CHADEMA imekosa Dira? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imekosa Dira?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masatu, Jul 7, 2009.

 1. M

  Masatu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kufuatia kushindwa mfululuizo katika chaguzi ndogo za Busanda na Bihalamuro, chama cha "demokrasia" na maendeleo chadema kimepoteza dira sasa badala ya kukaa chini na kufanya tathmini ya kisanyansi mpaka kupelekea kushindwa katika chaguzi hizo, viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kura.

  Madai kama haya yamekuwa yakitolewa na chama cha wananchi cuf katika chaguzi mbalimbali lakini chadema wamekuwa wakidai kuwa cuf ni walalamishi na sasa wimbo huo unaanza kuimbwa na chadema.

  Ukweli ni Chadema kimekosa mikakati thabiti kuweza kuongoza na kubaki na kulala kila uchao, kilichobaki sasa kwa Chadema ni kurudi kwenye drawing board na kuanza upya huku wakijua siasa za Mwembe ya yanga za kulipua mabomu na kuvurumisha helikopta hazilipi na watanzania washawatukia kuwa ni chama cha kikabila na familia
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Chadema ndio wameanza kukua sasa...walikuwa wakisifiwa na CCM (walipokuwa wanajua hawana impact kwamba ni wastaarabu etc..).CCM iliposhtuka kuwa wameanza kuwa na impact wakaanza ku-hit back "Tunasubiri tamko lao" bado ya kipigo tujui ni aina gani ya leadership tunayo?? kutoka chadema.....wako ngangari au nyoronyoro...
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Does this article make any sense ama tunataka sasa kushusha hadhi ya forum kwa kuleta inssues ambazo ni below standard of this forum ? Hivi Masatu hoja ama post hii si ungaliweza kuandika kule kule ziliko za CUF ama CCM tukabana matumizi ?Ni mawazo yangu na swali tu si lazima ufuate ninavyosema mimi .
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CHADEMA ni chama ambacho hakijawahi kuongoza nchi. CHADEMA kina sera zake ambazo unaweza kuzihoji na kuzijadilia. Lakini kusema CHADEMA kimekosa dira ni upotoshaji mkubwa unaofanywa na wale wanaoonekana kuwa CCM zealots ambao wanajua kabisa kuwa chama chao, ingawa bado kinaaminiwa na Watanzania kuongoza nchi, kimekosa dira na sasa hakijui kinaipeleka nchi wapi.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna kipimo cha mada siku hizi na hasa zinazogusa Chadema!
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wewe usichague habari JF tunajadili habari zote...kama inakuumiza roho (touch) angalia uondoke...
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Uzuri umesema kuwa hayo ni mawazo yako, kwa bahati mbaya mawazo yako ni upupu mtupu! nani kakulazimisha usome "article" ambayo unadhani hai make sense? unaonaje hayo mawazo yako ukayapeleka huku kwenye thread za cuf na CCM ili "kubana" matumizi.
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Same applies kusema CCM imekosa dira ni "upotoshaji mkubwa" ambao waweza fanywa na Chadema zealots, ingawa chadema kinaweza kuwa kinaaminika na baadhi wa wananchi kimekosa dira. CCM ina sera zake na waweza kuzi hoji na kujadili.
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mh , haya mie naangalia tu tuendelee
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ya nini kupoteza muda kuangalia kitu kisicho make sense? kwa nini "usibane" matumizi kwa kusoma thread za CUF na CCM huko?
   
 11. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa ugomvi huo wana JF ...taratibu
  Labda nikuulize masatu kukosa mwelekeo na dira unamanisha nini??
   
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Kwi kwi kwiiiii teh teheeeee

  - ni kweli kimekosa dira kwa sababu sasa inataka kuwanyanganya mafisadi tonge mdomoni

  -Ni kweli imekosa dira yaani kabisaaaa inapendwa kuliko Chama dola hadi inawazidi kura katika jimbo la pembezoni mwa nchi ambapo magazeti na TV hazifiki kama B'mlo, hadi inabididi kutumia umafya kuiba kura mchana kweupe bila haya wala soni?

  - Hakika Chadema imekosa dira, yaani hadi watu wanaisikiliza na kutoka usingizini hadi kuhoji ahadi hewa kule Busanda?

  Jamani Chadema imekosa dira, heee?? hadi inaamua kuwaanika hadharani mafisadi wote wanao liangamiza Taifa? ( orodha ya mafisadi?)

  ----jamanieeee njoni niwasimulie nduguzangu jinsi chadema ilivokosa dira

  -Yaani wabunge wake wachache bungeni, lakini wamelichachafya bunge hadi wakisimama kuongea wachumia matumbo wanahaha kutaka mwongozo wa spika kuzima hoja?

  -Yaani Chadema imekosa Dira, hadi wabunge wake wanaanika uozo wa mikataba ya kifisadi ya waziri kukimbia na mihuri yetu kwenye makoti kwenda kusaini mikataba ya kifisadi hotelini tena nje ya nchi?

  kweli Chadema imekosa dira.. duu wasaidieni make huku kukosa dira kwao karibia kunambwaga chini Tembo mzimaaaaaa!

  NB: Binafsi, nazidi kuwaombea wazidi kukosa dira kama hapo juu, make kukosa kwao dira kwa aina hii, ndiyo nafuu yetu sisi walala hoi. Mungu awazidishie chadema muendelee hivo na mfike mbali
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Waishiwa bwana! Huwa hawakosi vioja. Ndivyo tulivyo.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CCM is a ruling party. But right now they do not seem to know where they are trying to steer the country. Sera zipi za CCM? Hebu zimwage hapa tuzihoji/tuzijadili.
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Chadema sio imekosa au kupoteza dira bali jambo kubwa inakuwaje wengine nasikia wamebwaga manyanga ,yaani kauchaguzi kadogo tu haka wameanza kuchawanyika na hawajui pa kushika ,inakuwaje Zitto anawaelimisha wananchi waliopiga kura kuwa wasubiri mwakani ,hivi hajui la leo lifanywe leo ,Viongozi wa Chadema wanashindwa kuwaeleza wananchi ukweli kuwa kutoka Busanda ,Kiteto huko kote matokeo yakibadilishwa ,na badala yake wanasema hapo Biharamulo ndio wamebadilishiwa matokeo. Nawambia Chadema mambo bado ,kama hawakuwashawishi wananchi kuweka sera ya jino kwa jino au sera ya KiPemba roho kwa roho basi basi siku zote CCM wataibuka videdeya ,ndio maana yake ,CCM kama hukuwakurupusha na kuwawekea ndita kikweli basi wataendelea kutesa , jiulizeni sababu ya Zanzibar kupelekwa polisi,majeshi na vifaru ,ma granade rocket launcher katika chaguzi kuu ,mpaka kufikia mapolisi kukimbia na masanduku ya kura ,wananchi waliidhibiti CCM kikwelikweli na inawabidi na nyinyi kwa nguvu ambazo mnasema mnazo basi muifikishe CCM kutumia nguvu hizo za ziada katika kuulinda wizi wao vinginevyo inaposemwa CUF ni Chama kikuu Cha Upinzani Tanzania Nzima ,msione wivu na kupinga ,maana kufika CCM kuita Jeshi na mapolisi kulinda wizi basi ujue CUF ni tishio la kweli sio mchezo katika kuing'oa CCM madarakani.
   
 16. M

  Masatu JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mahakama ya Kadhi!
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Political bankruptcy
   
 18. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Really? thubutu all muslims votes? I think politics means people.....people is equvalent to "MTAJI"
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Political bankruptcy2
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Frustated Mind
   
Loading...