Mkuu Kilaza, asante!, ni mimi na account yangu haijabakwa!, ila nakiri sometimes if not most of the times, Pasco wa jf, huwa ni mpuuzi fulani!, ila 2015 November tutakutana humu kukumbushana baadhi ya maupuuzi, tulioshauri, yakapuuziwa!.
Naombea sana hili lako jina, liwe ni jina tuu, ila wewe mwenyewe usiwe kama jina lako, kwa sababu tunatofautiana sana uelewa wa issues humu ndani, werevu sikuzote huwa ni wasikilizaji wazuri wa ushauri!, hata akiambiwa na kichaa kuwa nyuma kuna nyoka, mwerevu atageuka!, mjinga ndio atapuuza kwa sababu aliyemwambia ni mwenda wazimu!.
Haijalishi huyo mwendawazimu aliwahi kuwafanyia nini nyuma, kinachotakiwa kufanywa na ni kusikiliza na sio lazima ku act!.
Mimi mwenyewe hapa nilipo sina chama, lakini nina marafiki zangu kibao CCM, Chadema, CUF na NCCR!, najua 100% sure ndani ya UKAWA kuna wana Ukawa wa ukweli na kuna "wasanii" tena ni wakubwa tuu, ila wako kwenye "payroll" ya wale "jamaa zetu", mimi nawajua fika!, kwa vile siko Chadema, nikiwashauri Chadema kuwa makini, kuwa ndani ya kundi lao la Mamba "Ukawa" na kenge wapo!, wanaweza wakapuuza!, jee unaijua kazi ya kenge kwenye kundi mamba?!. Kwa anayeijua kazi ya kenge kwenye kundi la mamba, hawezi kuambia kuna kenge na safari ikaendelea!, akapuuzia, eti tuu kwa sababu mtoa taarifa za kenge ndani ya kundi la mamba naye ni kenge!.
Asante.
Pasco.