CHADEMA kupokea ruzuku ni rasmi mmewatambua "Wabunge 19" Hivyo mmeutambua Uchaguzi-2020

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
"Uongozi wa Chadema,kuweni wawazi kwa wafuasi na wanachama wenu!"....

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ndio yenye jukumu la kugawa ruzuku ya kila mwezi kwa vyama vya siasa vyenye sifa kwa mujibu wa Sheria.

Ruzuku ya vyama vya siasa ni fedha zinazotolewa na Serikali kwa vyama vya siasa kwa ajili ya kusaidia shughuli za uendeshaji wa vyama hivyo. Vyama vinavyopata ruzuku ni vile vilivyopata angalau asilimia tano ya kura zote halali zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu na vyama vyenye Wabunge au Madiwani.

Kigezo kinachotumika ili chama kiweze kupata ruzuku ni kuangalia matokeo ya uchaguzi kuona kama chama kimepata asilimia tano ya kura au kama chama kimeshinda nafasi za ubunge au udiwani, kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 16 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, namba 5 ya mwaka 1992.

Chama kinachopata ruzuku kinaweza kupoteza sifa ya kupata Ruzuku iwapo kitapoteza kwa namna yoyote ile mbunge au diwani anayepelekea chama hicho kupata ruzuku. Pia chama kitapoteza sifa iwapo kitafutiwa usajili wake wa kudumu. Chama kikipoteza sifa ya kupata ruzuku kitaondolewa kwenye orodha ya kupata ruzuku.

JamiiForums1879127103.jpg

"Mwamba" na "Mwambafy".
 
Wanaitukana jamii ambayo ndio iliwaweka kwa muda hivyooo....

Hawana jinsi, lazima wajirudi, watubu, ndio maridhiano yaendelee!
 
Kama Chadema walipata asilimia tano ya kura, na wana mbunge kule bungeni, Aida Kenan, hiyo inaweza kuwa sababu kwao kupokea ruzuku, ni haki yao, sio hisani.

Suala la kuwatambua covid halihusiki na chochote hapo, wale walijiamulia kwenda bungeni kwa matakwa yao, kinyume na chama chao, wakaapishwa kinyemela, mwishowe wakafukuzwa na chama chao.
 
Magufuli 84%

Lisu 13%

Wabunge Mdee, Matiko, Bulaya, Mwaifongo waligombea Kwenye majimbo hivyo kura zao zinazalisha Ruzuku ya Chadema, watakapoondolewa Ruzuku ya Chadema itapungua
 
Fake news imewanasa wajinga wa bukusaba huku hamna habar na mamayenu anayeenda kukabidhiwa kadi ya chadema kule moshi.
 
Magufuli 84%

Lisu 13%

Wabunge Mdee, Matiko, Bulaya, Mwaifongo waligombea Kwenye majimbo hivyo kura zao zinazalisha Ruzuku ya Chadema, watakapoondolewa Ruzuku ya Chadema itapungua
Magufuli 84% za kutengeneza ambazo huwezi kuziona kwenye tovuti ya tume.
 
Back
Top Bottom