VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Jana,Zitto Zuberi Kabwe, alikuwa kwenye kipindi cha Makutano kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Magic FM.Kipindi husika huendeshwa na watangazaji wawili: Fina Mango na Sebo. Kipindi huanza saa 9 hadi 12 kila siku ya Jumamosi. Na jana ikawa vivyo hivyo.
Katika mahojiano yaliyoelekezwa kwa Zitto na Fina Mango,Zitto amesikika akisema kuwa hadi jana alikuwa hajapokea barua yenye tuhuma zake 11 ambazo anatakiwa kuzijibu ndani ya siku 14 kwasababu gani asivuliwe uanachama wa CHADEMA. 'Hadi ninapozungumza hapa,bado sijapata barua yenye tuhuma zangu' alisema Zitto.Kweli?
Ni katika misingi ya kisheria,barua huanza kufanya kazi pale inapomfikia mlengwa. Ndiyo kusema,Zitto bado hajui tuhuma zake. Kwahiyo, hawezi kuzijibu. Hivyobasi,siku 14 bado hazijaanza kuhesabiwa. Huu ndio ukweli wenyewe. Kwa kufanya hivi,CHADEMA haicheleweshi mchakato wake yenyewe?
Mpeni Zitto na wenzake tuhuma zao ili wazijibu na mtoe uamuzi. Au kama mmesamehe kichinichini sawa. Pia yawezekana kwenye siasa. Hamtakuwa wa kwanza.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Nakala kwa: Tumaini Makene Molemo Mungi Ben Saanane, Yericko Nyerere na wengineo

Last edited by a moderator: