Kufuatia kushindwa mfululuizo katika chaguzi ndogo za Busanda na Bihalamuro, chama cha "demokrasia" na maendeleo chadema kimepoteza dira sasa badala ya kukaa chini na kufanya tathmini ya kisanyansi mpaka kupelekea kushindwa katika chaguzi hizo, viongozi wa chama hicho hivi sasa wanamtafuta mchawi kwa kusingizia kuibiwa kura.
Madai kama haya yamekuwa yakitolewa na chama cha wananchi cuf katika chaguzi mbalimbali lakini chadema wamekuwa wakidai kuwa cuf ni walalamishi na sasa wimbo huo unaanza kuimbwa na chadema.
Ukweli ni Chadema kimekosa mikakati thabiti kuweza kuongoza na kubaki na kulala kila uchao, kilichobaki sasa kwa Chadema ni kurudi kwenye drawing board na kuanza upya huku wakijua siasa za Mwembe ya yanga za kulipua mabomu na kuvurumisha helikopta hazilipi na watanzania washawatukia kuwa ni chama cha kikabila na familia
Masatu pole sana nduguyu yangu.
Najua unakazi kubwa sana ya kuwaonyesha mabosi wako kuwa huwa una-post na kukilinda chama chako cha CCM-fisadi. Nilikuwa nategemea utoe post elimishi ila bado umejikita kwenye siasa za kiimla kama vile huoni yanayojiri Tanzania na umasikini wa kila kona baada ya sera za serikali ya CCM kushindwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka zaidi ya 30.
CCM hawajakosa tu dira ila hawana mwelekeo wala haijui wanakwenda wapi, hawana uongozi wala hawala mipango ya kimaendeleo ya nchi zaidi ya mipingo ya kuiba kura kutumia NEC.
Chadema wana DIRA na mwelekeo mzuri sana, ni chama ambacho kinakuwa na kuwekeza mtaji wake kwa wananchi wote na kutumia rasilimali watu ili kuweza kumkomboa mwananchi aliyesahaulika baada ya kulipa kodi kwa mika 50 na kuliwa na kundi dogo. Chadema yenye demokrasia ya kweli lazima ipitie kwenye mikiki mingi ya siasa hasa hili la kudai kubadilika kwa Tume Ya Taifa ya Uchaguzi ni lazima kubadili mfumo mzima na uendeshaji wa NEC. Sisi kama Chadema tunaelewa hilo ni gumu sana kwa CCM kukubali kwani huu ndio muhimili wa ninyi washika pembe wa CCM mnapotegemea na kutoa lugha za kejeli na jeuri hata kudiriki kutukana wananchi.
Chadema imejipanga vizuri kupambana na dhuluma na proganda zenu, tupo mstari wa mbele kuelimisha wananchi na kuhakikisha tunajenga base nzuri iliyo huru na yenye demokrasia ya kweli isiyo ya kiimla wala ng'ang'anizi madarakani hata kuua kama mnavyofanya ninyi. Ni wajibu wa Chadema kuhakikisha wananchi wanajua nini wajibu wa serikali kwao baada ya wao kulipa kodi na kuchagua viongozi. Ni wajibu wa chadema kuwaelimisha wananchi hatari ya viongozi wanaoingia madarakani kwa kuiba kura, rushwa, ghiliba na aina yeyote ile ya dhuluma, hili ndio tunda na zao la ufisadi, rushwa na utawala mbovu uliojaa mikataba mibovu na utendaji mbaya na usiofaa. Ni lazima wananchi wajue hali hii haitokwisha bila kuachana na viongozi wanoingia utawalani kwa kutumia njia badhirifu.
CCM chama chako kimejikita kwenye dhuluma, ndio maana hata wewe unashabikia kwa sababu unafaidika na wizi huu, ila umesahau kuwa badala ya kupambana na Chadema wanaopigania haki pamoja na yako, ungegeuka uwaambie watawala wako kuwa hata sisi(CCM) tupo ndani ya hili behewa.
Behewa la barabara mbovu, hospitali mbaya, elimu duni, wizi wa maliasili yetu, mikataba mibovu nk. Waambie kuwa sote ni wahanga wa haya madhila.
Masatu miaka hamsini sasa bado hatuna Hospitali icon ya taifa, Masatu miaka 50 hatuwezi hata kukusanya kodi zetu, hatuwezi hata kusaini mikataba kwa ajili ya wananchi wetu kisingizio hatuna wataalamu.
Miaka hamsini bado kuna shule hazina waalimu, zahanati hazina dawa na wahudumu. Jiji halina maji na umeme wa uhakika, CCM haina mwelekeo dira wala majibu. CCM haina chakujivunia ilichokifanya inashindana kutoa ahadi na mtoto mwenye miaka 18. Je mzee wa miaka 50 hana alichokifanya bado anaahidi apewe muda zaidi afanye alichoaahidi miaka 40 iliyopita.
Masatu wageukie wenzako mwelezane ukweli, kilio chetu ni cha kweli na mabadiliko tunayoyataka ni ya kweli na tunaweza na tutafanya.CHADEMA ndio chama chenye dira na nia ya kweli kumboa mwananchi, chama cha wananchi wote na mali ya wote kipo kwa ajili ya wote kwa maendeleo na ulinzi wa mali asili zetu kwa ajili ya kizazi hiki na kizazi kijacho.