Hivi kwani ni CHADEMA peke yake iliyoshindwa katika uchaguzi wa Biharamulo??
Hapana mwalimu, ni Chadema iliyo shinda B'mlo ikaporwa ushindi na mafya group kupitia kibaraka wao NEC!
Hivi kwani ni CHADEMA peke yake iliyoshindwa katika uchaguzi wa Biharamulo??
Kufuatia kushindwa mfululuizo katika chaguzi ndogo za Busanda na Bihalamuro, chama cha "demokrasia" na maendeleo chadema kimepoteza dira sasa badala ya kukaa chini na kufanya tathmini ya kisanyansi mpaka kupelekea kushindwa katika chaguzi hizo, viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kura.
Madai kama haya yamekuwa yakitolewa na chama cha wananchi cuf katika chaguzi mbalimbali lakini chadema wamekuwa wakidai kuwa cuf ni walalamishi na sasa wimbo huo unaanza kuimbwa na chadema.
Ukweli ni Chadema kimekosa mikakati thabiti kuweza kuongoza na kubaki na kulala kila uchao, kilichobaki sasa kwa Chadema ni kurudi kwenye drawing board na kuanza upya huku wakijua siasa za Mwembe ya yanga za kulipua mabomu na kuvurumisha helikopta hazilipi na watanzania washawatukia kuwa ni chama cha kikabila na familia
Ooh really? kwa hiyo maneno ya marehemu yashakuwa msahafu... hang on a minute... tunae marehemu mwingine anaitwa Chacha Wangwe yeye alisema Chadema ni chama cha kikabila na familia nae mka mkolimba! how about that?
viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kuraQUOTE said:Mtoa mada naona umechanganya mambo, mimi naona siyo kwamba wanasingizia, bali NI KWELI WANAIBIWA!. we have to be clear on the fact!
Ya nini kupoteza muda kuangalia kitu kisicho make sense? kwa nini "usibane" matumizi kwa kusoma thread za CUF na CCM huko?
Sina kumbukumbu kamili za mwaka 1995 japo ni kweli. Kuhusu mwaka 200 ni ukweli wa asilimia 100 maana katika maeneo yote alipopita Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba na mgombea Mwenza, Mh. Nasor, Chadema walishiriki kwa hali na mali na kuna maeneo Chadema walitumia magari yao, hoteli zao, mfano Kilimanjaro, Hotel Aishi ya Machame na Keys ya Moshi mjini na magari yote ya Chadema yalitumika. Kwa Moshi hata gari la Lipumba Land Cruiser short chases aliyosafiri nayo nchi nzima ikiwa imechoka alilazimika kuiacha na kukabidhiwa gari ingine yenye hadhi. Ilikuwa ni kwa nia njema na pengine kwa Chadema pia kutaka Lipumba asaidie kampeni za wagombea wao wa Ubunge, Philemon Ndesamburo kwa Moshi mjini na Freeman Mbowe kwa Hai.
Lakini hali ya sasa haishirii neema kwa mageuzi hata kidogo. CUF na Chadema sasa wanaangaliana kama mahasimu wakuu, tena kuliko hata ilivyo kwa CCM.
Ni Kweli waliunga mkono vyama vyote vilivyojitokeza kugombea urais wakati ule kabisa chini ya Bob Makani waliunga mkono hata mwaka
Mugo"The Great";514293 said:From CCM perspective kuongeza jimbo ni mafanikio(hii ni kweli) lakini from another angle CCM inapoteza umaarufu ndio maana ushindi wa 80-90% sasa hivi haupo. Unajua mti unaweza kuwa mmoja lakini ukiambiwa uelezee ulivyo itategemea na angle uliyopo. Kwako wewe kuongeza jimbo ni mafanikio (you are entitled to it) na kwangu mimi kupungua kwa %age ni sign ya decline. That's why katika kupima performance kuna A+, A, A-, B+, B n.k.
Lakini amini usiamini "ENZI ZA CHAMA KUSHIKA HATAMU aka UTAMU ZINATOWEKA"
masatu jibu hoja usilumbane kwa kutumia vina na nahau za mipasho eleza kisayansi nini kimekufanya uone na utuaminishe kuwa chadema haina dira
Masatu, isiwe tabu narekebisha namba. Miaka 48 ya uhuru na miaka 32 ya CCM na miaka ya 16 ya TANU baba ya CCM tangia uhuru. Naomba ujibu hoja .