi Tanzania tungekuwa hatutumia Facebook na JF hivi hii chadema tungekuwa tunaiona kama tunavyoichukulia humu mitandaoni? Kwa maana huko mitaani chadema ingekuwa inazungumzwa kama ilivyo huku mitandaoni?
Mimi pia najiuliza, hivi watanzania tungekua na tume huru ya uchaguzi na jeshi la polisi lisilopelekeshwa na akina pole pole, CCM ingekua madarakani kweli?

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
 
Mimi pia najiuliza, hivi watanzania tungekua na tume huru ya uchaguzi na jeshi la polisi lisilopelekeshwa na akina pole pole, CCM ingekua madarakani kweli?

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app

Pole sana. Asiyekubali kushindwa sio mshindani. Sisi sio CCM Lakini nakwambia JPM ameshinda na angeshinda. Nyie kazi mnazozijua Ni kubisha mpaka humu akisema mtu hoja tofauti Nanyi , hata kama kasema we Dume mtapinga jinsia zenu na kumsingizi JPM kazibadili
 
Back
Top Bottom